Mh Magufuli na msururu wa wanahabari, hii haikubaliki

Mimi nakerwa na watu wanaochunguza chunguza raisi ajaye katika CCM. Kwani ni lazima rais atoke CCM? Hizi sio zama za za chama kimoja na nyie waandishi wa habari mkome kupetipetiwa na waroho wa madaraka.
 
usidanganye watu magufuli yuko juu ndo maana hata wewe umeona muhimu kuandika habari zake.
Wanahabari wanatafuta habari zitakazouza gazeti, kuna habari zingingine hata ukiwapa posho watakula na hawataandika maana hazina mshiko, nina ushahidi wa hilo. Magufuli anauzika, ukiweka habari yake lazima gazeti liende.

Najua chuki tu juzi kaisema cdm ndo imekuwa taabu. Jamani ushabiki unatuletea upofu wa kufikili vizuri!
Acheni kukurupuka bora tu umepost na wewe.
hili ndio tatizo la wengi wetu sisi watanzania,tuantumia muda mwingi sana kutafuta makosa na madhaifu ya watu,kiongozi anapokua anafanya kazi kwa juhudi kutatua matatizo yetu hakuna anaemuunga mkono katika juhudi hizo nguvu zote zinaelekezwa kutafuta madhaifu na kuona anafaidi sana.lakini ukweli uongozi sio kitu rahisi na cha raha sana kama wengi wetu tunavyozani.nazani maendeleo hayaji kwa kukosoa tuu muda wote hata vitu bora vinavyoonekana wazi.
 
mbali na suala la uraisi,je ni sawa kutumia pesa za serikali kulipa posho wanahabari ili wamng'arishe? Tusipumbazike na mbwembwe za mtu,je ni sawa kukaripia walio chini yake mbele ya vyombo vya habari?mimi nakichukulia kitendo hiki kama ukosefu wa mawasiliano ya kutosha na uwajibikaji endelevu kwa baadhi ya watendaji
 
mi namkubali sana pombe!
Ana roho ngumu sana huyu!
Kama alithubutu kuwajibika kuuza nyumba za serikali basi anaweza kuuza mkeo huyu akiwa rais

Mkuu inabidi ujifunze jinsi serikali inavyofanya kazi. Dr. J.P. Magufuri asingeweza kuuza zile nyumba peke yake bila ridhaa ya baraza la Mawaziri! Huo ujinga wa sekata ya umeme ni maamzi ya baraza la mawaziri, yeye anatumwa tu kutekeleza!

Jamani, magufuri hakuamka tu na kwenda kuuza zile nyumba bila baraka ya Mkapa. Political scientists please help....
 
mbali na suala la uraisi,je ni sawa kutumia pesa za serikali kulipa posho wanahabari ili wamng'arishe? Tusipumbazike na mbwembwe za mtu,je ni sawa kukaripia walio chini yake mbele ya vyombo vya habari?mimi nakichukulia kitendo hiki kama ukosefu wa mawasiliano ya kutosha na uwajibikaji endelevu kwa baadhi ya watendaji

Is there any evidence? If yes, from which source (personal or from the ministry/) na ACG anakubaliana na hili?
 
Salamu wana jf,nimekuwa nikifuatilia hali ya mambo na mbio za uraisi wa 2015,nimeamua nianze na huyu mheshimiwa ambaye kwa wasiofahamu wanaaminishwa na vyombo vya habari kuwa ni kiongozi bora kuliko wengine na angefaa kuwa raisi,mimi binafsi naukubali utendaji wake lakini naona walakini mkubwa katika uropokaji na kitendo chake cha kutumia msururu wa wanahabari tena wanaolipwa posho kwa kutumia kodi zetu,inaniuma sana kuona kodi zetu zinageuzwa za kupumbaza na kulaghai fikra zetu,Mungu ibariki tanzania
wanalipwa shing' ngapi?
 
hivi mskaji wangu lengo lako ungependa lowassa asiwe hata na mpinzani nini mzee??maana unahaha kila post kusaka anaonekana kuutaka urais mbali na lowassa anakua target yako...ndio maana nikasema wewe kama sio mh.lowassa basi lowassa anakulipa pesa ya kutosha sana

Anaweza ukwaa wa kurugenzi ya lkulu
 
hili ndio tatizo la wengi wetu sisi watanzania,tuantumia muda mwingi sana kutafuta makosa na madhaifu ya watu,kiongozi anapokua anafanya kazi kwa juhudi kutatua matatizo yetu hakuna anaemuunga mkono katika juhudi hizo nguvu zote zinaelekezwa kutafuta madhaifu na kuona anafaidi sana.lakini ukweli uongozi sio kitu rahisi na cha raha sana kama wengi wetu tunavyozani.nazani maendeleo hayaji kwa kukosoa tuu muda wote hata vitu bora vinavyoonekana wazi.

Most of the people are not ready to show you the right way to succeed, what they will do is to wait and see what you choose and then begin to criticize you. This is typical of Tanzanians: negative minded all the time.
 
Back
Top Bottom