Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.

Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.

Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.

Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.

Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.

Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.

Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.

I'M on the team man!!!!!
 
Lowassa ni Tajiri sana hata kabla hajawa waziri mkubwa. Nitashangaa kama tajiri anaulizwa kuwa pesa anatoa wapi. Tatizo la Lowassa na baadhi ya viongozi wengine matajiri ni pale wanaposhindwa ku declare interests zao in time. EL anamiliki ma estate nyingi hapa Arusha, ana Shares kubwa kwenye makampuni ya utalii kama vile Leopard nk.

His he among big tax payers?
 
Pasco, kuwa mwizi si kuiba tu bali hata kushirikiana na mwizi pia ni wizi.

Lowasa ndiyo ni mtendaji mzuri sana na pia ni mfuatiliaji wa karibu wa mambo. Lakini katika hili skendo la Richmond hakuwa na sababu ya yeye kukubali kubebe zigo la wezi kama yeye si mwizi, lakini kwa sababu alikubali kubeba zigo la wezi kwa lengo la kuwalinda wezi hao basi na yeye ni mwizi unless proved otherwise. Na Tanzania hatuko tayari kuongozwa na wezi tena kwani tumeshaibiwa vya kutosha. Unasema kwamba ndani ya CCM wote wezi ila Lowasa ana unafuu kidogo, basi tuiweke CCM yote kando kwani si lazima nchi iongozwe na CCM.
 
Hela za Lowasa ni za wizi na ufisadi alizozipata kwa maraka ya umma aliyoshika na ni mnaomtetea humu mmenulnuliwa kwa hizo hela za kifisadi na anatafuta uraisi ili aibe zaidi na kufilisi nchi hamna lolote kama utenda kazi wapo watanzania wengi wazuri na watenda kazi bora siyo wezi kama Lowasa wenu na acheni upuuzi wa kumtetea humu JF watanzania si wajinga tena kama mnavyofikiria wapuuzi na wajinga wote mnaomtetea wakati unajua uhalisia wake ni mwezi na fisadi kubwa na siyo kwa deal la richmond tu
 
Lowassa ni mwizi kama walvyo wezi wngine wengi walioko CCM wakiwemo Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Kwete, Mwang'onda n.k

Sema yeye kazidi kuwa na mipesa kwasababu kila anachokifanya anawaza pesa....jengo la umoja wa vijana amepata % yake kubwa mno, na madili mengie kama hao....
Tofauti yake na wengine, nikwamba hawi bize sana na mademu japo mara chache huonekana na kina Frola Mbasha, sijui anafanya nini nao!!?? .........Ilhali wezi wengine kama JK muda mwingi huwa pia mademu, Ben sometimes hutaka kutubu,..Mzee Mwinyi kakabidhi sana mali kwa wake zake wengi na wanae wengi....
Ndio hayo tu, kwa kifupi japo yapo mengi mno!
 
Pasco, kuwa mwizi si kuiba tu bali hata kushirikiana na mwizi pia ni wizi.

Lowasa ndiyo ni mtendaji mzuri sana na pia ni mfuatiliaji wa karibu wa mambo. Lakini katika hili skendo la Richmond hakuwa na sababu ya yeye kukubali kubebe zigo la wezi kama yeye si mwizi, lakini kwa sababu alikubali kubeba zigo la wezi kwa lengo la kuwalinda wezi hao basi na yeye ni mwizi unless proved otherwise. Na Tanzania hatuko tayari kuongozwa na wezi tena kwani tumeshaibiwa vya kutosha. Unasema kwamba ndani ya CCM wote wezi ila Lowasa ana unafuu kidogo, basi tuiweke CCM yote kando kwani si lazima nchi iongozwe na CCM.
Kidatu, there you are!. Urais 2015 ni vita!. Watanzania tuna haki na utajiri wa mali asili zetu tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambazo hawa manyang'au waliopo wamezitoa sadaka kwa wanaojiita wawekezaji, huku wakikomba kila kitu na kutuacha beggera!. Tanzania sio masikini kihivyo!. Kwa vile Tanzania yenye utajiri na neema ni haki yetu, na haki hiyo hatutaletewa kwenye kisahani cha chai, ni lazima tuipiganie, haki hailetwi, bali inadaiwa na ikibidi inapiganiwa na ndipo inapatikana!.

Wengi wa wanaotamani ukombozi wa kweli, wanautamani wakiamini siku moja ukombozi huo utashushwa toka mbinguni na sisi kutunukiwa kama ile mikate ya mana enzi za Nabii Mussa!. Mimi nasema, haki hiyo lazima itafutwe, idaiwe, ipiganiwe na hata ikibidi damu za watu zimwagike ili ipatikane!.

Kwa wale tunaokubaliana kuwa urais 2015 ni vita, na ili ushinde vita lazima umjue adai yako, kwenye vita hivi vya ukombozi wa pili, adui yetu number moja ni CCM!. Sasa wale wote wanaodhania serikali ya CCM itaotoa utawala kwa wapinzani kama zawadi!, they are wrong!, CCM would wish to consolidate power ili itawale milele!. Kwa vile CCM does exist, mimi ni muumini wa falsafa ya Baba wa Taifa kuwa ukombozi wa kweli wa nchi hii utatokana na upinzani wa kweli ambao utatoka CCM!.

Mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, we can see a light on Lowassa, huyu ndie mtu pekee anaweza kuleta ukombozi wa kweli!. Hivyo tunampigania kwa nguvu zetu zote!.

Kitendo cha Lowassa kukubali kubeba zambi za wengine ili CCM iokoke ni uthibitisho wa ushajaa mkubwa alionao ambao mimi naufananisha na Bwana Wetu Yesu Kristu kukubali kubeba dhambi za ulimwengu ili sisi tuokoke!.

Wale mnaosema kwa Lowassa kubeba zambi za wezi, hivyo na yeye ni mwizi!, jee Yesu alivyokubali kubeba zambi za ulimwengu, jee na yeye ni mzambi!. Wajameni tusihukumu tusije tukahukumiwa!.

Naendelea kusisitiza, wale wote mnaoniaminia mimi Pasco wa jf, nawaombeni sana lets bank on Lowassa as the one and only anaweza kuleta mabadiliko ya kweli na tukapata 'ukombozi wa pili'!

Wale wote mnaonibeza na kuamini nimelipwa, nimenunuliwa, najikomba etc, endeleeni kuamini hivyo, kwa kuwasaidia tuu,
kwa wasionijua, tangu enzi za utotoni, pale Msasani kwa Mwalimu ilikuwa ni playing ground yetu!, sekondari nimesoma na mtoto wa kwa Mwalimu, nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben, wakati huo mtoto wa Mwinyi akiwa A-Level, Chuo Kikuu nimekutana na mtoto wa JK, hivyo ile access ya one to one na Nyerere (RIP), Mwinyi, Mkapa na JK has/is always there, hivyo kama ni lobbyst ya kujipatia kijipost chochote, basi ningeshalobby zamani na labda saa hizi ningekuwa kivulini!.

Lowassa ni sikio la kufa, sasa nijikombe kwa Lowassa ili nipate nini?. Naombeni mniaminie, kuna type ya watu ambao wao ni masikini na wanaridhika na umasikini wao, hawa wanaitwa "masikini jeuri" na mimi niko kwenye kundi hilo!. Sijalipwa senti tano na yoyote kumpigania Lowassa!.

Namalizia kwa msisitizo, Lowassa ni chaguo la Mungu, lile ambalo kwa binaadamu haliwezekani, kwa Mungu linawezekana!. Subirini mshuhudie "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".
 
Kama Lowassa ni msafi

1.Kwa nini alifukuzwa ukurugenzi wa AICC kwa kujilimbikizia mali ?,alifukuzwa na Juliasi Nyerere.

2.Kwa nini alijiuzulu kwa sakata la Richmond ambalo nyie mnadai hakuhusika,na kwa nini ameendelea kuficha ukweli hadi sasa kama ni mtu anayetakia mema taifa hili? mbaya zaidi kwa unafiki wake alidai anajiuzulu kwa sababu watu wanautaka uwaziri mkuu wake.

3.Atakuwaje mkombozi wa pili na wakati amekuwapo kwenye serikali kwa miaka mingi sana na hatujaona "something so special" from him?.Afadhali hata magufuli tunaona impact kila sehemu anayoenda.

4.Ni maamuzi magumu gani ambayo mnasema Lowassa ameyafanya? Usitaje kujiuzulu kwa sababu hayo pia ni maamuzi magumu kama ya jambazi anayeenda kuvunja nyumba ya mtu.Amejiuzulu ili kuendelea kulindana na aidha wezi wenzake au wazembe wenzake

Until unijibu maswali haya kiufasaha,ntahamia rasmi kwenye kambi ya Lowassa.

Ndio maana nyerere alimkataa kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka 1995. kwasababu alimjua kuwa si msafi.
 
Kama Lowassa ni msafi

1.Kwa nini alifukuzwa ukurugenzi wa AICC kwa kujilimbikizia mali ?,alifukuzwa na Juliasi Nyerere.

2.Kwa nini alijiuzulu kwa sakata la Richmond ambalo nyie mnadai hakuhusika,na kwa nini ameendelea kuficha ukweli hadi sasa kama ni mtu anayetakia mema taifa hili? mbaya zaidi kwa unafiki wake alidai anajiuzulu kwa sababu watu wanautaka uwaziri mkuu wake.

3.Atakuwaje mkombozi wa pili na wakati amekuwapo kwenye serikali kwa miaka mingi sana na hatujaona "something so special" from him?.Afadhali hata magufuli tunaona impact kila sehemu anayoenda.

4.Ni maamuzi magumu gani ambayo mnasema Lowassa ameyafanya? Usitaje kujiuzulu kwa sababu hayo pia ni maamuzi magumu kama ya jambazi anayeenda kuvunja nyumba ya mtu.Amejiuzulu ili kuendelea kulindana na aidha wezi wenzake au wazembe wenzake

Until unijibu maswali haya kiufasaha,ntahamia rasmi kwenye kambi ya Lowassa.

Mimi si shabiki wa EL lakini ukilinganisha na viongozi wengine ndani ya CCM yeye ni bora zaidi. Ni viongozi wangapi wamekumbwa na kashfa na kuundiwa tume mwishowe wanadunda. Tunaona hata wenzetu katika nchi zilizoendelea wakituhumiwa kwa kashfa huchukua jukumu la kuachia ngazi kitendo hiki ni uwajibikaji wa hali ya juu.
 
Kidatu, there you are!. Urais 2015 ni vita!. Watanzania tuna haki na utajiri wa mali asili zetu tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambazo hawa manyang'au waliopo wamezitoa sadaka kwa wanaojiita wawekezaji, huku wakikomba kila kitu na kutuacha beggera!. Tanzania sio masikini kihivyo!. Kwa vile Tanzania yenye utajiri na neema ni haki yetu, na haki hiyo hatutaletewa kwenye kisahani cha chai, ni lazima tuipiganie, haki hailetwi, bali inadaiwa na ikibidi inapiganiwa na ndipo inapatikana!.

Wengi wa wanaotamani ukombozi wa kweli, wanautamani wakiamini siku moja ukombozi huo utashushwa toka mbinguni na sisi kutunukiwa kama ile mikate ya mana enzi za Nabii Mussa!. Mimi nasema, haki hiyo lazima itafutwe, idaiwe, ipiganiwe na hata ikibidi damu za watu zimwagike ili ipatikane!.

Kwa wale tunaokubaliana kuwa urais 2015 ni vita, na ili ushinde vita lazima umjue adai yako, kwenye vita hivi vya ukombozi wa pili, adui yetu number moja ni CCM!. Sasa wale wote wanaodhania serikali ya CCM itaotoa utawala kwa wapinzani kama zawadi!, they are wrong!, CCM would wish to consolidate power ili itawale milele!. Kwa vile CCM does exist, mimi ni muumini wa falsafa ya Baba wa Taifa kuwa ukombozi wa kweli wa nchi hii utatokana na upinzani wa kweli ambao utatoka CCM!.

Mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, we can see a light on Lowassa, huyu ndie mtu pekee anaweza kuleta ukombozi wa kweli!. Hivyo tunampigania kwa nguvu zetu zote!.

Kitendo cha Lowassa kukubali kubeba zambi za wengine ili CCM iokoke ni uthibitisho wa ushajaa mkubwa alionao ambao mimi naufananisha na Bwana Wetu Yesu Kristu kukubali kubeba dhambi za ulimwengu ili sisi tuokoke!.

Wale mnaosema kwa Lowassa kubeba zambi za wezi, hivyo na yeye ni mwizi!, jee Yesu alivyokubali kubeba zambi za ulimwengu, jee na yeye ni mzambi!. Wajameni tusihukumu tusije tukahukumiwa!.

Naendelea kusisitiza, wale wote mnaoniaminia mimi Pasco wa jf, nawaombeni sana lets bank on Lowassa as the one and only anaweza kuleta mabadiliko ya kweli na tukapata 'ukombozi wa pili'!

Wale wote mnaonibeza na kuamini nimelipwa, nimenunuliwa, najikomba etc, endeleeni kuamini hivyo, kwa kuwasaidia tuu,
kwa wasionijua, tangu enzi za utotoni, pale Msasani kwa Mwalimu ilikuwa ni playing ground yetu!, sekondari nimesoma na mtoto wa kwa Mwalimu, nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben, wakati huo mtoto wa Mwinyi akiwa A-Level, Chuo Kikuu nimekutana na mtoto wa JK, hivyo ile access ya one to one na Nyerere (RIP), Mwinyi, Mkapa na JK has/is always there, hivyo kama ni lobbyst ya kujipatia kijipost chochote, basi ningeshalobby zamani na labda saa hizi ningekuwa kivulini!.

Lowassa ni sikio la kufa, sasa nijikombe kwa Lowassa ili nipate nini?. Naombeni mniaminie, kuna type ya watu ambao wao ni masikini na wanaridhika na umasikini wao, hawa wanaitwa "masikini jeuri" na mimi niko kwenye kundi hilo!. Sijalipwa senti tano na yoyote kumpigania Lowassa!.

Namalizia kwa msisitizo, Lowassa ni chaguo la Mungu, lile ambalo kwa binaadamu haliwezekani, kwa Mungu linawezekana!. Subirini mshuhudie "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".

Hakuna kipya unachongelea ambacho watz hatukijui. Huo usemi wa CHAGUO LA MUNGU NDIO UNAOTUTOKEA PUANI. BADILISHA STRATEGIES....
 
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?
sijui ni kwanini Nyerere alihoji kuhusu mali za Lowassa japo wakati huo kulikuwa na wana-ccm wengi tu waliokuwa na mali zisizo na maelezo, pia kuna waliofisadi zikaishia kwenye zip na matumbo hao hakuhoji
 
Hakuna kipya unachongelea ambacho watz hatukijui. Huo usemi wa CHAGUO LA MUNGU NDIO UNAOTUTOKEA PUANI. BADILISHA STRATEGIES....
Okada, utakuwa umechanganya mambo bila kujijua, JK alikuwa ni chaguo la mungu, Lowassa yeye ni chaguo la Mungu!.
 
Utajiri wake umeletwa na rasimali zetu waTz na kuhusu anavyotoa misaaa sasa na hakufanya hivyo wakati wa uwaziri wake mkuu ni kujisafisha na kujikombeleza kwa watanzania na viongozi wa dini ili nae aitwe chaguo la Mungu na najua endapo akiingia ikulu hizo hela zilizomgarim kwenye michango lazima zirudi
 
El akiingia madarakani nchi hii itakua na maendeleo, at the minimum mwelekeo mzuri kama Rwanda ya Kagame ilivyo.
Jamaa siyo muoga, mfuatiliaji na mtekekezaji. Kuna vitu vingine vya kiijinga tu vinafanywa na JK haviingii akilini, Mwakyembe kwa mfano alikua analalamika Bungeni eti Rais alidanganywa na NMB kwamba imechangia hela ya miradi ya maendeleo Kyela na kumkabidhisha Rais hundi FEKI awape wananchi wa Kyela!!!! Huyu ni Rais wa nchi anafanyiwa hivyo na yeye yupo kimya tu.
El hana sifa za kijinga hivyo, alienda Kigoma kwa DC Mongela alikataa kusomewa taarifa ya maendeleo, alikua anataka aone hayo maendeleo, siyo kusomewa taarifa na kuimbiwa kwaya na kuangalia ngoma na kupanda ndege na kurudi zake.
Watu wengi wanaompinga Lowassa wanapenda status quo na wakati huohuo wanalalamika maendeleo hakuna.
Ni taahira peke yake anayefanya kitu hichohicho kila siku na kutegemea matokeo tofauti.
 
Unajua ktk hili sakata la richmond, lowasa alifanya kosa sana kubeba mzigo ambao si wake. Hapa alikuwa anapaswa kutumia falsafa ya kila mtu atabeba msalaba wake. Binafsi namlaumu sana lowasa kwa hilo. Ona sasa tunamuhitaji atutoe hapa lakini ndo anakutana na vikwazo ambavyo vinamchafulia. Hapa yapaswa huyu jamaa tumsamehe ili tumtumie atuvushe hapa tulipo. Lowasa usivunjike moyo kwa kuwa wewe unaweza ukawa mtu sahihi wa kututoa hapa tulipo.
acha unafiki,atutoe hapa atupeleke wapi? labda shimoni! lowasa hafai kwa kuchovya wala kwa kulumangia kama rafiki yake. ukweli ni kwamba hawa jamaa ni mafisadi hata shetani anajua hilo.najua kuelekea 2015 wengi wenu mtanunuliwa naye na wengine tayari kama askofu fulani hivi wa kanisa lililoko pale posta
 
Pasco,

Nimepita tu ... ninaogopa kuuliza maswali maana huwa unayakwepa.
 
Nina maswali matatu tu kwa pro EL;
1. Kwani ndani ya CCM hakuna mtu mwingine zaidi ya EL?
2. Kwa nini EL anautaka SANA urais?
3. Kama anataka kuwasidia wa TZ, hawezi kusaidia kwenye capacity nyingine?

Nitafurahi nikijibiwa ili niweze pima kina cha maji!
 
1. At leaast in theory nchi hii ni ya kidemokrasia. Watu wengine wanapendelea El awe kiongozi wao, na wewe mpendelee wako.
2. Hataki sana madaraka. Kama umesahau, aliacha Uwaziri Mkuu bila kushurutishwa.
3. Anafanya hivyo sasa hivi kwa kuchangia miradi ya maendeleo, mfano ujenzi wa shule ya BAKWATA huko KIgamboni na ujenzi wa shule za wasichana wa Kimasai huko Monduli. Lakini ataweza kusaidia mengi zaidi na wengi zaidi akiwa Ikulu kuliko serikali ya sasa yenye kusaidia wachache. Historia yake inaonyesha hivyo.
 
Lowasa ni mtu alibahatika kujenga nyumba 3 katika kipindi cha awamu ya kwanza nyumba 1 ikiwa monduli na 2 dar moja wapo akiwa kajenga masaki wakati hiyo ya masaki wakati anaimalizia ndo nchi ya africa kusini inapata uhuru ubarozi wa A.kusini ukapanga pale kwa ghalama ya dora 8000 kwa mwezi.bahati nyingine wakati kampuni ya vodacom inaingia nchini aliweza chukua mkopo kwa kutumia nyumba yake hiyo ya masaki na kupata sh.200 mln zilizo muwezesha kuanzisha kampuni ya Alfatell ambayo ni vodacom provader inayo muingizia sh.4.5bln kwa mwaka mwanae akiwa ndo mkurugezi kwa ufupi hiyo ndo jeuri ya pesa ya Lowasa
 
Back
Top Bottom