Mh. Joseph Selasin: Asante Rais Kikwete

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Hongera Mheshimiwa Joseph Selasin, Mbunge wa Rombo kwa kuwa muwazi kuhusiana na utendaji murua wa Rais JK kwa kuwezesha ujenzi wa barabara jimboni mwake.

Amediriki kutamka mbele ya Rais JK kuwa "Ingekuwa amri yake barabara husika ingeitwa Jakaya Kikwete Road"


Source: Taarifa ya HABARI TBC, Saa 2 Usiku, October 30, 2012
 
Safi kada wa cdm kwa kuwa mkweli na kukubali ukweli mana kina slaa wanapinga kila kitu hata penye ukweli
 
Kwan kakosea nin? Sio kila jambo unapinga 2 wakat wa kutenda 2tende na 2kubliane na utendaji
 
Hiyo haina shida, wala sioni tatizo.
Kwa namna yoyote rais akitembelea eneo lako la kazi lazima uonyeshe kumpa heshima anayostahili japo kisera mnatofautiana

Lakini akishawapa kisogo tu ni M4C without any apology.
 
Safi kada wa cdm kwa kuwa mkweli na kukubali ukweli mana kina slaa wanapinga kila kitu hata penye ukweli
Ndio kazi ya upinzani, barabara kujengwa ni jukumu la serikali, ikijenga kwa nini isifiwe. Isipojenga lazima ikumbushwe, huyu Selasini nae sijui kimemkuta nini leo.
 
Maua mazuri yapendeza, chakula tayari kale kisha ukalale eee. Usisahau kushusha neti mwanangu mbu wengi eee.
 
Kuna pongezi zingine ni kejeli,TBC wawe makini.Nilisikia siku moja mikoa ya kusini akisomewa risala na kumsifu kwa kuwaondolea umasikini.Basi kwa siku mbili TBC hiyo ilipewa nafasi ya kwanza.
 
Isiwe Selasini anajiandalia mazingira ya kurejea kwao CCM. Maana kilichotokea kwa Nyimbo kinaanza kutupa shaka kama wengi waliojazana CDM si nyemelezi waliotumwa kukimaliza chama kwa kukikimbia wakati wa uchaguzi. Kuna haja ya CDM kuwa makini na watu wake.
 
Amediriki kutamka mbele ya Rais JK kuwa "Ingekuwa amri yake barabara husika ingeitwa Jakaya Kikwete Road"


Source: Taarifa ya HABARI TBC, Saa 2 Usiku, October 30, 2012......[/QUOTE]

napita tuu
 
aliyewezesha ni yeye au ni waziri wa ujenzi?....

anayepaswa kupewa hongera ni walipa kodi wa tanzania kwa kuwa pesa zao zilitumika kujenga barabara na siyo mwanasiasa bali ni wananchi. kujengwa barabara hakutegemei kuwepo au kutokuwepo kwa jk kwani hiyo ni mipango ya muda mrefu.
 
Napinga utamaduni huu potofu.JK alitoa hizo fedha mfukoni mwake?

-Hiyo ni kodi ya watanzania pamoja na wananchi wa Rombo na wanastahili huduma bora.Barabara ya Rombo siyo hisani ilikuwa ni huduma muhimu na ya lazima

-Sipingi yeye kumpongeza Rais lakini tusiwe chanzo cha raia kuamini kwamba huduma kama barabara ni hisani.Huku ni kufifisha elimu ya uraia na harakati za wananchi kujua haki zao

-Wananchi wa Rombo wanastahili kujua mbele ya Rais kwamba barabara ile ni matokeo ya kodi zao hivyo wafanye kazi kwa bidii na Rais atakiwe kuomba msamaha kwa serikali kuchelewesha barabara muhimu kama hiyo

Ni haki yetu wananchi wa Rombo kuwa na barabara na ni wajibu wa derikali kujenga barabara as long as wanakusanya kodi.Tena Rais ameonyesha dharau kwa kutoonyesha hata courtesy ya kuomba msamaha kwa kutucheleweshea barabara kama vile sisi ni raia wa Kenya.
 
Kwakuwa mheshimiwa Rais wetu anapenda kupewa sifa za kijinga........nampongeza Selasini kwa kutambua hilo. Rais wetu anapenda sifa za kijinga jamani dah! Hata hashtuki?

Ni jukumu la mkuu wa nchi kutekeleza majukumu yake kwa kuwatumikia wananchi waliomchagua.
 
Jk hajashtuka sifa alizopewa..........hahaaaa siasa bana.........
 
Back
Top Bottom