Mh Diallo, wafanyakazi wote Sahara Media Group ilikuwaje kura za ubunge Ilemela hazikutosha?

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Kumbe Media Group inawafanyakazi kibao Mwanza, nimebaini leo wakituma salamu za Krismasi.Ilikuwaje Mh. Diallo akapigwa mweleka na kijana mdogo wa kichaga Mh. Kiwia wa CHADEMA. Wafanyakazi wake hawakuwa mtaji wake?.
 
Alikuwa bize na mikakati ya kuhakikisha Masha hashindi Nyamagana na alikuwa na kebehi kwa wapiga kura wake akijua atashinda na hapohapo Masha alikuwa bize kuhakikisha Diallo hashindi Ilemela nayeye pia alikuwa na kajeuri kawajibu watu ovyo.Kwahiyo watu walichukizwa na dharau zile halafu Ongeza pale upepo wa dr.slaa ulivyotikisa kila kona utaona kwanini kura hazikutosha.Siasa za makundi ndo zimeiua ccm tunasubiri mazishi 2015
 
Ukumbuke wengi wao ni vijana na vijana wengi kwa sasa wanahitaji changes na huo uwingi unaousemea cdhani kama ni kigezo cha yeye kushinda
 
Hii thread haina maana. Ni sawa na mtu akurupuke aulize ni kwa nini CUF haikushinda Tanga mjini wakati asilimia kubwa ya wakazi wa pale ni Waislam
 
Hatupigi Kura kwa mtu kwasababu ni Mkuu wetu au mwajiri wetu katika Kazi
 
Kumbe Media Group inawafanyakazi kibao Mwanza, nimebaini leo wakituma salamu za Krismasi.Ilikuwaje Mh. Diallo akapigwa mweleka na kijana mdogo wa kichaga Mh. Kiwia wa CHADEMA. Wafanyakazi wake hawakuwa mtaji wake?.
wapiga kura ILEMELA NI zaidi ya elfu sitini(60,000) na wafanyakazi waliokuwa wakituma salamu waliwatumia watu wangapi?? na kwanini watu eti kwa kuwa wametokea kuwa wafanyakazi wa media Group basi Bw.Diallo is entitled to their votes ?? uhalali huo umetokea wapi?? na uhalali huo wa ajabu kumpa kura Diallo pia upitishwe na kwa marafiki na ndugu zao pia ?? Hii ndio kazi
ambao nimekuwa nikiifanya usiku na mchana kuwaelimisha hasa wana CCM kuwa kwa sababu wewe ni mwanachama wa CCM
basi hiyo haimaanishi kuwa mwana ccm yeyote anayegombea basi he/she is entitled to your vote! she/he has to earn through
hard work of convincing why she/he is better than somebody else and she/he must have a record to show to prove it.
 
Back
Top Bottom