Mh Habib Mchange unahujumiwa Kibaha mjini?

Status
Not open for further replies.
Ilishathibitika kuwa ile ya Dr.Slaa ilikuwa ni propaganda ya kupunguza kura zake za urais.Mchange ilithibitika kuwa aliwatumia fedha kwa njia ya M-PESA wajumbe(usimsahau mjumbe kutoka mwanza alivyotoa ushuhuda) na akiwagharamia wengine chakula,malazi na nauli kinyume na taratibu za chama!Hizo chuki zenu dhidi ya Heche ni uthibitisho kuwa hamuwezi kuwa viongozi.Uchaguzi wa bavicha ulishapita,badala ya kumuunga mkono mshindi ili mapambano yaendelee nyinyi mnaendekeza makundi yenu kumpiga majungu Heche!Kwa bahati nzuri mapambano yanawezekana bila nyinyi na labda ndo maana mnazidi ku"hate"!.Kikubwa hapa Mchange bado una nafasi ya kukamilisha ndoto zako ila strategies unazotumia sio sahihi.Kuwa makini na busara za washauri wako akiwemo huyu bwana/bibi!Wapo wanasiasa wengi wakubwa waliowahi kupata madoa makubwa(mfano Zuma),lakini kwa kufuata strategies za kueleweka leo wametimiza malengo yao.

Mnyantari.
haijawahi kuthibitika kama mchange alitoa rushwa mahali popote pale ndio maana hata chama chao hakijawahi kuunda chombo chochote kuchunguza ili kupata ushahidi ulio kamili.
kilichotokea pale ni ule mfumo wetu wa siasa chafu za kukimbilia kuitana mafisadi ndio maana KUBENEA KWA KUWA ALIKUWA ANA NDOTO ZA SIKU MOJA KUGOMBEA KIBAHA akaamua kutumia gazeti lake bila kudeclear interest kama ni mpinzani wa mchange akamchafua kijana wa watu.i
kama unaweza kuthibitisha wapi na kina nani waliolipiwa vyakula na mchange walete hapa jukwaani wathibitishe ukiondoa huyo mwenyekiti wako wa mwanza aliyelipiwa tiketi ya ndege na GODBLESS LEMA kuja dar kushudia unafiki ili wamkomeshe mchange wakiamini watakuwa wamemkomesha za zitto!..
ndugu yangu yawezekana haukifahamu unachokisema..hapa hatuzungumzii HECHE wala bavicha sababu miongoni mwa watu wenye uwezo mdogo kabisa duniani ni huyo john heche wako ndio maana ameshindwa hata kujitafutia kipato chake cha kuishi mpaka akaomba chama kimlipie kodi ya nyumba yaani komu na slaa wamemlipia huyo heche wako kodi ya nyumba ya miezi 12 pale mabibo ili aendelee kuwa kibaraka wao.
sema ni wapi imethibitika kuwa slaa amepewa kashfa ya mke wa mtu ili impunguzie kura tu na sio uweli?...
mchange inaonekana anawachoma sana nyie wazee wa matamko...teh teh teh
 
Bado sana kujifananisha na Zitto.Yeye ana staili yake ya kufanya siasa za hoja kwa umakini mkubwa sana.Anasoma sana,anafuatilia sana na cha ziada the guy is very intelligent.Sasa kutaka kumuiga bila kuwa na hivyo vitu ni kufurahisha tu jukwaa la siasa.Very long way to go boys...!
 
Mnyantari.
haijawahi kuthibitika kama mchange alitoa rushwa mahali popote pale ndio maana hata chama chao hakijawahi kuunda chombo chochote kuchunguza ili kupata ushahidi ulio kamili.
kilichotokea pale ni ule mfumo wetu wa siasa chafu za kukimbilia kuitana mafisadi ndio maana KUBENEA KWA KUWA ALIKUWA ANA NDOTO ZA SIKU MOJA KUGOMBEA KIBAHA akaamua kutumia gazeti lake bila kudeclear interest kama ni mpinzani wa mchange akamchafua kijana wa watu.i
kama unaweza kuthibitisha wapi na kina nani waliolipiwa vyakula na mchange walete hapa jukwaani wathibitishe ukiondoa huyo mwenyekiti wako wa mwanza aliyelipiwa tiketi ya ndege na GODBLESS LEMA kuja dar kushudia unafiki ili wamkomeshe mchange wakiamini watakuwa wamemkomesha za zitto!..
ndugu yangu yawezekana haukifahamu unachokisema..hapa hatuzungumzii HECHE wala bavicha sababu miongoni mwa watu wenye uwezo mdogo kabisa duniani ni huyo john heche wako ndio maana ameshindwa hata kujitafutia kipato chake cha kuishi mpaka akaomba chama kimlipie kodi ya nyumba yaani komu na slaa wamemlipia huyo heche wako kodi ya nyumba ya miezi 12 pale mabibo ili aendelee kuwa kibaraka wao.
sema ni wapi imethibitika kuwa slaa amepewa kashfa ya mke wa mtu ili impunguzie kura tu na sio uweli?...
mchange inaonekana anawachoma sana nyie wazee wa matamko...teh teh teh

Kwa kauli hizi zako yatosha kabisa kujua kuwa unasukumwa sana na chuki dhidi ya baadhi ya watu.Wewe unakanusha sasa ila mwenzako(au sijui ndiye wewe)alishindwa kujitetea ndani ya vikao halali juu ya hizo tuhuma.Alishindwa kuikana namba yake ya m-pesa na ujumbe mfupi aliomwandikia mjumbe wa Mwanza.Sasa nje ya vikao wadau wake ndo wanatoka mapovu mengi hivi?Mwizi akikiri kuiba na kurejesha alichokiiba na kupewa onyo asirudie bila kumpeleka mahakamani haimaanishi kuwa hakuiba.
 
Gumati, Mkukutwa, Mnyakatari na Hossam kwa haraka haraka naona kama ninyi ni wanachadema ama mko karibu na Mchange kwa upande mmoja na wengine wako upande wa Heche.
Mnachokifanya hapa ni kuharibu reputation ya chadema mbele ya wananchi na wanakibaha in particular.
Mchange aligombea uenyekiti wa bavicha na yaliyotokea kila mmoja anafahamu, hakuna sababu yoyote ya msingi kuendeleza malumbano yasiyokuwa na tija. Mchakato wa Uchaguzi ndani ya chama unaanza mwaka huu na kukamilika mwakani, Mchange awe mvumilivu kwakuwa bado anayo nafasi na umri unamruhusu.
Nafahamu kidogo kuhusu mkutano unaolalamikiwa kwamba Mchange hakuhusishwa, mkutano uliitishwa na bavicha mkoa wa Pwani na mwenyekiti wa bavicha mkoa ndiye alimualika Heche. Ni vizuri mkazijua taratibu za chama kuliko kuja kumshambulia hapa Heche na kumgombanisha Mchange na viongozi wake.
Naamini Mchange anafahamu taratibu za chama, ajiepushe na watu wanaomfarakanisha na viongozi wa kitaifa, watamharibia.
 
Thanks Machange kwakulitolea ufafanuzi, matarajio ya wengi ni kwamba utaendelea kuwa mmoja wa wanabadiliko wa tanzania, ukiendelea kutoa elimu ya demokrasia kwa wananchi wako kabla ya 2015 ili kuingia kwako bungeni kusiwe gharama sana wakati huo.
Nchi hii inahitaji kuwa na vijana wenye moyo wa kujitolea kuwatumikia wananchi, siyo matajiri.
Kumekuwa na matatizo ya kurubuniwa na serikali kurudisha kadi na kujiunga na magamba, vipi hili wewe halijakufikia?
wakuu.
nimeambiwa kuna post hapa jamvini ninatakiwa nitolee ufafanuzi. baada kwa umakini sioni kama kuna haja yoyote ya kutoa maelezo kwa kuwa yanayozungumzwa hapo yote ni maswala ya kufikirika tu.
sina haja ya kuanza kubishana na mtu yoyote nafasi yoyote na cheo chochote.
mimi ni mwanachama hai na makini wa chadema ila sina mkataba maalum wa kwamba nitakuwa mgombea wa milele wa chadema kibaha, mkataba pekee nilio nao ni mimi na wananchi wangu wanaoniunga mkono na kuniamini kwamba ni kifo tu kinachoweza kunizuia kuwa mbunge wao 2015. nasisitiza ni kifo tu kinachoweza kunizuia kuwa mbunge wa kibaha 2015 na sio ugombea.
kwa wale pangu pakavu tia mchuzi wanaoishi mjini kwa kutega masikio wasikie nani kasema nini ili wauze umbea kwa mabosi wao nawaomba waichukue hii kwa makini sana.
nimeitumikia siasa kwa muda mrefu wa kipindi changu cha utu uzima hivyo ni lazima kama ijana mwenye malengo niwe na matarajio.
simuogopi mtu yeyote kwenye kugombea nafasi yoyote ya kisiasa.
nawashukuru.
 
Kwa kauli hizi zako yatosha kabisa kujua kuwa unasukumwa sana na chuki dhidi ya baadhi ya watu.Wewe unakanusha sasa ila mwenzako(au sijui ndiye wewe)alishindwa kujitetea ndani ya vikao halali juu ya hizo tuhuma.Alishindwa kuikana namba yake ya m-pesa na ujumbe mfupi aliomwandikia mjumbe wa Mwanza.Sasa nje ya vikao wadau wake ndo wanatoka mapovu mengi hivi?Mwizi akikiri kuiba na kurejesha alichokiiba na kupewa onyo asirudie bila kumpeleka mahakamani haimaanishi kuwa hakuiba.
unachekesha sana ndugu yangu?...mbona mimi sijakuhisi kuwa wewe ni kubenea au heche...tujadiliane kwenye hoja tuwaache hao wasiokuwepo waendelee na shuhuli zao wanazoona zinafaa..mchange ameshatoa maelezo yake humu...yaonekana wewe unalako jambo..
kwa sisi tunaoifahamu vizuri chadema tunakwambia kuwa huyo bwana mdogo hakuwahi kukubali hayo mashtaka..keep in your mind kwamba kuchapisha nakala ama namba za simu za mpesa ama tigo pesa himaanishi kama ni kweli imetolewa rushwa?..angalia vizuri hiyo document kuna namba hadi za edward kinabo mle aliyeomba asaidiwe pesa na akasaidiwa kwa kiasi alichoomba kishkaji je nayeye amehongwa?...na kama amehongwa ili iwe nini?...ninamuunga sana mkono mchange kwa kuamua kukaa kimya kwenye hili sakata sababu mwishowake angeishia kuwaumbua wazee wake wa ndani ya chama tu..
kabla hujaandika chochote humu jamvini jaribu kutafakari mara mbili tatu hivi...
sakata la bavicha ni ishu nyingine na leo hapa tunajadili kuhujumiwa ama kushugulikiana kisiasa kibaha mjini...
jipange upya ndugu yangu...
 
Thanks Machange kwakulitolea ufafanuzi, matarajio ya wengi ni kwamba utaendelea kuwa mmoja wa wanabadiliko wa tanzania, ukiendelea kutoa elimu ya demokrasia kwa wananchi wako kabla ya 2015 ili kuingia kwako bungeni kusiwe gharama sana wakati huo.
Nchi hii inahitaji kuwa na vijana wenye moyo wa kujitolea kuwatumikia wananchi, siyo matajiri.
Kumekuwa na matatizo ya kurubuniwa na serikali kurudisha kadi na kujiunga na magamba, vipi hili wewe halijakufikia?

safi sana mkuu...ni kweli huyu bwana mdogo anaonyesha kuwa na kipawa cha kipekee na cha aina yake...anapaswa pia kuungwa mkono na wadau wengine ili tufikie lengo la kuwatoa magamba madarakani na sio vinginevyo..
ni bora tukaachana na majungu majungu hapa jamvini na kuwatia moyo hawa vijana wanaoamua kujitolea na kuharibu hata kyhatarisha maisha yao..
keep it up mchange
 
Gumati, Mkukutwa, Mnyakatari na Hossam kwa haraka haraka naona kama ninyi ni wanachadema ama mko karibu na Mchange kwa upande mmoja na wengine wako upande wa Heche.
Mnachokifanya hapa ni kuharibu reputation ya chadema mbele ya wananchi na wanakibaha in particular.
Mchange aligombea uenyekiti wa bavicha na yaliyotokea kila mmoja anafahamu, hakuna sababu yoyote ya msingi kuendeleza malumbano yasiyokuwa na tija. Mchakato wa Uchaguzi ndani ya chama unaanza mwaka huu na kukamilika mwakani, Mchange awe mvumilivu kwakuwa bado anayo nafasi na umri unamruhusu.
Nafahamu kidogo kuhusu mkutano unaolalamikiwa kwamba Mchange hakuhusishwa, mkutano uliitishwa na bavicha mkoa wa Pwani na mwenyekiti wa bavicha mkoa ndiye alimualika Heche. Ni vizuri mkazijua taratibu za chama kuliko kuja kumshambulia hapa Heche na kumgombanisha Mchange na viongozi wake.
Naamini Mchange anafahamu taratibu za chama, ajiepushe na watu wanaomfarakanisha na viongozi wa kitaifa, watamharibia.

sijakuelewa kidoupata muafaka muda si mrefu.go..
unaposema sisi sote ni wanachadema unamaanisha tukajadili kwenye vikao au?...
wacha tueleweshane humu ndani kuhusu haya mambo madogo madogo...tuwe tu wavumilivu tuta
 
Okey eleweshaneni hapa ndo penyewe, ila kaeni mkijua kama kuna mgombea ambaye alikutwa na kashfa ya rushwa hapo awali hatakua na nafasi ya kuwa mgombea kupitia CDM.
Kwa sababu hapa ndo JF naamini pia mtazidi kueleweshwa nani hastaili kuwa mgombea kupitia CDM na nani anastahili kuwa mgombea kupitia CDM.
Pia ambaye atakayekosa nafasi ya kuwa mgombea kupitia CDM atakuja hapahapa kuwaelewesha kwanini anaamini anastahili kuwa mgombea kupitia CDM.
Ila tumeshaeleweshwa na mgombea mtarajiwa kuwa "ugombea" sio issue kwake, sasa sioni sababu ya wapambe kulia zaidi kuliko mfiwa ili hali muhusika anajua option nyingi tu.
 
Wasiwasi wenu ndio unaowasumbua tu hakuna lengine lolote?..
swala ninaloliona hapa sio nani atagombea wapi na kwa nini, ninachokiona mimi ni vijana wengi humu jamvini kuamini katika kupiga majungu mwanzo mwisho.. ni vizuri umesema tuhuma za rushwa mimi nataka tufike mbele zaidi tusiishie tu kwenye tuhuma tuende mpaka kwenye vidhibiti vya hizo rushwa sio tuhuma manake kama tuhuma hata mbowe anatuhumiwa kuitapeli NSSF mabilioni ya shilingi lakini hajaenguliwa kugombea ubunge wala uenyekiti kwa sababu tu za tuhuma hizo..
cha msingi ni nyinyi kujipanga tu ki sawa sawa kuhakikisha mnamshinda mchange kibaha kama mnavyotaka iwe.
nawashauri pia mumshauri kubenea abadilishe mbinu ile ya kuchanga milioni moja moja misikitini na makanisani kama alivyofanya picha ya ndege na mikongeni haimsaidii kwa sababu anaowachangia wanamfananisha na LOWASSA tu kutumia njia hiyo.
kazi bado mnayo tena kubwa sana.
 
sijakuelewa kidoupata muafaka muda si mrefu.go..
unaposema sisi sote ni wanachadema unamaanisha tukajadili kwenye vikao au?...
wacha tueleweshane humu ndani kuhusu haya mambo madogo madogo...tuwe tu wavumilivu tuta

Sidhani kama umenielewa.
Mimi nimezungumzia taratibu za chama ktk suala la kuitisha mikutano na mialiko kwa viongozi wa ngazi ya taifa, kulingana mleta thread Hossam.
Kilichotokea baada ya mchange kutoa majibu yake nimeona ni mashambulizi tu ambayo ninaona kama hayatamsaidia mchange wala chama.

Hata kama nia ni kueleweshana hapa, kwa style hii nayoiona hapa hamtaelewana zaidi ya kujishushia heshima. Nimewaambia uchaguzi ndani ya chama ni mwaka huu, shida iko wapi tena?
 
Hossam na Mchange; you sound like mmepanga flani kufanya hichi mnachokifanya, any way time will tell.

kaka.
Mimi ni kama wewe tu.
nimeiona hii thread humu na nikatoa maelezo yangu kama nilivyoombwa kufanya hivyo.
ninachofahamu mimi inawezekana kuna watu humu jamvini wana motions zao wanataka kuzifikia kupitia majina ya watu.
mimi sifahamu lolote kama kuna mtu yoyote anataka kugombea kibaha mjini wala sina mamlaka ya kumzuia mtu yoyote agombee sio tu kibaha bali mahala popote pale isipokuwa nina misimamo na mipango yangu ambayo pamoja na watu tunaoaminiana ni kwamba 2015 sio ombi kuwa mbunge wa kibaha mjini bali ni lazima kwa sababu ambazo mimi ninazo na ninaziamini.
sasa kama kuna mtu yoyote anayenihofia kiasi cha kuanza kuja humu mitandaoni na kuwachanganya wadau wala asipate taabu wanakibaha wanajua wanachokifanya na ninamkaribisha sana aje tujenge chama.
wala hatuna haja ya kuzunguka humu ndani na kuuma uma maneno kana kwamba uchaguzi unafanyika kesho ama kana kwamba ni dhambi mtu kutamani kugombea jimbo lolote. cha msingi ni yeye tu mwenyewe tu kujifanyia tathmini kuwa anajionaje kuvamia jimbo lililoandaliwa na wanaume wenzie wakati kuna majimbo kibao yanapita bila kupingwa? ni vitu tu vya kujiuliza na kufanya maamuzi mepesi bila hata kushikiwa fimbo.
kwangu mimi nyekundu ni nyekundu na njano ni njano sijaumbwa kuwa mnafiki na wala sitakuja kuwa mnafiki katika maisha yangu yote.
ninaamini katika kile ninachokisimamia.
wabillah tawfiq
 
kaka.
Mimi ni kama wewe tu.

wala hatuna haja ya kuzunguka humu ndani na kuuma uma maneno kana kwamba uchaguzi unafanyika kesho ama kana kwamba ni dhambi mtu kutamani kugombea jimbo lolote. cha msingi ni yeye tu mwenyewe tu kujifanyia tathmini kuwa anajionaje kuvamia jimbo lililoandaliwa na wanaume wenzie wakati kuna majimbo kibao yanapita bila kupingwa?
wabillah tawfiq

Hizo kauli kwenye wekundu ni contradictory!
 
Wasiwasi wenu ndio unaowasumbua tu hakuna lengine lolote?..
swala ninaloliona hapa sio nani atagombea wapi na kwa nini, ninachokiona mimi ni vijana wengi humu jamvini kuamini katika kupiga majungu mwanzo mwisho.. ni vizuri umesema tuhuma za rushwa mimi nataka tufike mbele zaidi tusiishie tu kwenye tuhuma tuende mpaka kwenye vidhibiti vya hizo rushwa sio tuhuma manake kama tuhuma hata mbowe anatuhumiwa kuitapeli NSSF mabilioni ya shilingi lakini hajaenguliwa kugombea ubunge wala uenyekiti kwa sababu tu za tuhuma hizo..
cha msingi ni nyinyi kujipanga tu ki sawa sawa kuhakikisha mnamshinda mchange kibaha kama mnavyotaka iwe.
nawashauri pia mumshauri kubenea abadilishe mbinu ile ya kuchanga milioni moja moja misikitini na makanisani kama alivyofanya picha ya ndege na mikongeni haimsaidii kwa sababu anaowachangia wanamfananisha na LOWASSA tu kutumia njia hiyo.
kazi bado mnayo tena kubwa sana.

Hapo kwenye red tafuta mtu anaitwa Ben yupo huku JF alishiriki uchaguzi huo wa BAVICHA atakujuza in detail;
Otherwise ungekuwa na tabia ya kujisomea usingepoteza mda wako mwingi kunitolea mfano wa lowasa nakadhalika.
 
Hizo kauli kwenye wekundu ni contradictory!
ndo ondoa wewe sasa hiyo contradictory unayoiona..
kwangu mimi naona mchange ameeleza vizuri kabisa na ameeleweka kisawa sawa.
hakuna haja ya yeye kuonyesha uwoga wowote wakati anafahamu nini anachokifanya na ni kwanini.
Hongera mchange kwa ufafanuzi zaidi..i wish ungeenda mbali zaidi ukawabomoa watu fulani fulani wasiotakia heri vijana kwa maslahi ya mabosi wao...
they are almost done.
 
Hapo kwenye red tafuta mtu anaitwa Ben yupo huku JF alishiriki uchaguzi huo wa BAVICHA atakujuza in detail;
Otherwise ungekuwa na tabia ya kujisomea usingepoteza mda wako mwingi kunitolea mfano wa lowasa nakadhalika.

tatizo n nini sasa hapo?....kuombwa kufika mbali zaidi au kumwambia huyo bwana kubenea kutumia milioni moja moja kwenye michango ya misikiti na makanisa kama anavyofanya lowassa ndo hiyo wewe imekuuma sana?.
 
ndo ondoa wewe sasa hiyo contradictory unayoiona..
i..i wish ungeenda mbali zaidi ukawabomoa watu fulani fulani wasiotakia heri vijana kwa maslahi ya mabosi wao...

Contradictory ninayoiona? Karibu FB kama hujajisajili!
 
Duh Mchange!

Mara ya kwanza nilitaka kuamini kuwa wewe unaweza kuwa kiongozi, lakini kwa majibu yako haya huwezi kuwa na hufai hata kidogo. Hivi ni kiongozi gani anayeweza kusema kitakachomzuia kuwa mbunge wa Kibaha mjini ni kifo tu. Be serious bwana. Ina maana nafasi ya wapiga kura unaipeleka wapi mkuu? Eti unasema kwa mbinu unazozijua mwenyewe. This is non sense. Nilitegemea ungesema wananchi wataamua sasa haya mambo ya kujiapiza yametoka wapi. You have been always preaching in being democratic 'as you call njano to be njano or nyekundu to be nyekundu' and yet you can not practise it. Kweli Tanzania tuna kazi! Hivi unadirikiaje kusema eti jimbo limeandaliwa na wanaume na mtu mwingine asiwe na halki ya kugombea? Wewe vipi bwana, unamtisha nani? Kama ni kuandaliwa hata wewe usingegombea basi maana tayari ulikuta kulikuwa na watu. Naweza kubashiri kuwa wewe ukiwa madarakani kwa msemo wako wa mbinu unazozijua mwenyewe utakuwa kama Gadhafi au madikteta wengine wowote wanaong'ang'ania madaraka kwa nguvu zao zote.

Nakushauri angalia upya hizo mbinu zako na claim zako za hati miliki ya Jimbo la Kibaha

Regards
 
[h=1]Masalia ya Zitto yapukutishwa CHADEMA[/h]
picture-9.jpg

Na Alfred Lucas - Imechapwa 01 June 2011

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ililazimika kujigeuza mahakama ili kusikiliza malalamiko dhidi ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho (BAVICHA).
Katika kusikiliza malalamiko hayo, Kamati Kuu iliwateua wanasheria wake mashuhuri, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari kuwa majaji wa kuendesha kesi ya Habibu Mchange aliyekuwa anawania nafasi ya mwenyekiti.
Mchange ambaye anajitambulisha kuwa ni mfuasi wa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe lilalamikiwa na mwenyekiti wa BAVICHA mkoani Mwanza, Liberatus Mlebele kukiuka maadili ya uchaguzi, ikiwamo kusafirisha wajumbe wa mkutano wa uchaguzi kutoka mikoani hadi Dar es Salaam.
Ndani ya CC, Mchange alilazimika kujibu tuhuma moja baada ya nyingine ikiwamo malalamiko ya kushindwa kuwajibika yaliyofunguliwa na katibu wa BAVICHA jimbo la Kigamboni.
Katibu huyo alimtuhumu Mchange kushindwa kutimiza wajibu wake kwa kile alichoeleza, “Tangu achaguliwe kushika nafasi ya mwenyekiti wa BAVICHA wilayani humo hajahudhuria vikao.”
Mjumbe mmoja wa CC amedokeza gazeti hili kuwa Mchange ambaye alionekana kuwa na wafuasi wengi, alikatwa kwa kuwa alishindwa kujitetea mbele ya mahakama ya CHADEMA.
Kwa mfano, kati ya 20 Mei na 25 mwaka huu, Mchange alituma zaidi ya Sh. 2, 561,000 kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana kutoka katika mikoa mbalimbali nchini. Fedha hizo zilitumwa na Mchange mwenyewe kupitia mtandao wa M-Pesa na Tigo Pesa.
Namba ya Mchange iliyotumika kusambaza fedha hizo, ni 0658 178678. Alianza kutapakanya fedha kwa wajumbe 11 Mei 2011 saa 10:44.58 ambapo kiasi cha Sh. 28,500 zilitumwa kwa mmoja wa wajumbe wenye simu Na. 0659 374206.
Baadaye saa 11:04.24 alituma Sh. 15,500 kwenda Na. 0659 374206 na kisha 20 Mei 2011 saa 14:03.04 alituma Sh. 19,000 kwa mwenye Na. 0713 866650.
Tarehe 23 Mei 2011 saa 10:56.06, nyaraka zinaonyesa Mchange alituma Sh. 50,000 kwenda kwa mwenye Na. 0713 867745; tarehe 21Mei 2011 saa 11:54.47 alituma Sh. 40,000 kwenda kwa mwenye Na. 0717 268576 na saa 12:41.48 alituma Sh. 81,000 kwa mwenue Na. 0714 038536.
Wengine waliotumiwa fedha na Mchange; ni wenye Na. 0712 511508 aliyetumiwa Sh. 26,000 na mwenye Na. 0713 606169 aliyetumiwa Sh. 10,000 ambaye alitumiwa fedha hizo, saa 22:24.31.
Nyaraka za M-PESA zinamuonyesha Mchange akimtumia Peter Shiyo, mwenyekiti wa BAVICHA wilayani Maswa Sh. 50,000. Fedha hizo zilitumwa 23 Mei 2011 saa 16:39.
Tarehe hiyo 23 Mei 2011 saa 18:48, Mchange alituma kiasi cha Sh. 30,000 mwenyekiti wa vijana wilaya ya Singida Mjini, Wilfred Kitundu.
Aidha, siku hihiyo Mchange akitenda kama karani wa benki alituma Sh. 150,000 kwa mwenyekiti wa baraza hilo mkoani Mwanza, Liberatus Mlebele.
Mara baada ya kupokea fedha hizo, Mlebele aliwasilisha malalamiko kwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa akimtuhumu Mchange kumshawishi kwa njia ya rushwa ili amchague kuwa mwenyekiti.
Katika barua yake hiyo, Mlebele pamoja na mambo mengine alisema, “Ninakuandikia kwa nia njema kabisa ya kulinda hadhi ya chama chetu nikiomba maelekezo yako kama mtendaji mkuu wa chama.”
Anasema, “Tarehe 28 Mei 2011 Baraza la Vijana wa chama chetu litafanya uchaguzi wa viongozi wake wa kitaifa. Je, sisi wajumbe tumegharamiwa na chama ama wagombea kufika Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi huu?
Alisema, “Ninauliza hivi kwa sababu tayari mmoja wa wagombea ameshaniagiza kufika Dar es Salaam kwa gharama zake ili kukagua hoteli ambayo wajumbe wa mkoa wangu na kwingineko watafikia hali ambayo ninaihesabu kama rushwa.”
Mlebele alisema katika barua yake, “Niko tayari kutoa vielelezo sahihi juu ya kitendo hiki kama itabidi, ili kulinda hadhi ya chama chetu dhidi ya watu hatari kama hawa.”
Alisema, “Kwa kuwa mimi binafsi sipendi rushwa na siwezi kuvumilia vitendo vya rushwa na kwa kuwa natambua chama chetu kimekuwa kinara wa kupambana na rushwa nchini, ninaomba kamati kuu ichukue hatua stahiki dhidi ya mtu huyu ili kulinda hadhi ya baraza na chama chetu mbele ya wananchi.”
Ni maelezo hayo ya Mlebele yaliyozika ndoto za Mchange kuwa mwenyekiti wa BAVICHA. Taarifa zinasema Dk. Slaa aliwasilisha malalamiko yote mbele ya wajumbe wa CC. Barua ya Mabele iliwasilishwa kwa Dk. Slaa, 26 Mei 2011.
Taarifa zinasema kabla ya CC kujigeuza mahakama ya kusikiliza shauri hilo, mjumbe mmoja alinukuliwa akimtetea Mchange. Hata hivyo, alizimwa na Dk. Slaa aliyesimama kidete kutaka chama chake kichunguze suala hilo na kichukue hatua.
Katika barua yake, Mlebele anasema alifikia katika hoteli ya Bondeni One iliyoko Magomeni. Anamtaja Mchange kuwa ndiye aliyelipa fedha hizo. Alitoa nakala ya kitabu cha wageni kuthibitisha kuwa fedha hizo zililipwa na aliyemteja.
Mchange alikiri mbele ya wajumbe wa CC kuwa ni kweli kwamba simu iliyotajwa kupeleka fedha ni yake; alimhonga Mlebele kiasi kilichotajwa, alilipia sehemu ya gharama za hoteli na alikiri kumuagiza akusanye wajumbe wa mkutano wa uchaguzi.
Kamati kuu ya CHADEMA ilipitisha majina ya wagombea tisa katika nafasi ya mwenyekiti na kisha kukasimu madaraka yake kwa kamati ya wazee kwa hatua nyingine inazoona zinafaa.
Ni kupitia kamati hiyo, ndiko wagombea wengine watatu walifyekwa. Waliopatwa na panga la kamati hiyo iliyokuwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani na mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando, ni Mtela Mwampamba, Bernard Saanane na Grayson Nyakarugu, huku John Heche akionywa na na kuelezwa ikibainika alifanya vitendo kinyume cha maandili, atavuliwa madaraka.
Wote waliokatwa walipatikana na makosa ya rushwa, kutoaminika, kupanga matokeo, makundi na kutumiwa na watu wa kutoka nje ya baraza la vijana.
Akifanya marejeo ya kilichofanyika Jumamosi katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke, jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema chama chake kimeweza kunasua mitego yote ya rushwa iliyopandikizwa na CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom