Mh. Kikwete achana na utumwa wa fikra

Noboka

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
1,246
626
Dr. Kikwete wakati anahutubia mkutano wa wawekezaji huko Kenya nilimsikia anazungumza Kiingereza chetu kile cha kuunga unga, alipopewa nafasi balozi wa Kenya nchini Tanzania yeye akaongea Kiswahili. Binafsi nimekuwa nashangaa inakuwaje viongozi wetu hawataki kukitukuza kiswahili? Nakumbuka wakati mmoja Mkapa kwenye mkutano wa AU alitoa hotuba kwa kiingereza (ingawa Mkapa kiingereza chake ni kile cha kwa Malkia hasa), lakini alipohutubia Joakimu Chisano akaongea kiswahili fasaha mkutano huohuo.

Wazo langu:

Kiingereza ni muhimu lakini Kiswahili nacho kina nafasi yake, hata kama tumeshindwa kuuza vizuri rasilimali kama madini na mbuga za wanyama, bado viongozi wetu wangelitilia umuhimu suala la lugha ya kiswahili bado tungeweza kuuza hiyo huduma kwa wale wanaoihitaji. Siwezi kushangaa kwa wale mlioko huko majuu kuwa walimu wa kiswahili huko ni kutoka Kenya au Ghana. Kama mkuu wa nchi bado fikra zimefungwa na ukoloni je anatuongoza anatupeleka wapi?
 
hakika ! Hakika !

Kuna ushamba wa matumizi ya Kingereza , mara nyingi tunaaminishwa kuwa ni Lugha ya Kisomi ! Ujinga kabisa
 
Alafu wapambe wake wanamsifu kwamba amepigania kiswahili kuwa lugha rasmi ya AU. Anashindwa kukitumia hapo Kenya tu, sijui huko Au atakitumiaje? Ushamba tu kama wa katibu wa Umofia kwenye riwaya ya No longer at ease!
 
Dr. Kikwete wakati anahutubia mkutano wa wawekezaji huko Kenya nilimsikia anazungumza Kiingereza chetu kile cha kuunga unga, alipopewa nafasi balozi wa Kenya nchini Tanzania yeye akaongea Kiswahili. Binafsi nimekuwa nashangaa inakuwaje viongozi wetu hawataki kukitukuza kiswahili? Nakumbuka wakti mmoja Mkapa kwenye mkutano wa AU alitoa hotuba kwa kiingereza (ingawa Mkapa kiingereza chake ni kile cha kwa Malkia hasa), lakini alipohutubia Joakimu Chisano akaongea kiswahili fasaha mkutano huohuo.
Wazo langu:
Kiingereza ni mhimu lakini Kiswahili nacho kina nafasi yake, hata kama tumeshindwa kuuza vizuri raslimali kama madini na mbuga za wanyama, bado viongozi wetu wangelitilia umhimu suala lalugha ya kiswahili bado tungeweza kuuza hiyo huduma kwa wale wanaoihitaji. Siwezi kushangaa kwa wale mlioko huko majuu kuwa walimu wa kiswahili huko ni kutoka Kenya au Ghana. Kama mkuu wa nchi bado fikra zimefungwa na ukoloni je anatuongoza anatupeleka wapi?

Hiyo cha mtoto, kali ya mwaka ilikuwa hapa hapa Dar, nafikiri wakati wa Tsunami ya Japan, Bw. Mkapa (raisi mstaafu) alikwenda kutoa pole Ubalozini, kama kawaida yake akatoa hotuba yenye maneno magumu ya kiingereza ilipofika zamu ya Balozi wa Japani akatoa Hotuba kwa Kiswahili fasaha kabisa! Kwa kifupi kituko kama hiki huwezi kuona sehemu yoyote Dunia hii isipokuwa Kusini mwa Jangwa la Sahara tu! Halafu Dr Watson (DNA nobel laureate) akisema sisi waafrika tuna IQ ndogo Duniani tunaandama na kudai afukuzwe kazi, lakini matukio yanayoendelea Barani kwetu (kusini mwa Sahara) ni ngumu kufikiria vingine!
 
Dr. Kikwete wakati anahutubia mkutano wa wawekezaji huko Kenya nilimsikia anazungumza Kiingereza chetu kile cha kuunga unga, alipopewa nafasi balozi wa Kenya nchini Tanzania yeye akaongea Kiswahili. Binafsi nimekuwa nashangaa inakuwaje viongozi wetu hawataki kukitukuza kiswahili? Nakumbuka wakati mmoja Mkapa kwenye mkutano wa AU alitoa hotuba kwa kiingereza (ingawa Mkapa kiingereza chake ni kile cha kwa Malkia hasa), lakini alipohutubia Joakimu Chisano akaongea kiswahili fasaha mkutano huohuo.

Wazo langu:

Kiingereza ni muhimu lakini Kiswahili nacho kina nafasi yake, hata kama tumeshindwa kuuza vizuri rasilimali kama madini na mbuga za wanyama, bado viongozi wetu wangelitilia umuhimu suala la lugha ya kiswahili bado tungeweza kuuza hiyo huduma kwa wale wanaoihitaji. Siwezi kushangaa kwa wale mlioko huko majuu kuwa walimu wa kiswahili huko ni kutoka Kenya au Ghana. Kama mkuu wa nchi bado fikra zimefungwa na ukoloni je anatuongoza anatupeleka wapi?

Inashangaza tuna waalimu wa kiswahili kutoka mexico, of all the places! kwanini isiwe kutoka Tanzania?
 
unashangaa kiingereza cha kuunga kuunga wakat yeye doctor wa kupewa? wenzake wanasoma yeye anapewa udaktar....majanga
 
Huyo ****** jamani msameheni.....unajua tena pale Msoga yeye ndio king kijogoo so lazima ajitutumue wasije wakadhani ni mla mihogo mwenzao!

JK ni DHAIFU. Kwa hisani ya JJ Mnyika.
 
Huyo ****** jamani msameheni.....unajua tena pale Msoga yeye ndio king kijogoo so lazima ajitutumue wasije wakadhani ni mla mihogo mwenzao!

JK ni DHAIFU. Kwa hisani ya JJ Mnyika.

Sijui kama huu ni uvumi tu lakini numesikia kwamba kanuni za utendaji katika serikali ya Bongo zinasema kwamba ukivaa ile suti ya malkia (yaani 3-piece akimbatana na kitanzi shingoni) unatakiwa upige lugha ya malkia (potlea mbali kuungaunga vipande). Ukivaa suti ya kaunda basi ni ruksa kuchapa kile kipwani. Sasa mlitaka mzee na pamba zake kali avunje kanuni??!!
BTW, kuhusu Kiswahili kama taaluma na kama raslimali ya kuuza na kupata faida, Wakenya wametuzidi hatua kumi. Kwa mfano asilimia kubwa ya waalimu wa Kiswahili ughaibuni ni Wakenya. Sisi Wabongo iko maneno mingi tu, vitendo ni zero. Hatuna ujasiri na elimu yetu (iwe ni katika Kiingereza au Kiswahili) haijengi moyo wa kujiamini. Badala yake ni elimu ya ukariri na matokeo ya ukariri ni kama hayo mnayoyashuhudia kwa mkuu wa kaya na washauri wake!:eek2:
 
Back
Top Bottom