Mh. Cheyo huo ndio ushauri gani kwa rostam aziz na jk?

YanguHaki

Senior Member
Oct 11, 2010
129
9
Mzee Cheyo kumshauri Rostam Aziz aache siasa ni kukwepa kuzungumzia ukweli wa mambo na kuonesha jinsi gani hawa wazee wetu akiwemo Mrema walivyojichokea. Wameishiwa hoja kabisa! Rostam Aziz ni nani kwenye siasa za Bongo zaidi ya kuwa ni mwanachama wa CCM na mjumbe wa vikao vyake na pia ni mbunge wa Igunga? Hizi ni sifa ambazo wanachama wengi wa vyama mbalimbali wanazo. Kuacha siasa kwa Rostam hakutakuwa na maana yoyote kwa Watanzania labda kuipunguzia CCM mzigo wa lawama na kashfa. Watanzania wanataka Rostam achunguzwe na kupelekwa mahakamani kwa makosa mazito kama ya uhujumu uchumi n.k sio kufanyiwa usanii kama wa akina Mramba na wengineo.Wanataka achunguzwe kwani kila penye kashfa ya mabilioni jina lake halikosekani kutajwa lakini yupo anadunda mtaani bila hofu yoyote. Cha ajabu hakuna kiongozi yeyote nchini anayestuka kwenye suala hili zaidi kutafuta mchawi-nani amevujisha siri n.k. Kwa upande wa JK kumtosa pekee Rostam hakutamsaidia hata kidogo. Kwanza, itakuwa a little bit too late! Pili, atakuwa amefungua Pandora Box! Kwamba wengine wote wachafu nao watoswe nje ya chama kitu ambacho hataweza kukifanya mpaka anaondoka madarakani 2015. Kikubwa ninachotaka kusema ni kwamba hawa wazee sasa wanacheza ngoma wasioijua ila muda sio mrefu tutajua tune yake.
 
An empty stomach is not a good political adviser. Hawa wazee baada ya njaa kali kuwazidia na kushindwa kuendeleza vyama vyao, sasa wanajaribu kupapasa kila upande waweze kuzeeka na kitu! Unfortunately wana wafurahisha ccm pekee huku wenye akili washajua mchezo wanaojaribu kuucheza; kuudhofisha upinzani wenye nguvu uliomu-overtake
 
I see! Kuna watu wana makombora duniani!!!!!!
 
Back
Top Bottom