Mh! Kwa hii sidhani kama ni sahihi

Mwl.ngonyani

New Member
Jun 26, 2011
4
0
Juzi asubuhi nikiwa nyumbani mke wangu alikuja nyumbani huku ameshika gazeti moja la kampuni maarufu kwa kuchapa magazeti ya udaku. Nilimwomba nilitazame(ingawa mimi sio msomaji wa magazeti ya aina hiyo).nilishangaa nilipokuta ukurasa mmoja watu wanatafuta wachumba huku wakiweka gazetini namba za simu za mikononi. Nilimuuliza mke wangu kuhusu hilo je ni sahihi? Hapo ulizuka mjadala wa muda kidogo kabla ya kuafikiana kuwa "hayo ni mambo ya utandawazi na ujana tu". Lakini jana alfajili niliamua kufanya utafiti niliandika kupitia mtandao huu kama natafuta mke ili nijionee huku nikiacha email adress niliyocreate jana hiyo hiyo. Huwezi amini nimekuta message 124. Duh!! Labla nikiri mapema kuwa sikumaliza kuzisoma, kabla ya mke wangu kunieleza kuwa tuwaulize wadau wanasemaje? Je mdau wa JF unaionaje hii!
 
Mh Mwl Ngonyani......jana tu ulikuwa watafuta mchumba, leo ushampata na kuoa na kuanza kufumaniana?
https://www.jamiiforums.com/mahusia...taka-ndoa-serious-nahitaji-mke-tafadhali.html

Pole.

lol, 'kumkoma Nyani Giladi mchana kweupeeee!'

funny-pictures-mortal-kombat-monkey.jpg


...big up Mwj1
 
Sijafumaniwa mwee! Mnatamani sana nigongwe red card? Nilichokuwa nakifanya jana ni reseach, na message nilizokuta ni za mabinti ambao walikuwa sample ya utafiti bila wao wenyewe kujua.
 
Mwalimu jina lako linaonekana kama wewe ni mngoni....Kuna thread ilipita hapa ya wangoni.. nasikia wangoni ukiwapa hela itafika lakini mwanamke hafiki....

Sasa mwalimu nafanya reseach..kama jina lako linaendana na mnyama, na kama wewe ni mngoni..sasa kama wewe ni mngoni unaweza fanya reseach ya mapenzi na wanamke?? ..yaani ni sawa na kumpa simba abebe ndama wa n'gombe..
 
whatever happened to informed consent in research participation and confidentiality? hujawatendea haki walioonesha interest na umekiuka maadili ya utafiti!
Sijafumaniwa mwee! Mnatamani sana nigongwe red card? Nilichokuwa nakifanya jana ni reseach, na message nilizokuta ni za mabinti ambao walikuwa sample ya utafiti bila wao wenyewe kujua.
 
Hujafanya fair kbc...nimekuona wa ajabu kwa kweli..mtu una mke badala utulie huko mkishauriana mambo yenu na mkeo unaanza kuleta upuuzi humu. Kuna watu wako serious wanapotafuta humu unawaharibia.
 
Watu hukutana kwa njia
Mbali mbali..
binafsi naona hili ni jambo
la kawaida kabisa..
 
mwalimu na mkeo inaonekana hamna kazi za kufanya maana mnajishuhulisha na yasiyowashukhulisha!
 
umefanya vibaya mwl kuna watu wanatafuta wachumba kweli na wapo serious sasa weye waleta mchezo
 
Back
Top Bottom