Mh. Jakaya Kikwete: Heshima ya Suruali ni Mfuko!

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Mh. Jakaya Kikwete,

Natanguliza samahani kama matumizi ya misemo ya taarab yatakukwaza. Sio kwamba mimi ni mmoja wa wale wanaoamini kwamba unapenda mipasho au wasaidizi wako kama Salva wanavyosemekana kutoa majibu ya kimipasho kwenye masuala nyeti yanayotugusa kila siku.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete, kumekuwa na migomo mara kwa mara, maandamano kila siku, kwa nini? Je hili ni swali unalojiuliza?

Katika hali ya kawaida ningetegemea mawaziri wako na wasaidizi wako wajiulize. Sidhani kama wanajiuliza na kama wanajiuliza sidhani kama wana majibu sahihi!

Sitashangaa wakitoa majibu kama 'ni CDM wanachochea, ni Dr Slaa anawashawishi, ni chuki za udini hizo'. Sitashangaa kamwe!

Lakini nitashangaa kiasi kama hutawashangaa kwa majibu hayo. Sitashangaa sana. Inawezekana unalitegemea hilo!

Mimi pamoja na WanaJF wenye nia njema tunajitolea kueleza sababu ni nini! Endapo utasoma hii thread chukua yale ambayo utaona ni sahihi ili uyafanyie kazi. Si dhumuni la hii thread kukurushia lawama moja kwa moja lengo ni kukueleza ukweli ambao mawaziri na wasaidizi wako hawathubutu kukueleza. Aidha wanakuogopa au hawakutakii mema! Vile vile inawezekana hawana uwezo wa kutambua na kutatua matatizo.

Hapa JF utaambiwa ukweli. Sio kwa lengo la kukudhalilisha bali kwa lengo la kuikoa nchi yetu na balaa ambalo linaweza kutokea....wewe ni shuhuda wa kilichotokea Kenya, kinachotokea Ivory Coast, kinachoendelea Misri na kilichojiri Tunisia!! Unajua vizuri sana!

Tunakoelekea hakutakuwa na muda wa kuambiana ukweli wala kupeana ushauri. Kila mmoja atakuwa anaokoa roho yake! Kila mmoja atakuwa anapigania mkate wake! Itakuwa tumechelewa sana!

Nisizunguke sana, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, kama nilivyosema 'heshima ya suruali ni mfuko'. Watanzania mifuko yetu imetoboka! Haina kitu! Wanafunzi hawawezi kupata mahitaji yao ya kila siku, walimu, manesi, madaktari na wengineo! Wakandarasi wanaidai serikali yako Bil 700+ hawajalipwa! Dowans wanaidai tanesco Bil 94 ambazo serikali yako kupitia waziri wa fedha imesema hazina haina! Wakulima hawana fedha za kununua pembejeo na msimu wa kilimo umeanza! Wazazi hawana fedha za kuwalipia watoto wao ada na mahitaji mengine!

Kitaalamu watu wa uchumi watakushauri kuhusu mfumuko wa bei nk. Hayo mimi sina uelewa nayo! Ila na wewe ni mchumi labda utalielezea au unalielewa vizuri zaidi! Kwa mtanzania wa kawaida tatizo lililopo ni kupotea kwa heshima ya mfuko! Vijana hawana ajira! Ukame umeathiri kilimo, mishahara haitoshi kukidhi mahitaji nk! Mfuko hauna heshima yake Mheshimiwa Jakaya Kikwete!

Unatakiwa ufanye nini?

1. Kwanza jitambue. Wewe ndie kiongozi wa juu na unayo mamlaka yote kuongoza. Nafasi hiyo hukupewa na mtu yeyote zaidi ya wananchi waliokuchagua. Sio Rostam, Edward, Ngeleja wala Makamba! Ni wananchi!

2. Pili amua. Fanya maamuzi magumu. Achana na biashara za sheria ichukue mkondo wake na hadithi za 'sitaki kuingilia uhuru wa mahakama'. Kumwambia Jaji Mkuu ambaye ni mteule wako kesi zote za ubadhirifu na rushwa zisikilizwe haraka na kwa umakini mkubwa umeingiliaje uhuru wa mahakama? Mbona kesi ya yule aliyetaka kumuuza Albino Mwanza iliisha ndani ya wiki si zaidi ya tatu, akafungwa na haki itatendeka? Kinachotokea sasa hivi ni watu wanaiba fedha za serikali wanaamini wakishikwa watapewa dhamana kesi itakaa muda mrefu watahonga wataachiwa!! Watanzania huwa wanasahau! Ndio imani iliyopo!
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, ni kweli hujui kwamba kuna watu wako tayari kukaa jela miaka 7 ilii mradi fedha walizoiba zipo salama? Mfano, nikiiba Bilioni 5 nikafungwa miaka miwili kuna tatizo gani? Mshahara wa meneja wa benki ka mwezi ni milion mbili kwa mwaka ni milioni 24! Kwa miaka miwili ni Milioni 48! Kipi bora mtu aibe bil 1.3 afungwe miaka 3 abaki na Bil 1.3 au akae uraiani miaka 3 apate mil 72!!
Siamini kwamba Mheshimiwa Jakaya Kikwete haujui kwamba wafanyakazi wa serikali na hata mawaziri wako ni wezi! Wanaandaa risiti za uongo, wanaongeza bei za vitu, wanatumia vyombo vya serikali vibaya nk! Mambo haya ndio yanasababisha matumizi ya serikali kuongezeka na wananchi kupata hasira zaidi! Fanya maamuzi na washughulikie wahusika!
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, ulikuwa na list ya wanaokwepa ushuru ukasema unampa Kamisha Mkuu wa TRA!! Kwa nini usiifanyie kazi wewe mwenyewe?

3. Tatu mfukuze Makamba. Hana msaada kwako! Sina la zaidi.

4. Nne ongoza nchi na wananchi wako. Serikali yako imejitenga sana na wananchi walioiweka madarakani. Hata nyumbani kwako usipomwambia mke na watoto wako unapata mshahara kaisi gani, unadaiwa sh ngapi na matumizi ni yapi usilalamike wala kushangaa mkeo akita ummnunulie Audi zawadi ya birthday na mtoto akitaka ML 500 ampe girlfriend wake zawadi karudi kutoka UK! Hawajui shida na mahangaiko yako! Mbaya zaidi wakiona wewe unatapanya! Unakunywa bia kila siku! Unasafiri kila siku hawajui unaenda wapi na kufanya nini! Wanaona jirani analima shamba lao anavuna anasafirisha mazao wao wapo tu! Wanasubiri ahadi yako utawapa Audi na ML 500 kama zawadi! Watachoka kusubiri watadai kwa nguvu utahama nyumba!

Jaribu kuwashirikisha, ni nchi yao! Mbona ni watu waelewa sana wananchi wako?

5. Washauri wako hawana manufaa kwako! Inawezekana wachache ni wazuri lakini kuna mambo mengi yanayoenda sivyo yanasababisha tuamini kwamba timu yako ya ushauri ina walakini! Mfano, wanashindwaje kuona tatizo kabla halijatokea? Mbona wanaweza kuona vurugu za CHADEMA kabla hazijatokea hata kama kwa kuona huko watu wanakufa?

Mheshimiwa Jakaya Kikwete, wanaJF watasema zaidi! Watakusaidia ili kuokoa nchi yao! Wasikilize! Kuwa mvumilivu kwani utakayoyasikia ndio mawazo yao! Wana haki ya kusema na watasema!

Heshima ya suruali mfuko Mheshimiwa Jakaya Kikwete!!
 
Hakika hili ni bandiko maridhawa,tena lililobeba ujumbe muhimu kwa mustakabari wa uhai wa taifa letu.asante mkuu!
 
Hakika hili ni bandiko maridhawa,tena lililobeba ujumbe muhimu kwa mustakabari wa uhai wa taifa letu.asante mkuu!

Mawazo na michango isiyo ya kishabiki itasaidia kufikia lengo. Tusubiri tusikie WanaJF wanayapi ya kumueleza JK
 
Tatizo kubwa la Mh Rais ni kutochukua maamuzi stahili kwa wakati stahili, kuendelea kuwa na watu kama Rostam, Lowassa, Chenge, n.k. kwenye nafasi nyeti za Chama kama vile Kamati kuu na NEC ni kuwadharau watanzania wanaoamini watu hawa wamehusika na ubadhilifu unaowasababishia ugumu wa maisha.
Umekuwa ukijitetea kuwa huwezi kumhukumu mtu bila mahakama kusema ni mharifu lakini Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa Mke wa Mfalme hastahili na hatakiwi kusingiziwa katembea nje ya ndoa yake. Kusingiziwa peke yake kunatosha kumkosesha umalikia na hivyo mazuri yote ya ufalme.

Waondoe kwenye Kamati Kuu, NEC, n.k. wale wote wanaotuhumiwa, wapo wengi ambao hawana mawaa na wanaweza kuzishika nafasi zao, kama utawaamini na kuwapa fursa.

Pili Makundi hayajengi, wewe kama kiongozi mkuu hutakiwi uonekane unaunga mkono kikundi fulani kwenye jamii, kufanya hivyo ni kuwasaliti walikuchagua ambao hawako kwenye kundi unalounga mkono. Mwanzo kulikuwa na kundi la wanamtandao na ambao hawakuwa kwenye mtandao, sasa linakuja kundi jingine ambalo ni hatari zaidi la Udini! Kwa sasa kuna kundi ambalo umeliacha liote mizizi la waislamu ambao wanaunga mkono serikali yako, hata pale ambapo kila mtanzannia anaona serikali imekosea (mfano mauaji ya Arusha, Mbarali, malipo ya Dowans, n.k.) hili ukiliacha bila kulishughulikia litaiingiza nchi hii katika mgogoro mkubwa, sidhani kama kati ya vitu ambavyo unataka watanzania wakukumbuke kama rais wa nchi hii ni kuwa wewe ndiye muasisi wa mgogoro wa kidini Tanzania.

Naomba nitoshee hapa, na wana JF wengine nao watatao ya kwao
 
Mawazo na michango isiyo ya kishabiki itasaidia kufikia lengo. Tusubiri tusikie WanaJF wanayapi ya kumueleza JK

Kidonda cha mwenzio unaona wekundu..Msando, ni lini ukahisi maumivu ya yule ombaomba ambaye hajala,while umepigilia masambusa yako na karedbull? Hivi unataka kusema kikwete na jopo lake hawajui yote hayo? Mimi naamini kuwa sote tulokulia shamba hatuwezi sahau adha na taab za huko..japo ulimbukeni na ubinafsi vinatusahaulisha..Shida za msingi zinazoipekenyua nchi yetu..anyway,mwenda bure si mkaa bure huenda akaokota..
 
Hivi ndo tuseme Mheshimiwa huwa hasomi haya!? na hakuna mtu wa pelekea!? kama ni hivyo anapata wapi habari za matatizo ya wananchi!! AU ANALALA TUU!
 
Kamanda, saluti. Ni kitu ambacho huwa najiuliza mara nyingi! Tumekulia shamba, nimechunga mbuzi, nimeenda shule na kuni na kopo la maji, nimeshika namba asubuhi, nimekula ugali na maziwa ya mgando kama mlo kamili, nimekunywa chai na kiporo cha wali nk!! Kuna wengine wamelala njaa, hawakuwa na chochote mpaka walipofanikiwa kufika mjini na kukamata nafasi za uongozi! Wanaijua njaa, wanajua tabu! Tunajua shida ni nini! Lakini tunakuwa wa kwanza kuwasahau wenye shida! Ubinafsi unachukua nafasi! Kwa historia ya Mh. Jakaya Kikwete alizaliwa kwenye nyumba ya nyasi! Kulikoni asijue shida za fukara/fakiri/maskini wa nchi hii? Na yeye si aliwahi kuwa hivyo? Tafadhali nisaidie katika hili!
 
Mtoa Mada nakupongeza kwa namna ulivyoaandika yaani lugha yako ina staha hata kama mtu hatakubalina na ulichoandika lakini uwasilishaji wako wa ujumbe unamfanya hata huyu unayemuandikia ausome. Sio wengine wanatumia lugha za kejeli, matusi, kebehi hata mhusika anaona ujinga kusoma, maana kama unaandika kwa ujinga si hata content itakuwa ujinga.

Angalia sasa wachangiaji walivyooanza lugha zao za Bandarini..............................
 
Hivi ndo tuseme Mheshimiwa huwa hasomi haya!? na hakuna mtu wa pelekea!? kama ni hivyo anapata wapi habari za matatizo ya wananchi!! AU ANALALA TUU!

Henge, sio tu hasomi, ina maana haoni? Hasikii? Unaweza kusema yuko busy na JF ni sehemu ndogo sana ya yeye na wasaidizi wake kupoteza muda lakini hawaoni maisha ya watanzania? Wananchi wana shida! Wananchi wanateseka!

Huwezi amini tarehe 3.2.2011 nilihudhuria kikao cha wazazi shule ya msingi niliyosoma! Kila mtoto anatakiwa achangie sh. 8,300 ya chakula, mlinzi na mpishi! Ilibidi ipigwe kura lini siku ya mwisho kulipa na kuna mzazi aliomba mwisho iwe tarehe 15.03.2011!! Hili nimeshuhudia! Mwisho wengi wakasema iwe tarehe 28.02.2011!! Unaweza ukaona hali waliyonayo wazazi wetu vijijini!

Napata mawazo kama yako!
 
Nina imani kama JF italeta mabandiko kama haya hata Rais atakuwa member wa JF na kuchukua yale mazuri tunayomshauri hapa jamvini. Umefika wakati wanaJF tubadilike tuache lugha za kihuni na kumwita JK majina yasiyokuwa na maana. Hongera mkuu japo nimepitia juu juu nitarudi baadae nisome kwa yakini ikibidi kama kipo cha kuongezea na mimi niongezee nitilie mkazo. Rais wetu ni msikivu naamini atatusikiliza.
 
Tatizo kubwa la Mh Rais ni kutochukua maamuzi stahili kwa wakati stahili, kuendelea kuwa na watu kama Rostam, Lowassa, Chenge, n.k. kwenye nafasi nyeti za Chama kama vile Kamati kuu na NEC ni kuwadharau watanzania wanaoamini watu hawa wamehusika na ubadhilifu unaowasababishia ugumu wa maisha.
Umekuwa ukijitetea kuwa huwezi kumhukumu mtu bila mahakama kusema ni mharifu lakini Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa Mke wa Mfalme hastahili na hatakiwi kusingiziwa katembea nje ya ndoa yake. Kusingiziwa peke yake kunatosha kumkosesha umalikia na hivyo mazuri yote ya ufalme.

Waondoe kwenye Kamati Kuu, NEC, n.k. wale wote wanaotuhumiwa, wapo wengi ambao hawana mawaa na wanaweza kuzishika nafasi zao, kama utawaamini na kuwapa fursa.

Pili Makundi hayajengi, wewe kama kiongozi mkuu hutakiwi uonekane unaunga mkono kikundi fulani kwenye jamii, kufanya hivyo ni kuwasaliti walikuchagua ambao hawako kwenye kundi unalounga mkono. Mwanzo kulikuwa na kundi la wanamtandao na ambao hawakuwa kwenye mtandao, sasa linakuja kundi jingine ambalo ni hatari zaidi la Udini! Kwa sasa kuna kundi ambalo umeliacha liote mizizi la waislamu ambao wanaunga mkono serikali yako, hata pale ambapo kila mtanzannia anaona serikali imekosea (mfano mauaji ya Arusha, Mbarali, malipo ya Dowans, n.k.) hili ukiliacha bila kulishughulikia litaiingiza nchi hii katika mgogoro mkubwa, sidhani kama kati ya vitu ambavyo unataka watanzania wakukumbuke kama rais wa nchi hii ni kuwa wewe ndiye muasisi wa mgogoro wa kidini Tanzania.

Naomba nitoshee hapa, na wana JF wengine nao watatao ya kwao

Ntemi, kwa mwendo huu tutafikia lengo! Hongera sana kwa mchango wako!
 
Nimefurahishwa sana na thread hii lakini nataka nikuhakikishie kuwa siyo JK kuwa haya hayajui, wapo UWT ambao kazi yao ni kutafuta maoni ya wananchi na kwenda kumjuza mkuu hali jinsi ilivyo lakini amekuwa mwoga wa maamuzi na hufikia wakati hutupa/kupuuza maoni hayo. Hapo ndipo jamaa wa UWT nao hushangaa inakuwaje mkuu anashikwa na kigugumizi katika mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wake?
Alishaambiwa toka awali Makamba si mtu mwema kwa chama lakini mpaka leo bado anamg'ang'ania kama ruba! Labda anajua siri zake nyingi za waganga wa kienyeji alimpeleka kisha akaona mafanikio sasa mzimu wa waganga wa Makamba unamuandama, na kama si hayo basi anajua siri nyingi kama ilivyo kwa Kagoda ambayo haishikiki! Pamoja na haya lakini hakuna njia muafaka wa kudeal na mtu kama huyu ambaye anataka kukiua chama kutokana na mdoma wake.
Dowans watu wanamwambia hilo ni janga ambalo linaweza kuondoka na chama lakini ang'ang'ania walipwe ili hali kila kitu kesha juzwa. Unajua urais ni njia ambayo maamuzi yake yanategemea sana washauri ambao huwa hawakurupuki lakini mwenye uwezo na mamlaka ya mwisho wa kutamka ni rais.
Yapo mengi lakini mkuu apunguze uoga katika maamuzi, aelewe hawezi kamwe kuwaridhisha wote katika nchi aangalie nguvu ya umma ipo wapi ndiyo afuate.
 
Mzee wa Rula, zaidi ya hao UWT wapo Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya! Hawa kazi yao ni kumwakilisha Raisi katika maeneo yao!

Matatizo yote ya wananchi yanajulikana! Yako wazi sana! Ingawaje imefikia mahali matatizo hayo yanaonekana ni kawaida na wananchi wamekubaliana na hali halisi!

Lazima tufike mahali tuseme hapana. Tufike mahali tutoe mapendekezo nini kifanyike!

JF ina uwezo huo! Ukiangalia uwezo wa watu kulaumu na kushutumu utaona kabisa inawezekana kushauri na kupendekeza!
 
ndefu sana kusoma lakini umeiandika kwa ustadi mkubwa sana....
 
haya ndio mabandiko ya maana......... yaaani nimeisoma na kuipednda sana hii kitu tatizo anayeambiwa sasa ujuha mwingii....kichwa juu juu tu
 
ndefu sana kusoma lakini umeiandika kwa ustadi mkubwa sana....

ukitaka kumficha mtu mweusi kitu basi weka kwenye maandishi..... na ndio maana munaangamia kwa kukosa maarifa
 
Ni hoja nzuri mtoa hoja...I hope those clever chaps would advise the president basing on the facts that you have well narrated in your thread.
JK ndio nahodha wa hii meli yetu inayopitia mawimbi mazito. Ni muda muafaka sasa aonyeshe kwa vitendo yeye ndiye kinara wa meli kwa kufanya mambo tofauti. Heshima haiji kwa kuogopwa..anapewa mtu kwa kustahili. Mtoa mada umesema ukweli kwamba hali ikiwa hivi ilivyo...migomo kila sehemu, watu kukata tamaa ya maisha, maisha magumu na gharama za maisha zenye kupanda kwa kasi...tutafika mahala tunaweza kumegeka! Watu wema wa Tanzani hatutaki kuyaona hayo maana hayatatusaidia lolote ila kutuongea balaa tu.
 
Mheshimiwa Jakaya, nchi yetu ina wataalam wengi sana mpaka wengine tunaexport kwenda nchi za nje!! Tafadhali watumie wataalam hawa katika teuzi zako; vigezo vya kuteuliwa katika nafasi mbali mabali viwe uadilifu na uwezo na si uanamtandao au uswahiba; ukifanya hivyo nchi yetu itaendelea na matatizo kwa wananchi yatapungua.
 
At last mwanasheria Msando umefanikiwa kuirudisha jf kuwa uwanja wa great thinker , lakini tatizo lililopo ni katiba yetu hakuna mahali inamlazimisha mtumishi mkuu wa nchi "rais" tuliyemuajiri kuwa kurazetu na kumlipa kwa kodi zetu awawajibike kwetu pindi tukimhoji au tukimuuliza ndiyo maana tunapojadili masuala ya msingi ambayo tunamtaka atupatie majibu anakuwa na jeuri ya kusema hizo ni kelele za mlango hazimkoseshi usingizi
LAKINI katiba ikimbada kuwa rais atawajibika kujibu kero za wananchi basi hali itakuwa tofauti hata watu kugombea nafasi hiyo watakuwa wakijiuliza mara mbilimbili niende au niwaachie wenye nia ya kweli ya kuongoza ?
Kwa sasa rais kukusikiliza ni feva amekupa na kukujibu ni akijisikia ila kwa haya namuombea kwa mungu ajisikie kuyajibu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom