Mh Masilingi vs Prince Bagenda

mutua12

Member
Aug 20, 2008
39
2
Wakuu hivi kwa nini wanasiasa wa Tanzania wanapenda sana kupakana matope?

Badala ya kuweka kipaumbele cha kuleta maendeleo kwa wananchi wake wao kazi kusemana tu.

Ndio maana hutuendelei, sasa hivi wanafikiria uchaguzi wa 2010 hakuna cha ahadi walizotoa 2005. Kusema kweli huyu mtu anitwa Bagenda anatumiwa sana, hafai .

Lakini inaonekana pia Mh kachukia sana ndio maana hata mavazi(combat) yake aliyovaa kama ni ya CHADEMA vile.

Yetu mimacho.
 
Bagenda hafai hakika -- ni kuwadi wa kutupa, ni kama vile Muhingo Rweyemamu wa magazeti ya habari Corporation ya Rostam, ingawa huyu anafanya ukuwadi wake kiakili zaidi. lakini wote ni supporters wakubwa wa mafisadi.

Hilo gazeti analolihariri ni la Karamagi, fisadi aliyethibitika, sasa Bagenda ataandika nini?
Ila inashangaza kuwa sasa hivi kaanza kumpigia debe Tibaigana ambaye ameonyesha dhamira kuligombea jimbo hilo. Tibaigana alikuwa afisa wa polisi wa cheo cha juu na RPC wa Dsm na kwa dhamira yake hiyo, ni dhahiri alikuwa anaudanganya umma kwamba yeye hana chama wakati huku akituma vikosi kuwapa kipondo waandamanaji wa vyama vya upinzani. Kumbe ni kada wa CCM! Aliingia lini CCM -- mwaka huu?

Tibaigana atapata shida sana kulitwaa jimbo hilo hasa akimpata mpinzani machachari mwenye data za madhambi yake alipokuwa bosi wa mapolisi hapa Dar. TUSUBIRI!
 
Hapo umenena , Tiba naye akijaribu ataanguka kama ilivyo kuwa jimbo la Mbeya Vijijini
na akiendelea kuwa pamoja na huyu kuwadi atakuwa amejimaliza mwenyewe.
 
kama hoja ni kufaa au kutofaa Masilingi mweupe hafai kabisa sio kwa maneno ya Bagenda huo ndio wasifu wake, Aliweza kutumia vyema wadhifa wake wa kuongoza taasii nyeti ya usalama wa taifa kujijengea ufalme jimboni kwake kwa kuwatisha wanaompinga ndani ya chama chake na kuwa tetemesha wananchi wapenzi wa vyama vya upinzani kilio mnachokiskia sasa ana hofu nampinzani wake ndani ya chama chake ana hofu na hukumu ya wananchi dhidi yake kwa kuwa hawezi kutumia historia ya wadhifa wake kwa kuwa mpizani wake nae kidume. DAMU YA KABENDERA IMEANZA KUMRUDI
 
siasa ni mchezo mchfau,tunayasubiri mazito zaidi!! na yatakuja tu maana uchaguzi ndo huyafichua.
 
Hata mimi nilishikwa kwikwi kumwona masingili aki-enjoy airtime ya ITV. Si mnakumbuka ugomvi wa Mengi na Masilingi?!

Kweli siasa haina adui wa kudumu na biashara haigombi.

Naumia kuona hawa waandishi mamluki pamoja na mkurugenzi wa ikulu wote ni wahaya. Hivi hili kabila limepatwa na shetani gani? Natamani nibadili kabila! Wanyakyusa naomba mnisajili...

Ilo gazeti la Karamagi si kwamba linajaribu kupandikiza dhana potofu tu bali limevuruga umoja usio rasmi wa wabunge wa kagera. Sasa wanakwenda bungeni kama ngedele wasio na agenda. Tofauti sana na wabunge wa kusini na wale wa kaskazini.
 
___________________________

OMUTWALE: Naam, umenena. katika post yangu sikuwa na maana kuwa Masilingi naye anafaa, la hasha. Naye ni fisadi tu, kwani alisha utetea ufisadi katika sakata hilo la yeye na Maengi wakati wa kuuzwa kwa Kilimanjaro Hotel.

Alitishia kumshughulikia Mengi, kama vile Masha alivyotishia hivi karibuni. Hivi watu hawa hawawezi kufanya ufisadi wao bila ya kutisha wengine?
 
Bagenda hafai hakika -- ni kuwadi wa kutupa, ni kama vile Muhingo Rweyemamu wa magazeti ya habari Corporation ya Rostam, ingawa huyu anafanya ukuwadi wake kiakili zaidi. lakini wote ni supporters wakubwa wa mafisadi.

Hilo gazeti analolihariri ni la Karamagi, fisadi aliyethibitika, sasa Bagenda ataandika nini?
Ila inashangaza kuwa sasa hivi kaanza kumpigia debe Tibaigana ambaye ameonyesha dhamira kuligombea jimbo hilo. Tibaigana alikuwa afisa wa polisi wa cheo cha juu na RPC wa Dsm na kwa dhamira yake hiyo, ni dhahiri alikuwa anaudanganya umma kwamba yeye hana chama wakati huku akituma vikosi kuwapa kipondo waandamanaji wa vyama vya upinzani. Kumbe ni kada wa CCM! Aliingia lini CCM -- mwaka huu?

Tibaigana atapata shida sana kulitwaa jimbo hilo hasa akimpata mpinzani machachari mwenye data za madhambi yake alipokuwa bosi wa mapolisi hapa Dar. TUSUBIRI!

Ama kweli, hapa naomba kuuliza, nasikia huyu Tibaigana ana resort pale Mkuranga na nasikia (mimi hupita njia kwa nje sijaiingia kuiona ilivyo ndani) ilivyo ni ya kiwango cha zaidi ya mishahara yake yote ya upolisi uchanganye na marupurupu yake na viinuwa mgongo vyake vyote havitotosha thamani ya hiyo resort, nasikia ina ukubwa wa kijiji kizima, Jee ni kweli haya jamani? kama kweli, hiyo mifedha yote aliitowa wapi? au alikuwa akifanya uZombe na ufisadi alipokuwa polisi?
 
Mkuu DSM,

Ni kweli anayo na kwa kawaida kitega uchumi kama hicho hakiwezi kujengwa kwa mshahara + Marupurupu + Kiinua Mgongo, la hasa, kwa vyovyote vile amekopa pesa kutoka kwenye taasisi za fedha (e.g. Banki nk)

Ni sehemu nzuri kupumzika weekend!
 
Ama kweli, hapa naomba kuuliza, nasikia huyu Tibaigana ana resort pale Mkuranga na nasikia (mimi hupita njia kwa nje sijaiingia kuiona ilivyo ndani) ilivyo ni ya kiwango cha zaidi ya mishahara yake yote ya upolisi uchanganye na marupurupu yake na viinuwa mgongo vyake vyote havitotosha thamani ya hiyo resort, nasikia ina ukubwa wa kijiji kizima, Jee ni kweli haya jamani? kama kweli, hiyo mifedha yote aliitowa wapi? au alikuwa akifanya uZombe na ufisadi alipokuwa polisi?
Enzi za Tibaigana na Mahita ndio majambazi walitamba,ni mtu wa fisadi EL kwa hiyo mtoto wa fisadi ni fisadi tu.Bagenda huyu anatumiwa na mafisadi akina Karamagi na EL,Bagenda asipochunga uandishi wake atakumbwa na kesi nyingi za kashfa.
 
Tiba ana haki yakugombea...kaama kunaa mtu anajua kibaya au mabayayake ayaweke hadharani mara tu akitia mguu wake kwenye siasa...lile jimbo siola masilingi.
 
Ama kweli, hapa naomba kuuliza, nasikia huyu Tibaigana ana resort pale Mkuranga na nasikia (mimi hupita njia kwa nje sijaiingia kuiona ilivyo ndani) ilivyo ni ya kiwango cha zaidi ya mishahara yake yote ya upolisi uchanganye na marupurupu yake na viinuwa mgongo vyake vyote havitotosha thamani ya hiyo resort, nasikia ina ukubwa wa kijiji kizima, Jee ni kweli haya jamani? kama kweli, hiyo mifedha yote aliitowa wapi? au alikuwa akifanya uZombe na ufisadi alipokuwa polisi?

Kwa kifupi ni kwamba, Tibagana ni Tajiri wa Kupindukia, ingawa hamfikii Mahita. Ma RAPC wanacheza RAFU nyingi sana ndugu yangu, achana nao kabisa, sio binadamu hao.
 
Ni dhahiri Masilingi ni mfa maji asiyeacha kutapatapa, tena nilimdhania ana busara lakini kwa maneno yake kwenye vyombo vya habari nimegundua hata lugha ya Kiswahili inampa shida sana kuongea.Namshanga hata Mkapa kumpa nafasi nyeti kama ile aliyoishika kwa awamu iliyopita.
Sina hakika na mparaganyiko wa wabunge wote wa Kagera ,Lakini mlitegemea nini kwa wajuaji wale?Kila mmoja anajua kuliko mwenzake,Hilo la Tiba kuingia katika ulingo wa siasa mie sitii neno ,Kwani mapolisi wa wakati ule najua walikuwa wanashirikiana na majambazi na kugawana na wakubwa zao.
Bagenda namheshimu kama Mtaaluma aliyebobea tena mwandishi wa vitabu mahiiri hapa nchini,Alipotea step tu alipoingia kwenye siasa.Sasa anavuna alichopandwa.
 
Tibaigana angekuwa mjanja angetulia kimya na CAPITAL yake aliyojikusanyia jeshini (POLICE) maana akiendela kujianika katika siasa ataumia na kuwaumiza wenzake wengi. Jamaa ana madudu mengi mno na wapo wengi wanamsubiria kuanika uozo wake hadharani. Hakuna mahala pazuri kufanya hilo kama katika ulingo wa siasa....

omarilyas
 
Masilingi naye anatabia fulani ya dharau na maneno ya kashfa.Sishangai kuviona vita vinavyoendelea. Nakumbuka vizuri kubinafsha kilimanjaro hotel
 
mkuu kausha, ni KABENDERA SHINANI!!?? hebu mwaga data zaidi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom