Mh.mbunge Jeremiah Sumari wa Arumeru mashariki-CCM

Posho anavuta? Maana ni kodi yetu! Sheria za kazi wanasema miezi 3 unakula nusu mshahara baada ya miezi Sita unaachishwa.
 
Ukikosa vikao bila na kuwa na sababu ya nmsingi. Kuugua nadhani ni swababub ya msingi. lakini technically, yeye hajala kiapo, hivyo kuna uwezekano kuwa habanwi na hizo kanuni kwa sabbau hawaja mbunge rasmi

Kama hajawa mbunge rasmi analipwa mshahara ama halipwi?
 
wadau huyu mbunge hata hajaapishwa toka uchaguzi uishe yupo kitandani ni mgonjwa sana hivyo hatuna mwakilishi jimboni kwetu,je selikari inaonaje kama tukifanya uchaguzi mwingine tutafute muwakilishi mwingine? Sumari abaki mbunge wa viti maalum.

inatakiwa muandamane kudai uchaguzi. sumari hata kwenye viti maalum sidhani kama atafaa maana ubongo wake umevamiwa na wadudu atakuwa chizi.
 
Posho anavuta? Maana ni kodi yetu! Sheria za kazi wanasema miezi 3 unakula nusu mshahara baada ya miezi Sita unaachishwa.

Mbunge asipohudhuria mikutano mitatu automatically anakosa sifa ya ubunge. sasa kwa summari ambaye hata kuapishwa hajaapishwa na huu ni mkutano wa tano sheria sijui zinasemaje.
 
Kwenye bunge la Uingereza kulikuwa na sheria inasema kwamba kama mbunge anaumwa ugonjwa wa akili (mental illness) kwa zaidi ya miezi sita anakuwa disqualified automatically. Lakini wale wenye magongwa mengine ya kawaida walikuwa wanaendelea na ubunge. Hata hivyo, wanaharakati walilalamika kwamba huo ulikuwa ni ubaguzi. Hivyo sheria itabadilishwa mwaka huu to the effect kwamba hata mbunge akiwa na ugonjwa wa akili hatakuwa disqualified automatically baada ya miezi sita.

Kimsingi wale wanaosema kuwa mbunge asiondolewe kwa kigezo kuwa anaumwa kwa muda mrefu wana hoja nzuri tuu. Hata hivyo, hoja ya namna hiyo inaleta maswali mengi. Swali muhumu na la msingi ni kama mbunge anaumwa kwa muda mrefu to the extent hawezi hata kuhudhuria vikao vya bunge, atakuwa kweli anawatumikia wapiga kura wake ipasavyo? Kwamba kwa vile mbunge anaumwa ugonjwa wa muda mrefu basi haki ya wanapiga kura kuwakilishwa inahairishwa mpaka mbunge atakapopona?

Nafikiri hili ni eneo gumu hasa kuhusiana na haki za wanajimbo. Labda niulize ni wakati gani haki za wapiga kura zina-override matatizo ya afya ya mbunge? Kitu kingine, kama mbunge anasumbuliwa na ugonjwa kama terminal cancer, bado atakuwa anahangaika kuhakikisha kuwa hataadhirika kifedha kama akiacha ubunge mapema?

Mbunge mgonjwa angeweza kujiuzulu kwa sababu anajihisi hawezi tena kuwatumikia wanajimbo wake ipasavyo lakini anaweza asifanye hivyo kwa sababu za kifedha ambazo labda zitatumika kutibu ugonjwa unaomkabili. Lakini wakati huo huo inabidi tufikirie jinsi ya kuwalinda wanajimbo kwa sababu wanaweza wasiwe na mwakilishi kwa kipindi chote cha miaka mitano. Hii ni bila hata kufikiria itakuwaje kama huyo mbunge mgonjwa akachaguliwa tena baada ya hiyo miaka mitano.

Tunaweza kulinganisha hili suala la mbunge na lile la rais wa Nigeria aliyekuwa anaumwa?
 
wadau huyu mbunge hata hajaapishwa toka uchaguzi uishe yupo kitandani ni mgonjwa sana hivyo hatuna mwakilishi jimboni kwetu,je selikari inaonaje kama tukifanya uchaguzi mwingine tutafute muwakilishi mwingine? Sumari abaki mbunge wa viti maalum.

wewe nadhani huwa unasoma machache katika vyombo vya habari acha huyu ambaye anasemekana kachaguliwa hajaapishwa tunaywe waziri yupo katika matibabu kabla ya bunge la bajeti mpaka leo hawajathubutu kumuondolea uwaziri na kumuachia ubunge ije iwe huyu jamani watanzania naibu waziri ndiyo anayeongoza wizara
 
Kwenye red. Kwani huyo sumari ni wa kike?
 
wadau huyu mbunge hata hajaapishwa toka uchaguzi uishe yupo kitandani ni mgonjwa sana hivyo hatuna mwakilishi jimboni kwetu,je selikari inaonaje kama tukifanya uchaguzi mwingine tutafute muwakilishi mwingine? Sumari abaki mbunge wa viti maalum.

Yes. Kama ccm bado wanamhitaji wampe viti maalum, naunga mkono wazo lako maana Wameru wanaonekana mazuzu!
 
wewe nadhani huwa unasoma machache katika vyombo vya habari acha huyu ambaye anasemekana kachaguliwa hajaapishwa tunaywe waziri yupo katika matibabu kabla ya bunge la bajeti mpaka leo hawajathubutu kumuondolea uwaziri na kumuachia ubunge ije iwe huyu jamani watanzania naibu waziri ndiyo anayeongoza wizara

Tanzania tumelogwa hakika! Hii laana imeanzia wapi? Ina maana hakuna maombi yanayoweza kuvunja hii laana tukajitambua? Nadhani tayari Mungu ametutupa kisogo maana hii siyo kawaida wajameni!
 
Wizzo, sio kweli kuwa Mbunge, Mhe. Jerry Solomon, hakuapishwa, siku wabunge wanaapishwa, nilikuwepo Dodoma, nilimshuhudia kwa macho yangu mwenyewe!.
Hili la kuugua, ni ubinadamu.
Nawaombeni wana jf wenzangu, wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia, ndio maana moyoni mwangu, nafsi yangu ilimlilia hata Saadam, Osama na juzijuzi Gadhafi, licha ya yoye waliyoyafanya. Damu ya binadamu ni ile ile kwa wote, nikimaanisha damu ya Ghadafi iliyeuwawa kinyama ni sawa na Damu ya Obama au ya Baba Mtakatifu!. Hivyo nawaombeni sana tusimbeze yoyote kutokana na maradhi/kuugua, tuweke ubinaadamu mbele.
Pasco
Pasco hapo hapo una potosha Jerry Summary hajaapishwa! Wakati wa kampeni na uchaguzi alikuwa mgonjwa. Tuulize sisi wanajimbo wa Arumeru mashariki. Usiropoke.
 
Kuwa mgonjwa haikupi nafasi ya kuhurumiwa kwa ubaradhuli wako, mwizi akiugua hupatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi. Mubarak alipelekwa Mahakamani akiwa kwenye machela, kama Sumari ni fisadi sheria ichukue mkondo wake kama kwa mwananchi yeyote yule. Akifa azikwe.

Kama ni kweli amekaa muda wote huo bila kuwakilisha wananchi lazima hilo jimbo lifanyiwe kazi, CCM hawawezi kuliongelea hilo kwahiyo ngoja tulifanyie kazi na halina muda mrefu tutapata muafaka wake siku si nyingi. Ngoja tuwaone kesho kama watapitisha huo mswada wao wa kipuuzi kisha tutajua la kufanya, waliokuwa wanajadili hapo Blue Perl Hotel nao wametoa tamko kwamba iwapo hao wapumbavu watapitisha huo mswaada maandamano rasmi yatakuja.
 
Wizzo, sio kweli kuwa Mbunge, Mhe. Jerry Solomon, hakuapishwa, siku wabunge wanaapishwa, nilikuwepo Dodoma, nilimshuhudia kwa macho yangu mwenyewe!.

Hili la kuugua, ni ubinadamu.

Nawaombeni wana jf wenzangu, wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia, ndio maana moyoni mwangu, nafsi yangu ilimlilia hata Saadam, Osama na juzijuzi Gadhafi, licha ya yoye waliyoyafanya. Damu ya binadamu ni ile ile kwa wote, nikimaanisha damu ya Ghadafi iliyeuwawa kinyama ni sawa na Damu ya Obama au ya Baba Mtakatifu!. Hivyo nawaombeni sana tusimbeze yoyote kutokana na maradhi/kuugua, tuweke ubinaadamu mbele.

Pasco

You missed the point...swala sio kubeza ugonjwa wa mbunge bali ni uwakilishi wa wanajimbo la Arumeru Mashariki full stop.

Ingekuwa vyema kama ungemalizia kwa kutoa mtazamo wako wenye kujenga ktk hili na sio kutoa hoja out of context.

Nitafarijika utawaonyesha wanajukwaa hapa kuwa mbunge anapokuwa mgojwa kwa muda mrefu (kiasi cha kushindwa kufanya majukumu yake ya uwakilishi) hakuaathiri uwakilishi wa wanajimbo husika.

Nikirejea mchango wako ni kwamba unachosema ni hivi... swala la uwakilishi kwa sasa halina maana sana... kwa sababu mbunge ni mgonjwa....na kwamba as long as mbunge ni mgojwa basi wanajimbo wa Arumeru wasubiri...nashauri uongeze ktk mchango wako kuwa waendelee kusubiri kwa muda gani?
 
Pasco, suala hapa si kuapishwa au kutokuapishwa. Mantiki ni je mbuge huyo anafanya kazi za kibunge kama alivyochaguliwa na wananchi? Sheria zinasema nini juu ya mbunge aliye mgonjwa kwa muda mrefu? Kama sheria imedokeza na watekelezaji wa sheria hawataki kuzitekeleza, basi huko ni kuwanyima wananchi uwakilishi. Lakini kama hakuna kipengele chochote kinachomtaka mbunge ajiuzulu endapo ataugua kwa muda mrefu, basi hayo ni mapungufu yaliyomo katika sheria zetu na hususani katiba. Katiba mpya inaweza kuja, tuwasilishe mapungufu hayo.

Hapo umenena,ndicho cha msingi
 
Pasco hapo hapo una potosha Jerry Summary hajaapishwa! Wakati wa kampeni na uchaguzi alikuwa mgonjwa. Tuulize sisi wanajimbo wa Arumeru mashariki. Usiropoke.
Captain, kuapishwa ni Dodoma na sio jimboni Arumeru. Wakati wa kuapishwa tulikaa naye hoteli moja pale Dodoma Hotel na alikuwa na mkewe!. Need I say more?.

Rejea katiba ya JMT, mbunge ambaye hajaapishwa, sio mbunge kikatiba hivyo within 180 days bila kuapishwa NEC ingeshalitangaza jimbo la Arumeru vacant!.

Sheria ya sick leave ni miezi 3 with full salary na miezi 3 mingine with half salary baada ya hapo ni discreation ya mwajiri.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Captain, kuapishwa ni Dodoma na sio jimboni Arumeru. Wakati wa kuapishwa tulikaa naye hoteli moja pale Dodoma Hotel na alikuwa na mkewe!. Need I say more?.

Rejea katiba ya JMT, mbunge ambaye hauaapishwa, sio mbunge kikatiba hivyo within 1807 days bila kuapishwa NEC ingeshalitangaza jimbo la Arumeru vacant!.

Sheria ya sick leave ni miezi 3 with full salary na miezi 3 mingine with half salary baada ya hapo ni discreation ya mwajiri.

Hapo kwenye red mwajiri wake ni nani?
 
Vichwa vya habari vingine bwana!!!!
Yaani kila nlivyosogea neno by neno nilishaanza kufikiri kua litamalizia na zile issue zinazokaribishaga salaam za "R.I.P",
Anyway, iko siku tu!!!
 
Back
Top Bottom