Mh Mbowe (MB)afanya mkutano mkubwa jimboni Hai

Wakati wa kupokea kadi za CHADEMA,wameomba radhi kwa vitendo vyao vya fujo na vurugu walivyokuwa wanafanya wakati wa kampeni mwaka jana
 
Hongera kamanda Mbowe na wananchi waliohudhuria mkutano huo,kikubwa ni kuelekeza nguvu kwenye kufungua matawi na kuongeza wanachama.
Alunta continua!
 
hapo sijaigusa Chadema, umeelewa wewe?
Hii kichwa haihitaji kuchochea ndiyo ielewe kama baadhi ya member fulani humu ndani. siyo dhambi kuigusa CDM kwenye ukweli lakini bado naamini huwezi kumdhamini Mhindi kwenye box labda biashara.
 
Hii kichwa haihitaji kuchochea ndiyo ielewe kama baadhi ya member fulani humu ndani. siyo dhambi kuigusa CDM kwenye ukweli lakini bado naamini huwezi kumdhamini Mhindi kwenye box labda biashara.

We endelea na siasa zako za ndiyo mzee.
 
Na Kamanda Lema Jana Na Leo Ni Mashina Tu Kwa Kwenda Mbele, Mapambano Mbele Kwa Mbele...

Wao waache waendelee kuwavunjia nyumba wale walowabeba na fuso kwenda kwa kampeni
 
Hivi hapo kuna uchochezi gani niliufanya?
Siyo lazima iwe kwenye thread hii, hiyo nimeichukulia kama general statement tu, anyway back to the topic alichokifanya Mbowe ni kama walichokifanya akina Milya Arusha kuja kufungua matawi na kuhamasisha chama tu.
 
Wabunge wa Magamba mko wapi mbona hamfanyi mikutano? Nape pekee yake ataweza?. Posho mkinge nyie mikutano afanye Nape, tokeni Dar nendeni majimboni mkisubiri mpaka ugeni wa Nape au JK majimboni mwenu hamuwezi kukwepa kuzomewa.
 
Leo Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA,kamanda Freeman Mbowe,amefanya mkutano wa hadhara jimboni Hai,mkutano mkubwa pamoja na kufungua shina la wakereketwa.Wakati wa ufunguzi wa shina hilo wanachama wa ccm akiwepo Ndugu wa Mwenyekiti wa ccm wilaya ndugu Olomi,amejiunga na CHADEMA,mbali na Olomi aliambatana na wanachama 30 wa ccm.
Pamoja na kujiunga na CHADEMA pia wameomba radhi,kwa fujo walizofanya wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana..
Mapambano yanaendelea

Asante kwa taarifa ila hapo penye red; hayo maneno yanatia kichefuchefu. Sioni sababu ya copying and pasting, CHADEMA wangeweza kutafuta jina lao badala ya kuiga na kwa ubunifu nadhani wanaongoza. Kama ambavyo CCM enzi za Makamba walivyowahi kutamka hadharani kwamba neno UFISADI halipo kwenye msamiati/Kamusi ya chama chao ; ikiwezekana, neno "wakereketwa" lifutwe kabisa kwenye misamiati ya CHADEMA. Nadhani maneno UMMA au PEOPLE yanajitosheleza bila kuhitaji misamiati ya kimagamba.
 
Utumwa wa fikra ni utuma mbaya sana. Hata kitu cha kawaida kinaonekana cha ajabu. Yaani Mbowe kufanya mkutano jimboni kwake ni news? Au huna cha kufanya? Tunakoelekea huko basi hata akienda haja ndogo tutaambiwa. Ajabu ya ndugu wa kiongozi wa CCM kuingia CDM ni nini?

Wewe Mbopo wahi madaktari maana ugonjwa wa utumwa wa fikra uliokuanza unaelekeza kukoma hadi kuona, kusema, kunusa, kutenda hata kuogopa watu kama Mbowe na CDM. Wazungu wanaita frustration kwa sababu ya mafanikio ya wengine. CHUKUA HATUA
 
Leo Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA,kamanda Freeman Mbowe,amefanya mkutano wa hadhara jimboni Hai,mkutano mkubwa pamoja na kufungua shina la wakereketwa.Wakati wa ufunguzi wa shina hilo wanachama wa ccm akiwepo Ndugu wa Mwenyekiti wa ccm wilaya ndugu Olomi,amejiunga na CHADEMA,mbali na Olomi aliambatana na wanachama 30 wa ccm.
Pamoja na kujiunga na CHADEMA pia wameomba radhi,kwa fujo walizofanya wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana..
Mapambano yanaendelea

Nanyaro Ephata,
Hapo kwenye red umekosea Mkuu. CDM huwa tunatumia msamiata 'WAFURUKUTWA' badala ya 'WAKEREKETWA'. WAKEREKETWA ni msamiati unaotumiwa na chama cha Magamba tangu enzi za TANU.
 
Utumwa wa fikra ni utuma mbaya sana. Hata kitu cha kawaida kinaonekana cha ajabu. Yaani Mbowe kufanya mkutano jimboni kwake ni news? Au huna cha kufanya? Tunakoelekea huko basi hata akienda haja ndogo tutaambiwa. Ajabu ya ndugu wa kiongozi wa CCM kuingia CDM ni nini?

kwani we magamba mbopo kama unaona hii habar haina umuhim kwako si usiisome wala ku comment
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom