Mh Betty Machangu jitokeze kugombea uenyekiti wa UWT kwani una sifa na uwezo mkubwa

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Nakushauri Mh Betty Machangu chukua fomu ugombee nafasi hiyo kwani una sifa na uwezo mkubwa sana kuliko aliyekuwepo sasa.
Nakufahamu vizuri sana utendaji wako tangu ukiwa kama mkuu wa wilaya ya Nzega.
Wanachama wa UWT kama kweli mnataka maendeleo ya jumuiya yenu basi huyu mama ndio suluhisho kwenu. Kweli huyu Mh Betty Machangu ana uwezo mkubwa sana. Anajua kupanga mikakati ya maendeleo.
Tafadhali sana mama Machangu nakuomba ufanyie kazi hili ombi la wengi. Jumuiya inakuhitaji sana katika kipindi hiki. Tunakuomba uchukue fomu na tutakuunga mkono na utashinda kwa kishindo.
 
Kama hutojali Mh Betty Machangu karibu hapa jamvini angalau utupe hata salamu tu ili tujue kama ombi letu unalifanyia kazi.
 
usimdanganye mwenzio, si ana kashfa ya rushwa wakati wa kura za maoni viti maalum UWT huyu??
 
Tahadhari, najua kuna wale wapambe wa Sophia simba. Kama mtakuja na hoja zenu za kummaliza huyu mama mjue mtashindwa kwa kuwa mungu atamsimamia hadi anaibuka mshindi.
 
usimdanganye mwenzio, si ana kashfa ya rushwa wakati wa kura za maoni viti maalum UWT huyu??
Mkuu hakuwa na kashfa bali unajua huyu mama ni threat sana kwa bibi Simba. So aliundiwa hivyo visa ili kumchafua. Anyway kama una evidence weka hapa jamvini. Ila kwa kweli huyu Mh Machangu anahitajiaka sana kuongoza UWT kwa sasa. Kwanza una ujuzi sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya kifedha. Kwa kuwa jumuiya kwa sasa ina rasilimali nyingi lakini hazileti tija kwenye jumuiya hata kwa taifa pia.
 
Huyu mama ni mjanja na mnafiki sana. Takukuru walimshindwa. Kwanza PHD yake ina utata. Uliza IFM alikokuwa anafundisha. Haeleweki. Sio material ya uongozi, .
 
Mkuu si kweli kama Takukuru wamemshindwa bali hakuwa na hatia ila alizushiwa ili kumchafua. Na kuhusu hapo unapopaita wewe IFM mbona mambo yake yapo wazi kabisa. Kuhusu elimu yake haina utata kabisa ila tu kama una nia ya kumchafua basi sema hivyo.
Unajua sisi watanzania huwa tunapumbazwa sana na vitu vidogo sana. Jamani wanajumuiya ya UWT muungeni mkono huyu mama ataleta matunda. Pole mkuu kama umetumwa na shangazi. Kaa ukijua shangazi hana hadhi ya kuongoza hii jumuiya!
 
Atajisafisha mwenyewe mbona mnausemea moyo wake.
Hapana mkuu siusemei moyo wake bali ni kumuunga mkono tu ili aweze kushika huo wadhifa. Anyway tunamuomba na yeye ajitokeze hapa kwenye jamvi tuongee nae. Mh Betty Machangu twakuomba jamvini.
 
Mambo yapi makubwa amefanya Nzega ,just curious
Mkuu huyu mama amefanya mambo mengi tu mazuri katika wilaya ya nzega akiwa mkuu wa wilaya kabla hajahamishiwa kasulu. Na kama ilivyo kawaida yake alipofika kasulu ameacha mazuri mengi sana aliowafanyia wana wa kasulu hata wao ni mashahidi kwa hili. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
 
mambo makubwa mambo GANI ??
Kuhusu swala la rushwa mama huyu alikamatwa hotelini akigawa rushwa na jela alilala takukuru wasingeweza kumweka
jela kama walikuwa hawana ushahidi. kuhusu kuachiwa na takukuru unajua kuwa takukuru ni taasisi ya serikali na inaendeshwa na inatumiwa kwahiyo ni swala la kupigiwa simu tu na kesi inafutwa.kufutiwa kesi na takukuru hakumaanishi you are not guility.
 
Nakushauri Mh Betty Machangu chukua fomu ugombee nafasi hiyo kwani una sifa na uwezo mkubwa sana kuliko aliyekuwepo sasa.
Nakufahamu vizuri sana utendaji wako tangu ukiwa kama mkuu wa wilaya ya Nzega.
Wanachama wa UWT kama kweli mnataka maendeleo ya jumuiya yenu basi huyu mama ndio suluhisho kwenu. Kweli huyu Mh Betty Machangu ana uwezo mkubwa sana. Anajua kupanga mikakati ya maendeleo.
Tafadhali sana mama Machangu nakuomba ufanyie kazi hili ombi la wengi. Jumuiya inakuhitaji sana katika kipindi hiki. Tunakuomba uchukue fomu na tutakuunga mkono na utashinda kwa kishindo.

Ungekuwa umemtendea sana haki Mama Machangu kama ungeweka wazi utendaji wake walau kwa Nzega tu. Anzia na alipoikuta Nzega, akafanya nini na kuiacha vipi kiasi kwamba tumuone anastahili kugombea nafasi ya ubunge wa bila kupingwa wa viti maalum vya CCM kwa kigezo cha kuwa Mwenyekiti wa UW-CCM. Otherwise itakuwa ni sawa na kupiga rangi upepo.
 
Mkuu si kweli kama Takukuru wamemshindwa bali hakuwa na hatia ila alizushiwa ili kumchafua. Na kuhusu hapo unapopaita wewe IFM mbona mambo yake yapo wazi kabisa. Kuhusu elimu yake haina utata kabisa ila tu kama una nia ya kumchafua basi sema hivyo.
Unajua sisi watanzania huwa tunapumbazwa sana na vitu vidogo sana. Jamani wanajumuiya ya UWT muungeni mkono huyu mama ataleta matunda. Pole mkuu kama umetumwa na shangazi. Kaa ukijua shangazi hana hadhi ya kuongoza hii jumuiya!
kufutiwa kesi sio ushahidi kuwa hakufanya kosa hilo kwani kama kufutiwa kesi walifutiwa wote mpaka waliokuwa wanagawa rushwa mkutanoni wakina Mwakalebela na sitta aliyekatwa saa nane usiku na bahasha za fedha. takukuru siyo taasisi huru kama tulivyojionea ktk issue za Rrichmond na EPA nafirkiri hauitaji ushahidi zaidi ya huo
 
kwa kuwa UWT walionyesha dalili ya kumwua mwl,
na mwisho ben akafanikiwa, nasema hivi 'sina imani tena
na U.W.T.' na kama inawezekana ifutiliwe mbali.
 
UWT ni ile ya Lucy Lameck, Thabita Siwale, Sofia Kawawa. Kwa sasa UWT inamharibia mwanamke sifa, hasa kama wewe ni kiongozi (hata kama ni kiongozi UWT -kata). UWT= fedheha. sorry!
 
kwa kuwa UWT walionyesha dalili ya kumwua mwl,
na mwisho ben akafanikiwa, nasema hivi 'sina imani tena
na U.W.T.' na kama inawezekana ifutiliwe mbali.
Mkuu umenikumbusha mbali sana, hivi ndo enzi zile bibi titi alishtukiwa? Duh namlilia sana mwalimu kama angelikuwepo leo basi tungemtumia kwa wakati huu mgimu kwetu!
 
we ndo meneja kampen wake...una uhakika gani kwamba yeye anataka hiyo nafasi.?
 
Mbali na kashifa ya rushwa mmesahau alipokuwa Nzega alijimilikisha katapila akawa anawakodisha wafanyabiashara ni kati ya wanawake wachafu waliojiingiza kwenye siasa nitawaletea habari yake alipomwacha kwenye mataa mzungu wa watu airport ngoja nikusanye data
 
Back
Top Bottom