Mh. Jaji Gabriel Rwakibarila Mruhusu Mh Godbless Lema afanye kazi ya wananchi.

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
Mh. Jaji Gabriel Rwakibarila Mruhusu Mh Godbless Lema afanye kazi ya wananchi.
LEMA AOMBA KESI ITUPWE
Peter Saramba, Arusha
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, jana aliiomba mahakama kutupilia
mbali tuhuma dhidi yake kwa sababu ni za uwongo, chuki na fitna.

Amedai kuwa hali hiyo ndiyo iliyowafanya Waziri mkuu aliyejiuzulu,
Edward Lowasa na aliyekuwa mgombea kupitia CCM, Dk Batilda Burian,
hawakufika mahakamani kutoa ushahidi licha ya kutajwa mara kadhaa.
Akiongozwa na wakili wake, Method Kimomogoro katika kutoa ushahidi,
Lema alidai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na wapiga kura watatu,
imetokana na chuki za mlalamikaji wa kwanza, Mussa Mkanga baada
ya kukosa udiwani katika Kata ya Sombetini.
Alimwomba Jaji Gabriel Rwakibarila kuwaamuru wadai kumlipa ghrama
zote alizoingia na muda wake aliopoteza tangu alipoanza kuhudhuria
shauri hilo lililoanza kuunguruma Julai mwaka jana, ili iwe fundisho kwa
watu wengine.

Alimweleza jaji kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa ameshindwa
kutekeleza majukumu yake ya kibunge, kwa sababu ameazimika
kuhudhuria mahakamani kushughulikia kesi hiyo.

Alidai kuwa kesi hiyo imetokana na madai ya uwongo uliotungwa na
wadai Mkanga na wenzake Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaowakilishwa
na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida.

Aliieleza mahakama kuwa kama tuhuma dhidi yake zingekuwa za ukweli,
Lowasa na Dk Burian waliotajwa kwa namna ya kuonekana kudhalilishwa
na kushushiwa hadhi yao mbele ya jamii, wangefika mahakamani kutoa
ushahidi ili kuthibitisha tuhuma dhidi yake.
Lema alidai viongozi hao wameacha kwenda mahakamani kutokana na
ukweli kwamba maneno yanayodaiwa kuwa aliyatamka dhidi yao si ya kweli.

Alidai kuwa hiyo pia ndiyo sababu ya Dk Burian kutofungua kesi dhidi
yake baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

Aliieleza mahakama iliyojaa wasikilizaji kuwa hata katika barua yake
ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi, Dk Buriana alishindwa
kuorodhesha au kutoa mifano ya kauli za matusi, kashfa na udhalilishaji
alizodaiwa kuzitoa.
Lema alidai kuwa kitendo hicho ndicho kilichomlazimisha msimamizi
wa uchaguzi katika Jimbo la Arusha Mjini, Raphael Mbunda kumruhusu
kuendelea na kampeni.
Shahidi hiyo alidai hata vielelezo vya nakala ya CD zizodaiwa kurekodiwa
maneno yake ya matusi hayakuwasilishwa mahakamani kuthibitisha tuhuma
dhidi yake.

Alidai kuwa CD hizo zingewasilishwa mahakamani kesi hiyo ingekuwa
imeisha mapema kwa sababu ukweli ungedhihirika.

Katika hatua nyingine, Jaji Rwakibarila aliendelea kuwavunja mbavu kwa
vicheko wananchi wanaohudhuria mahakamani baada ya jana kuanza mtindo
mpya ya kudhibiti wanaosinzia wakati kesi inaendelea kwa kuwaamuru
kusimama kwa dakika kadhaa kabla ya kuwaruhusu kuketi tena
MAONI YANGU:
Serekali inaingilia uhuru wa mahakama=PERIOD
 
wanamchosha kamanda wetu kiakili. Mbona muuaji wa baba wa taifa anadunda kwenye vogue?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom