Mh Kikwete, uchapakazi wa Lowassa ulificha udhaifu wako

naninibaraka

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
910
668
Ni jambo lililowazi kabisa kwamba serikali hii ya awamu ya nne sasa imepoteza mwelekeo kuliko serikali zilizopita,uchapa kazi wa Mh Lowassa alivyokuwa pm ndo uliofanya watu wengi kutoona udhaifu binafsi wa rais wetu.

Mahali popote utendaji wa viongozi unategemea zaidi utendaji wa viongozi waandamizi, ni ukweli usiofichika kuwa baada ya Lowassa kuondoka serikali imeyumba sana. Utendaji huu wa Lowassa wa kusimama na kutoa decision kwa wakati na pia kupata feedback kwa watendaji ndo ulimfanya rais arelax zaid.

Lowassa ameondoka Kikwete amebaki kama yatima hajui anzie wap na amalizie wap,changamoto ni nyingi,mh kikwete kummefanya mara nyingi kuwa mwoga wa kutoa kauli stahiki kwenye maswala mbalimbali yanayogusha maisha ya watz

Nawasalisha
 
Labda ungesema ubovu wa Lowasa ndiyo uliyofanya serikali ya JK ionekane hivyo refer kashfa za richmond/dowans nk pia unaweza kuona matatizo ya kampeni chafu za kutumia pesa nyingi walizoiba.

yeye alikuwa anachapa kazi pale palipokuwa na masilahi/dili fulani na alikuwa anapambana na wabaya wake kwa kuwafukuza bila kujali haki yao ya kikatiba ya kujieleza

kuna kashfa nyingi mf. mwingine alipokuwa ardhi kuliuzwa open space nyingi dar kwa mkono wake na zinasababisha matatizo mpaka kesho. ni vigumu kumsafisha huyo jamaa
 
Ukweli ndio huo tumebaki na pazia tu pale magogoni.

Nyinyi hamuwezi kuona anachofanya JK...

Kwanza hamtaki kuona hata kama inaonekana..

Pili mko bize mnaangalia maandaman, lema etc..

Kuona ni kuchagua..kwakuwa mmechagua ku-tune kwenye habari za kizushi hamtaona manafanikio ya JK

Sisi wengi tunafuatilia, tunaona miradi na barabara, inakwenda vizuri..
 
Baba Riz anachojua ni kupiga picha na waigizaji muvi na wanamuziki afu na kuchezea mabembea afu na kuchekacheka tu hata mambo yasiyo na msingi! Eti wakawaambia watu kuwa ni chaguo la 'mungu'!! Nadhani inabidi warudi kumalizia ni mungu yupi waliyemaanisha!!
 
Tanzania, Tanzania, Tanzania, nakupenda nchi yangu Tanzania. Siamini mahali ambapo mijadala ililenga kupambana na mafisadi, leo tumekua watetezi wakuu wa ufisadi. Haijalishi ni jambo gani mwizi amesaidia, mwizi ni mwizi tu.

Katika mtaa, baadhi ya wezi na wauza dawa za kulevya ndio wanafanya kazi ya kusaidia jamii, kujenga misikiti na makanisa na kadhalika, haijalishi wanatumia fedha chafu.

Tusikubali tukawa kama Taifa moja ambalo matajiri wa dawa za kulevya ndio wanaendesha nchi na wakiguswa nchi inayumba. Tunakumbuka Pinda aliwahi kusema wakiguswa nchi itayumba, sasa naona na yeye atueleze wazi sasa tutangaze kwamba wizi ni ufisadi ni halali vinginevyo mafisadi wa Kagoda, Richmond, Meremeta, Rada, ndege ya serikali, Kiwira, na majizi mengine wafikishwe mahakamani wakaponee huko vinginevyo Lema atoke na Watanzania wote waliofungwa kwa vikesi vya wizi wa simu, mashati na kuku.
 
Nyinyi hamuwezi kuona anachofanya JK...

Kwanza hamtaki kuona hata kama inaonekana..

Pili mko bize mnaangalia maandaman, lema etc..

Kuona ni kuchagua..kwakuwa mmechagua ku-tune kwenye habari za kizushi hamtaona manafanikio ya JK

Sisi wengi tunafuatilia, tunaona miradi na barabara, inakwenda vizuri..
Topical,
Hujapata habari ujenzi wa barabara umesitishwa? Serikali haina fedha.
 
Mr Kikwete naomba ushughulikie swala la kushuka kwa shilingi naona upo kimya hapa, leo nimekwenda dukani nakuta bidhaa zinauzwa kwa US dola......
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100 bila lowasa ccm by byeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee karibu chademaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaamagogoni
 
Yes, kuna ombwe la uongozi maana hakuna hatua zinazochukuliwa ndio maana munapata nafasi ya kuanza kumuona Lowassa shujaa. JK angechukua hatua dhidi ya Lowassa, kusingekua tena na hizi porojo. Kama kweli kuna udhaifu, hivi kweli Lowassa pekee ndiye suluhisho? Jamani, Watanzania wako makini sana. Kwa sasa sijaona bado mwanasiasa makini ndani ya CCM, japo wapo wenye afadhali ila si Lowassa, hasa kwenye uso wa uadilifu.
 
Topical,
Hujapata habari ujenzi wa barabara umesitishwa? Serikali haina fedha.
Mishahara yenyewe hakuna. Shilingi ya Gavana Balalo (RIP) na ya Gavana Ndulu kama mbingu na ardhi na pia haipo, nchi imekua fukara ghafla na wakilogwa wachape noti tumekwisha.
 
.......Lowassa, yule waziri mkuu aliyejiuzulu, aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, mimi wala sio muumini wake, lakini ni muumini wa uchapakazi wake, mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni, sipendi kuwa mnafiki , unafiki kama ule wa Samweli Sitta John (SSJ aka CCJ) na ule wa Mwakyembe, sitaki, kwani mi ni kijana nikiruhusu unafiki wa jinsi ile, sikawii kuwa mchawi.. Lowassa, yule aliyehamasisha ujenzi wa shule za kata, zilkaengwa, akajiuzulu, na zenyewe zikajiuzulu, yamebaki kama magofu, hamna waalimu na wanafunzi wake pia; Wakuu wa Wilaya wanaelewa utendaji na au uchapakazi wake, JK, analijua hili, wengi wetu tuliojaliwa ile tabia ya kitizedi ya kudandia hoja kwa kutofikiri kwa kina, tumenasa kwenye mtego wa kumchukia Lowassa, ukiuliza utaambiwa Richmond,. Richmond ilimkuta Lowassa na utajiri wake,....kama serikali ya Nyerere ilivyomkuta Sir George Kahama enzi zile na mali zake.. Maswali ya kujiuliza ni nini alichofanya Lowassa cha kumtofautisha na JK AMA NA VIONGOZI WENZAKE NDANI YA ccm. Ni lipi? Ni ufisadi gani unaomfanya tumtoe gamba tumwache JK, MKAPA? ni upi? Kama Lowassa ni Gamba ndani ya CCM hamna anayebaki kuwa sio Gamba....msituaminishe upupu. Watanzania tutalaumu sana umaskini wetu, lakini unafiki una nafasi yake katika kutufanya tufikie mahala hapa; kama hoja ya kutenganisha kofia mbili yaani urais na uenyekiti wa chama ndio unamfanya Lowassa awe Gamba, ni udogo wa mawazo, na ni umaskini kuliko umaskini mwingine wowote, Jamani tuyatoe mawazo yetu jela, tuyavue mavazi, yale mavazi ya njano, ya ufungwa, vinginevyo hatuna wa kumlaumu badala ya kujilaumu sisi,,,,,aah hovyooooo!
 
Nyinyi hamuwezi kuona anachofanya JK...

Kwanza hamtaki kuona hata kama inaonekana..

Pili mko bize mnaangalia maandaman, lema etc..

Kuona ni kuchagua..kwakuwa mmechagua ku-tune kwenye habari za kizushi hamtaona manafanikio ya JK

Sisi wengi tunafuatilia, tunaona miradi na barabara, inakwenda vizuri..
Usitake kunichekesha,
Tuone nini alichofanya, shilingi inayoporomoka, uchumi unavyoelekea shimoni, au unataka tuone ma VX wanayoendesha viongozi,
au unataka tuone idadi ya safari zake 400 yaani karibu sawa na miaka miwili rais hayuko nchini kati ya sita aliyokaa, unataka tuone mafanikio
mengine zaidi ya haya? tuoneshe wewe.
 
Sina shaka na uchapakazi wa EL.Alikuwa jembe si utani!Tatizo ni madudu mengine yanayosemwa kumhusu pamoja na kampani yake.Hata hivyo watanzania tuko milioni 40 na ushee,hivyo 2015 si lazima awe EL tu!,,,tunayo nafasi ya kupata raisi bora miongoni mwa mamilioni ya Watanzania.
 
Ni vigumu kumuamini mwana siasa yeyote
Unajua, kwenye siasa unaweza kuwa msafi au mchafu sana tu, lakini kwa vyote pia vinaweza kugeuzwa na kuwa kinyume kabisa na ukaonekana tofauti kabisa, na zana muhimu katika hili ni vyombo vya habari! Kile kiburi cha EL wakati anajiuzulu si bure kuna mengi ambayo hatuyajui. Kwa Jamvi hili tunaweza kuona taarifa ambazo vyombo vya habari vimepotosha kabisa kwa mawili, kwanza vikitaka kuuza habari, pili kwa maslahi yao binafsi ambavyovyote vinashabihiana. Vyombo vya habari sivishambulii kwa makusudi, lakini hata nchi za magharibi zinavitumia vizuri sana kueneza kitu ambacho vijana sikuhizi hamkifahamu sana kinaitwa "propaganda". Sumu inakuwa chakula na chakula kinakuwa sumu.

Sasa basi, mara nyingi kwakuwa vyombo vya habari ndio dirisha pekee la kuchungulia yanayoendelea kwa viongozi na utawala wao, basi kinachosemwa na kuandikwa huonekana ndivyo kilivyo.

Katika utawala wowote ule, lazima kuwe na active agent, awe ni yule mkuu au msaidizi wake, hawezi kuwa wa chini sana maana itageuka kuwa conflicting, ukizingatia inahusisha maamuzi. Mh Nyerere aliwika sana kwa kuwa alikuwa maarufu na mwenye uwezo ukilinganisha na wasaidizi wake, Marehemu Sokoine alpoibuka hata Nyerere umaarufu wake ulikaribia kupotea kabisa (ambapo hapa kwa mujibu wa kanuni mojawapo ya leadership utawala unakuwa mgumu kwa hawa wawili na inakuwa haifanyi kazi) mafahali hawa waili wasingeweza kukaa zizi moja hata kidogo, wote walikuwa wanapenda kuwa na final decissions, wako ambitious, hard working na visionary most likely wangegongana tu!, Mwinyi aliwabadili mara kadhaa mpaka alipo,mpata ambaye ni loyal na obidient maana nayo ina matter, na hatimaye Ben hakufanya kosa, alimweka mtu ambaye asingeweza kuinfluence mambo bila yeye kuwa na mkono, kitu ambacho kiliimarisha mwonekano wa uwezo wake bila kuwa na mshindani wa ndani, zingatia kuwa pia Ben anapenda kuwa na maamuzi ya mwisho na huwa anapenda yaonekane mara moja (ktu ambacho vijana wengi wanakitamani ingawa hawakipendi kinapowakuta maana huchanganya na independence yao).

Sasa, kwa swala la hawa wawili, wote ni watu wanapenda umaarufu, mmoja ni active na mwengine ni passive, mmoja ni mtaalamu na mwingine ni mwanasiasa tu, na mmoja ni mtu asiyefanya maamuzi kwa haraka na huchukua muda kufanya maamuzi mpaka ashawishike vya kutosha na wakati mwingine huruhusu liwalo na liwe lakini asiwe yeye aliyeamua (Pragmatic) na mwingine ni mtu wa kufanya maamuzi haraka mwenye kuona opportunitioes na kujua linkage ya mambo kwa haraka na mwenye kufanya maamuzi haraka bila kuhpfia risk inayokuja ilimradi awe ameona results na benefits mbeleni. Mf. Yeye kumuondoa mzembe kazini halikuwa jambo linalohitaji siasa kuamua, kuvunja mkataba hata wa nchi haikumsumbua, na ni mtu ambaye akijua hadhi yake iko hatarini yuko tayari kufanya lolote lile ili mradi kurekebisha mambo (nadhani anaweza hata kujinyima)! Hii ndiyo tofauti ambayo wamekuwa wakipambana, sio kwamba walikuwa hawajui tofauti zao, na matokeo ndiyo hayo tuliyoyaona.

Kwa sasa ninachokiona ni hivi, ni vigumu kukubaliana au kukataa hoja hii, hakuna ukweli katika mengi tunayoyasikia, na matokeo yake ndiyo tunachagua viongozi tusiojua undani wao kwa sababu tu ya dirisha hili la vyombo vya habari. Viongozi wengi tuliowachagua wamepata nafasi zao kwasababu ya uwezo wao wa kutumia dirisha hili na kutuonyesha wao ni wachapa kazi kwelikweli. Bahati mbaya sana Mh. Kwa sasa anapata shida mojawapo ya hizi, aidha hana washauri wazuri wa kuweka mambo yake sawa kwenye dirisha hili, au ni mgumu kushaurika kutokana na tabia yake ya kuwa pragmatic ambayo wengi wa wasaidizi wake hawaielewi. Hii imepelekea kwa Mh Raisi kuonekana "Legelege" kitu ambacho nina uhakika wanaokisababisha ni watu wake wa karibu kabisa wa ndani ambao sio waaminifu. Wenye kuvujisha siri na wasioweza kutumia vyombo vya habari katika kuweka mambo sawa ya kiutawala.

Siamini kama Raisi ni mdhaifu kiasi hiki, hapana siamini kabisa, ila naamini walioko karibu nae ni wazembe hakuna mfano, wenye ubinafsi na wasio na maslahi na nchi hii ambao kwakiasi kikubwa ndio wanaoupotosha ukweli na hawamsaidiii raisi ipasavyo kuweka mambo sawa. Haya tutayajua baada ya utawala wa raisi huyu, na iwapo tu atakayekuja atakuwa mkweli. Ninashawishika kusema raisi huyu amekumbwa na mahasimu wengi sana kutokana na maamuzi aliyoyafanya mwanzoni ambayo yaliwathiri hadi watu wake wa karibu ambao walikuwa wachafu, ni muhimu kulikumbuka hili. Kama kuna kinachomsumbua sassa, ni vita ambayo ni kubwa kiasi cha kuona ni vema kupuuzia baadhi ya mambo ili kutokutoa faida kwa maadui ambao, nadhani hakutarajia kuwaona wakiwa wengi hivi, na karibu hivi, maana hata wengine inabidi aishi nao tu atafanyeje.
 
Back
Top Bottom