Mh Kikwete Kuwa Mkweli, Usidhani Tumesahau!

Nijuavyo mimi hakuna issue ya maana iliyoelezwa hapa.

Kashfa zote za EPA, scandal ya Meremeta, Deed Green, Tangold, Mwananchi Gold, IPTL na Kiwira zilitokea kabla ya Kikwete hajawa Rais na hicho kinachoitwa IPTL ni mkataba ambao uliingiwa na Tanesco tena wakati huo ukiwa umeshapitiwa na Baraza la mawaziri. Wanaotaka ajibu maswali hayo wanachotaka kujua kutoka kwake badala ya kwenda kwa Mkapa ni nini? Hawa hawa kwa kushirikiana na Marando ndiyo sasa wanaodai wizi wa fedha za ununuzi wa nyumba ya ubalozi Italia ni wa kutungwa kwa nia ya kumkomoa Mahalu wakati wanajua kwamba huyu Profesa kaiba kweli na ushahidi uko bayana. Ndio sasa wako busy kutayarisha nyaraka za kushinikiza mashtaka yafutwe.

Ukweli ni kwamba baadhi ya watu humu kama aliyepost thread hii ni watu waliovikwa kitambaa cheusi usoni na kukosa ufahamu wa jinsi viongozi wao walivyo na uhusika mkubwa katika yale wanayoyapiga vita.

Hata kama kuna masuala yalitokea kabla ya JK kuwa Rais, issue ni kwamba alipogundua kuna uozo mkubwa namna hiyo alichukua hatua gani kama Rais? Hivi Rais mzima anapowapa wezi kurudisha fedha walizoiba muda wa kuzirudisha na baada ya kuzirudisha mambo yakawa shwari kwa wezi ambao mpaka leo majina yao yako kapuni, unafikiri hiyo ni sahihi? You can fool people for sometimes but not always! By the way, hizo fedha zilizorudishwa na wezi, TSh 74bn/- zilifanyiwa nini? Si afadhali wezi wangeendelea kujinafasi nazo tukajua moja badala ya kutufanya mbumbumbu kiasi hicho? Oh, wake up, please!
 
Hawezi kujibu lolote huyu, ni maneno tu huyu tushamzoea. Amezoea kupiga domo tu!
 
Hawezi kujibu lolote huyu, ni maneno tu huyu tushamzoea. Amezoea kupiga domo tu!

Wamekuja na hadith za magamba ili kufunika hoja zisizo na majibu, lakini tutaendelea kuwapigia kelele ili waendelee kukosa raha!
 
Wafuasi wa Chama cha Magamba, akina Mbopo, et al, kama kawaida yao wameiona njia?
 
Hata kama kuna masuala yalitokea kabla ya JK kuwa Rais, issue ni kwamba alipogundua kuna uozo mkubwa namna hiyo alichukua hatua gani kama Rais? Hivi Rais mzima anapowapa wezi kurudisha fedha walizoiba muda wa kuzirudisha na baada ya kuzirudisha mambo yakawa shwari kwa wezi ambao mpaka leo majina yao yako kapuni, unafikiri hiyo ni sahihi? You can fool people for sometimes but not always! By the way, hizo fedha zilizorudishwa na wezi, TSh 74bn/- zilifanyiwa nini? Si afadhali wezi wangeendelea kujinafasi nazo tukajua moja badala ya kutufanya mbumbumbu kiasi hicho? Oh, wake up, please!

Ungekaa na wanasheria wangekueleza maana ya plea bargaining na iko kila mahali hapa duniani.
 
Wafuasi wa Chama cha Magamba, akina Mbopo, et al, kama kawaida yao wameiona njia?

Hoja hujibiwa kwa hoja. Suala la ufuasi ni la kawaida na wala sijutii maamuzi yangu, lakini nashukuru uongo wenu tunaubaini na kuudhibiti.
 
Ungekaa na wanasheria wangekueleza maana ya plea bargaining na iko kila mahali hapa duniani.

Sidhani kama ndugu Mbopo unataka kusema kwamba wezi wa EPA wali-bargain na Rais wetu JK ili endapo wangerudisha maburugutu ya noti waliyoiba then that's it! Kwa taarifa yako Tanzania haina Sheria inayohusu mambo ya plea bargaining! Kama ipo iweke hapa ili tuijadili! Pia suala la plea bargaining haliishii kwenye negotiation bali linatakiwa lifikishwe mahakamani ili mtuhumiwa akakubali kosa kisha apunguziwe adhabu kwa sababu ya kukiri kosa! Sasa hii plea bargaining ilifanyika namna gani? Acha kupotezea ndugu, haitakusaidia kitu! JK aeleze TSh 74bn/- amezipeleka wapi, that's it!
 
Hoja hujibiwa kwa hoja. Suala la ufuasi ni la kawaida na wala sijutii maamuzi yangu, lakini nashukuru uongo wenu tunaubaini na kuudhibiti.

Mbopo ingelikuwa ni heri kwako ukaionea huruma nafsi yako ikiri ukweli hata kama unauma! Unataka kutuambia kwamba tunapodai kwamba JK aliyafumbia macho kwa makusudi kabisa masuala ya Meremeta, TanGold, Buzwagi, Mwananchi Gold, Kagoda, Kiwira (tena kwa hili alidai tumwache Mzee apumzike), Deep Green Finance, nk ni uwongo ambao eti mmeubaini na kuudhibiti? Dhambi hii aliyoifanya JK na wafuasi wake haisameheki hata kwa dhabihu! Yeye aendelee kula kuku tu Ikulu na kutabasamu kwa sana, historia itamhukumu maana historia ni hakimu mzuri sana!
 
Back
Top Bottom