Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,876
- 2,740
jana wakati natazama taarifa ya habari ITV niliona hayo maaandishi kwa chini kuwa Jakaya sasa ni PhD holder. wadau mtuambie, since when? au ndio zile za online? au ndio zile za heshima?
kama ni stahili hii nadhani kuna watu kibao wanazistahili hizi hapa bongo na kwingineko
Ni doctorate ye heshima aliyopewa na Jomo Kenyatta University kutokana na mchango wake wa kuleta amani Kenya baada ya vurugu ziizotokea baada ya uchaguzi wa 2008
Hi Hater!
amani iliyoko kenya na hapa TZ zina tofauti gani? kigezo cha kuigundua amani ni kipi? mbona hatujampa ya hapa kwetu kwa kuidumisha hiyo amani? watanzania tuna amani? nikipata haya majibu nitasuuzika kweli
Hi Hater!
Waulize hicho chuo cha Kenya wata kuambia vigezo walivyo tumia kumpa hiyo doctorate. Tanzania hatuwezi kumpa doctorate ya kudumisha amani kwa sababu hiyo amani kaikuta na ni wajibu wake kama raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kudumisha hiyo amani.
mambo mengine haya hitaji hata kupoteza muda mnajadili, kama wamempa PhD si yake na sidhani inaharibu nini kwa nchi yake. Sisi tunacho mgombeza JK ni kutoshughulikia kero za waTZ, mambo ya degree zake ni yake binafsi.
Phd zingine muangalie pa kuziweka.Pengine wala hazifit.Hivi kweli JK kuitwa Dr.hata kama ni wa bure nyie na hao waliompa mnamwonaje mtu huyu?Siyo kwamba inapwaya kabisa si mahali pake???
Heshima Mbele kwa Wadau na wachangiaji woote wa JF, nimekuwa nikifuatilia kwa kipindi kirefua sana forum hii na michango na post mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwekwa humu, nyingi zikiwa za kuelimisha jamii juu ya yale yanayoendelea TZ, Africa na Dunia kwa ujumla, Hongereni sana kwa kazi hii njema ya kuelimisha jamii,
nami kwa kujiunga leo hii nitajitaidi kwanza kujielimisha na michango mbalimbali humu lakini pia kuweza kutoa nami mawazo au mchango japo mdogo kwa wanajamii kuchangia kwa lengo la kupanuana mawazo.
Ningali mgeni jamvini japo sina kamba mguuni naomba kuelimishwa namna njema au hatua za kuanza kupost mijadala kwa wana jamii kuanza kuchangia, bado sijajua namna ya kuanza mbali ya kouna hii Quick Reply.
Asanteni.
kama ni stahili hii nadhani kuna watu kibao wanazistahili hizi hapa bongo na kwingineko
hahahah... mkuu heshima mbele. yaaani hii kuuliza yote ni sababu JK ama? acheni chuki za kishamba mbona waliopita karibia wote walikuwa nazo.Kwani PhD yake wewe inakufisadi nini hasa?
bahati ya kumjadili imemdondokea yeye safari hii