Mh Mbowe ndani ya USA!!

jk asije akafikiri yeye tu ndo ana awezo wakuruka abroad tena kwa kodi za walala hoi
 
Mbowe Pse angalia sana Msosi wako na Kinywaji usije ukatoka Ngozi Nnee. Bado tunakuhitaji
 
Wanahangaika end of the day Magamba wanaruka hewani bila shida! siasa ni mchezo mchafu I ever had!
 
Wameenda kwa minajili gani?
Maana ni Mbowe na Nyalandu.. Au ilikuwa coincidence tu walikutana airport...??!
 
Hapo Mh.Mbowe anafanya nini na huyo gamba?kamanda wetu kuwa makini usije lishwa vya kulishwa yakawa yale yale ya kupelekana Apollo India,ni angalizo tu kamanda wetu.
 
jasusi hata ukumbi pm jamani wekeni wazi ama mnaogopa asilishwe potassium cynide na kile chama chetu cha mauwaji??teeehhh teeehhhh
Pdiddy,
Usiwe na wasi. Nilimtumia MTM pm ya anwani kulikofanyiwa mkutano na makamanda wetu.
 
IMG_0671.JPG
Mbowe kava kishamba au kikomunisti, hajui kuchagua nguo za kumechisha? angalia mwenzake alivyotulia, yeye kama kaokoteza tu, inasikitisha kwani yeye ilikuwa apige alegance yenyewe.
 
Jasusi, we don't see any updates up to now..... Kunani@ D. C?
Bukanga,
Samahani jana kikao kimemalizika usiku sana na sikuweza kuingia kwenye mtandao. Tulitegemea angalau vijana kumi hivi lakini by word of mouth taarifa zilitapakaa na kulitokea vijana zaidi ya thelathini. Kwa wengi wao ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana na kamanda Wenje. Wenje ndiye aliyeanza kuzungumza na kutoa historia fupi juu ya maisha yake na uamuzi wa kugombea ubunge Nyamagana. Alisema haikuwa kazi rahisi kushindana na mtu kama Masha ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani na polisi wote wakiwa chini yake. Aliwaambia vijana kwamba bila ku take risk huwezi kufanikiwa maishani. Kamanda Mbowe alizungumzia zaidi mchakato wa katiba. Alielezea sababu za wabunge wa Chadema kusisia kikao hasa pale ilipoonekana kwamba Makinda amekiuka taratibu za kibunge kuwabana. Alipendekeza kuwa ni bora Spika wa bunge awe mtu neutral. Makinda yuko kamati kuu ya CCM na huyo huyo anategemewa kuwa partial kwenye bunge la multi party. Haiwezekani. Alisema Chadema iliamua kukutana na rais kumpa taarifa ya madhara yatakayotokea iwapo wataendelea kulifanya zoezi la katiba mpya kuwa zoezi la kutafuta katiba itakayoridhisha CCM peke yake. Alisema baada ya maelezo ya kikao cha siku nzima, Kikwete alikubaliana na hoja za Chadema lakini akawaambia hawezi kukataa mswada wa CCM kwa sababu "atakuwa mgeni wa nani?" Kwa mujibu wa Mbowe, hivi sasa hoja za Chadema zimekubaliwa na Kikwete na matokeo yake ndiyo haya tunayoona kwenye vyombo vya habari kuwa wabunge wa CCM wanamsusia Kikwete. Amesema hata kwenye tume itakayoendesha mchakato wa katiba rais ataiteua lakini kutokana na majina yaliyopendekezwa na pamoja na Chadema, asasi za kiraia, viongozi wa kidini, na vyama vinginevyo. Kamanda Mbowe alizungumzia mambo mengi tu lakini hasa hasa aliwaambia vijana walioko hapa kwamba wanaweza kuwa "resource" kubwa kwa Chadema. Aliwataka wawe tayari ku take risks kujiandaa kugombea nafasi za ubunge katika uchaguzi wa 2015, akisema kuwa wakijitokeza mapema, Chadema itawasaidia kuwafunda na kuwatayarisha. Vijana wa eneo hili la DC, Virginia na Maryland, wamekubali kuunda ushirikiano na kamanda Wenje aliwapa contacts zake akisema atakaporudi next time akute huu ushirikiano umeimarishwa na kuahidi kuwa mwaka 2016 atakuja Marekani kama waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa chini ya serikali ya Chadema. Kuna vijana walipiga picha nadhani watakuja baadaye kuzitundika humu. Pia alikuwepo mwandishi anayetumikia Ebony FM ya Iringa, alirekodi mazungumzo yote pamoja na maswali na majibu na ameniambia atatayarisha ripoti kadhaa zitakazotangazwa na redio hiyo. Kwa hiyo walioko kwenye maeneo hayo mnaweza kuyanasa matangazo hayo na labda baadaye kuyaweka hapa JF. Kwa kifupi ni hayo tu wana JF. Samahani sikuweza kuyatundika haya jana usiku kwa sababu nilizoelezea hapo awali.
 
Vijijini Chadema inafahamika sana ila inahitaji kutangazwa zaidi.
Mmaroroi,
Usemayo ni kweli. Jana kwenye tafrija mama mmoja aliuliza swali juu ya juhudi hizo baada ya kumwambia Mbowe kuwa alikuwepo kwenye uchaguzi wa 2010 kijijini kwake. Na ingawa alichelewa kujiandikisha na kupiga kura alijaribu kuwashawishi ndugu zake, mama yake majirani kupigia Chadema kura na wote walimjibu kuwa wanapigia CCM. Hiyo bado ni changamoto kubwa kwa uongozi wa Chadema
 
Jasusi,

Kwanza natanguliza personal appreciation kwa mawasiliano, pili nimefurahi sana suala la utaifa lilikua mbele ya kila kitu, tatu yasiishie hapo i can bet kwamba 80% ya professionals hawana tena imani na mfumo uliopo sasa
 
Safi sana kamanda mbowe.nashangaa sana kuskia watu walioko usa,wanaojua demokrasia ni nini wanakumbatia ccm. Kuna dr mmoja apo usa wakati kikwete yuko apo alimpongeza eti anainua uchumi wa nchi.hiv huyu anajua dadake,kaka,mama na ndugu wanaishi maisha gani?watz wa usa amkeni,kama baba na mamako walikuwa ccm miaka hiyo,kwa sasa wamekipa mgongo chama hicho
 
Back
Top Bottom