Mh. Mbassa (CHADEMA) ashinda kesi jimbo la Biharamulo Magharibi

Mdau inabidi ufunguke zaidi. Siyo wote tunamjua huyo Oscar. Ni wapi huko?

Naomba nitumie fursa hii kueleza kwa kifupi Oscar ni nani, Dr. Mbassa, na kesi waliyokuwa wakikabiliana nayo!
Oscar William Mukasa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 alikuwa ni Mbunge wa Biharamulo magharibi kupitia CCM (Biharamulo ni moja kati ya wilaya 6 za mkoa wa Kagera, na wilaya pekee inayowakilishwa na Mbunge wa Upinzani). Oscar alikaa katika Ubunge wake kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja na nusu. Kabla yake jimbo hilo lilikuwa likishikiliwa na mbunge machachari na mkongwe katika siasa kupitia TLP akijulikana kama Phares Kashemeza Kabuye, alifariki kwa ajali ya gari akiwa anaenda Dar kuhudhuria mkutano mkuu wa chama chake, na ndipo ukaitishwa uchaguzi mdogo uliomweka Oscar madarakani. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, ilibidi Oscar asimame kutetea kiti chake na mpinzani wake na wa pekee alikuwa ni Dr. Anthon Gervase Mbassa kupitia CHADEMA. Matokeo yalimweka Dr. Mbassa kuwa Mbunge. Lakini Oscar (bila shaka na chama chake cha CCM), hawakuridhika na matokeo, na hivyo kuyapinga kupitia mahakamani. Kesi hiyo imeanza kusikilizwa kwa takribani mwezi mmoja na jana ndio ilikuwa hukumu.

MWENENDO WA UKUMU ILIVYOKUWA.

Hukumu ilitarajiwa kuanza kusomwa saa 3.00 asubuhi lakini watu wakiwa mahakamani likatolewa tangazo kuwa hukumu itasomwa saa 7 adhuhuri, ulipofika muda huo ikatangazwa tena kuwa ni mpaka saa 9 alasiri. Hali hii ilianza kujenga shaka kwa wanachi waliokuwa pale wakiisubiria na hasa ikizingatiwa kuwa kesi hii ilikuwa imevuta hisia za watu mbalimbali!

Hatimaye ilipofika saa 10.41 Jaji aliingia mahakamani na saa 10.45 alianza kusoma moja kwa moja. Upande wa mlalamikaji, kulikuwa na hoja 9, ambazo zote zilitupwa kutokana na kile alichokiita kuwa na "USHAHIDI UNAOJITOSHELEZA NA USIO NA SHAKA" kusoma huko kuliendelea ambapo kulikamilika saa 2.52 usiku. Ambapo Jaji alimtaja kuwa mahakama inamuona kuwa Dr. Anthony Gervase Mbassa kuwa mbunge halali na kwamba kesi ile inatupiliwa mbali kwa gharama! wanasheria wanaweza kusaidia kutoa tafsiri ya maneno hayo. Mimi mwenyewe nilikuwepo mahakamani na niliushudia mwenendo mzima.

Mh. Dr. Anthony G. Mbassa, licha ya kuwa mbunge wa Biharamulo magharibi kupitia CHADEMA, pia ni waziri kivuli wa Afya.
 
Excellent. Umefunguka vizuri sana Edwin. Kumbe sijakosea kuoa Biharamulo, mashemeji bright kama wewe ndo nawataka. Gud day shem
 
Kilichonisikitisha ni kuchelewa kupata taarifa, yaani hukumu zote mbili : Sumbawanga na Biharamulo zingetoka by alasiri ingenoga sana.
 
Back
Top Bottom