Hilo ni jambo lingine, tumuunge mkono ili amalizie muda wake kwanza.Matamko kama haya aliwahi kuyatamka Mhe. BWM.
Mkuu, kwa hali halisi ya TZ kwa sasa, unaonaje Mhe. JK akaongezewa muda wa kuiongoza nchi yake ya TZ baada ya 2015?
Umekufikisha wapi zaidi ya mafanikio kila nyanja? huoni? husikii? hutazami? basi hata hugeuki nyuma kutazama ulikuwa wapi kabla ya Kikwete na leo uko wapi? au bado ulikuwa tegemezi la wazee? (mtoto wa shule).
Hakika Kikwete kawabana vyanzo vyenu vya wizi vingi sana mpaka mnamchukia. Lakini kwa maendeleo, hakuna zaidi ya wakati huu, na kila dalili zinaonesha kuwa Kikwete atatuachia future nzuri sana, tushindwe wenyewe tu.
Unapaswa kukumbuka sawia siyo kuandika uongo hapa mtu mzima.Jk aliongoza kura NEC na Mark alikuwa wa Tatu,Mzee Salimu wa pili kama ilivyojiri pia katika Mkutano mkuu.Ukizungumzia kikao cha Kamati kuu JK alikuwa afutwe kulingana na uonfgozi kutokubaliana nae na ushauri wa Sekretarieti ya Chama,Lakini ushauri wa Mzee Kingunge na Mzee APSON unaedai kuachakazi baada ya kikwete kuapishwa kitu ambacho siyo.Apson alistaafu Mwanzoni mwa mwaka 2007 miaka miwili baada ya JK kuwa Rais.
Kwanza Inasemekana TISS ndiyo iliyoshinikiza chini ya Apson kuhakikisha Kikwete anashinda kwa sababu anakubalika na kumwacha nchi ingeingia katika machafuko.Na ukumbuke hakuna Mtanzania wakati huo isipokuwa wachache sana kama mimi ambao tulikuwa against na ushabiki wa kitanzania kuhusu uwezo wa Kikwete na wengine wakafikia kusema ni chaguo la Mungu sasa hapo Hata APSON NA MZEE Kingunge wangeshauri tofauti unadhani ni nini kingetokea?
Kabla ya kuandika tufanye tafakuri na kuwa na usahihi wa kile tunachokiwakilisha kwa watu.
Nakumbuka Vizuri mchakato wa kumtafuta Mgombea Ndani ya CCM mwaka 2005 Ulivyo kuwa Na makundi na vuta niku vute nyingi...
Kwa Wanaofahamu Kwenye Top 3 ya 2005 Jina la JK lilikuwa Halipo..walipita Wengine Na ambae alipata Nafasi ya kwanza ni Mwandosya ndie angegombea Uraisi wa nchi mwaka 2005,Baada ya vuta nikuvute Mh kingunge Alisimama na kuwauliza wajumbe wa CCM, hivi Tumsimamishe JK anaekubaliwa Chama kiendelee kuongoza hata kama uongozi wake utakuwa mbovu Au TUMSIMAMISHE mtu mwingine Tushindwe CCM ife? Ndipo wajumbe wakakubaliana kumpitisha JK ambae hata 3 bora hakuwepo.
Awali ya hapo Bwana BWM akiwatumia TISS kukusanya Maoni Nani Anakubalika kati ya waliochukua Form Ripoti ilikuja Kuwa JK ANAKUBALIKA but Apson ambae alikuwa Mkurugenzi kwenye Report hiyo Ali koment kuwa Jamaa anakubalika lakini Hafai katika uongozi na Hataisaidia IDARA YA TISS kufikia Malengo..
Jk Alipo apishwa na kutinga ikuru alikutana na Barua ya kujiudhuru ya Apson...
"lawama lawamani"