Mh. Mbunge - Sintatoa siri za bunge

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
762
Wana JF kwanza nawapongeza kwa u serious humu jamvini kwenye kujadili maswala kwa ajili ya maslahi ya taifa letu. Mungu Ibariki Tanzania.

Naombeni mnijuze kitu kimoja wakati wabunge wanapokula kiapo pale bungeni. Ningependa pia maoni ya wabunge ambao pia ni members wa humu jamvini yangeweza kuwa na sense zaidi.

Wakati mbunge ana apa kuna maneno mengi sana anasoma, Sina shida na yote isipokuwa hili moja. "SINTATOA SIRI ZA BUNGE"

1. Tulikupitisha kuwa mgombea ubunge kwenye chama chetu, tukafanya wote kampeni, tukakupigia kura, tukalala wote ofisi za halmashauri kusubiri matokeo, ukatangazwa kuwa mbunge mteule na kisha ukaenda Dodoma kuapa.

2. Kwenye kula kiapo unasema hutatoa siri za bunge nje. SIRI ZIPI HIZO? Sisi ndo tumekutuma ukatuwakilishe huko bungeni mana wote tusingeweza kuwa wabunge. Iweje leo tena wewe mwenzetu eti kuna mambo ambayo sisi hatutakiwi kuyajua?

Lakini pia bunge huwa linaendeshwa kwa uwazi na ukweli kwa maana ya kwamba mijadala yote inafanywa live media zikiwa zinarusha kwahiyo hakuna siri yeyote. Labda kama utaniambia hutatoa siri za kamati za bunge ambazo huwa hazirushwi live. Na kamati ikikaa inakuwa siyo bunge tena ila ni kikao.

Tuwekane sawa hapo wajameni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom