Mh. Beatrice Shelukindo aeleza ukweli kuhusu posho

Kuna dalili za kiushabiki na kuteteana kwenye Bunge letu Mh Shekilindo anaongea tofauti na wengine ,katibu wa bunge naye anaongea luwake ,spika anongea vingine pia unashindwa kuelewa nani yuko sahihi ,Shelukindo anadai posho rais kazikataa ,spika anakubali zimepitishwa,katibu anaeleza wanasubiri mchakato wa kusaini kutoka kwa Rais huku posho hizo zimesha ingizwa kwenye account za wabunge tumwamini nani kama si, wametugeukia na kigeugeu cha nini na hawa wabunge wanajua kabisa utekelezaji wa budget za serikali unakwama kwa ajili ya ukosefu wa hela au upungufu wa hela mpaka msubiri wafadhili waweze kubust budget sasa hizi za kujiongezea kimyakimya zinatoka wapi ,na hasa ni kwa ajili ya luxury si dhani Mh yuko kwa ajili ya wananchi ambao wanaishi china ya $ 1 usd kwa siku, akigubikwa na huduma mbovu za Afya,elimu,usafiri,maji,chakula na malazi je mmeshasahau watu waliowachagua wako kwenye hali gani?na hasa anakotoka Mh SHELUKINDO hawa ndio maskini wa kutupwa huko alikotoka,Spika ndio usiseme na asingepaswa kusahau mapema kiasi hicho.
 
Kazi tunayo awamu hii

yote haya CHADEMA ndiyo walio sababisha tuwe tunazijua siri hizi awali walikuwa wanapeana posho kama wanavyopenda na hatukujua wala hatukuhoji...
 
Zitakuwa zimeongezwa na wamelipwa; Katibu wa bunge anatafuta jina au justification nyinginr ndio maana akasema ni malimbikizo ya madai yao.
 
Akihojiwa na Othman Miraji wa Deutsche Welle Mh. Shelukindo amekiri kuwa ni kweli mpango wa kuongezwa posho ya Tsh.200,000/=ulifanyika kutokana na ugumu wa maisha ya mjini Dodoma. Akiri rais kukataa kusaini ombi la posho hizo. Na kusisitiza kuwa si kweli kwamba wameanza kulipwa. Amesema tume ya kuangalia upya posho hizo itakutana jumamosi. Haya wadau nafikiri kweli posho hizo bado hazijaanza kutolewa kutokana na kauli za watu zaidi ya wawili kukataa kuwa posho bado. Mwasemaje wanaJf?

Speaker naye kama mkuu wa nchi hajui kinachotokea ni mvivu wa kufikiri!!!
 
bi kiroboto kaisha sema sasa huyu mjukuu wake anatuambia nini?hana jipya kaishakula asianze kujikweza anawezaje kupinga kitu alichodhibitisha bi kiroboto?kwani mjukuu na bibi nani wa kuaminiwa?
 
Speaker naye kama mkuu wa nchi hajui kinachotokea ni mvivu wa kufikiri!!!

Wewe Osokoni ina maana yeye hakusign po pote ndiyo maana hakumbuki posho aliyopewa?

Mimi nina hakika hao wamepewa hiyo posho kwa kutarajia kwamba Raisi angesaini huo waraka, lakini sasa lilivyoripuka wanataka kuua soo wajenge hoja ya kujilipa posho kwa jina jengine.
 
hii ni nchi ya majuha, viongoz majuha, sasa kila mtu anasema lake na yule wanayemuita rais amekaa kimya hata hajui nini kinaendelea, inawapasa wajue siku kikinuka kama Misri wananchi watagawana vyote walivyochuma kifisadi
 
yule mama jinsi alivyobanwa na mtangazaji nilitamani hata kipindi kisiishe ili aendelee kumubana, yule mwanahabari katuonesha kuwa yeye ni mwanahabari kweli na sio hawa waliopo nchini ambao kazi yao ni kuambiwa na kuanddika kile walichoambiwa bila hata ya kuhoji kama nilivyoshuhudia leo na ndio maana tumeishia kuwalaumu kuwa waandishi wengi wa habari wanahongwa na kuandika wanachoambiwa wakiandike tena pasipo kuhoji kile wanachokiandika. Amauti
 
hii ni nchi ya majuha, viongoz majuha, sasa kila mtu anasema lake na yule wanayemuita rais amekaa kimya hata hajui nini kinaendelea, inawapasa wajue siku kikinuka kama Misri wananchi watagawana vyote walivyochuma kifisadi

Halafu cha kushangaza wote walikula viapo!Tena waliapa huku wameshika vitabu vitakatifu!Haya majitu yalitakiwa yawe yanaapa huku yameshika misaburi yao badala ya kushika vitabu vya dini.
 
Mbona hata pale Kisutu huwa wanaapa wameshika hivyo vitabu lakini baada ya hapo longolongo ka kawaida tu? Sasa itaku mjengoni ambako magamba yamekwamia kiunoni? Hapo lazima wauaminishie umma kuwa yametoka hata kama kila mtu anaona hayajatoka.Hilo la posho ukija kumwuliza atasema vyombo vya habari vimepotosha
 
Sasa naanza kuwa na wasiwasi na usikivu wa masikio yangu kama si uelewa wangu, kwenye ile taarifa ya habari ya saa Mbili usiku ITV nilimwona na kumsikia huyu bibi Nanihii akitamka pamoja na mambo mengine kwamba hizi posho zilianza kulipwa kwenye mkutano ulioisha na kwamba Zitto Kabwe hakuweza kupewa kwasababu ya kanuni zinazotoa sifa ya kuzipata ni lazima Mbunge awe amesaini asubuhi na jioni wakati huo Zitto asingeweza kwani hakuwepo. Leo hii huyu Shelukundu anatwambia tofauti. Je tumwamini nani!

Mie nilishawahi kusema kwamba huyu mwanamke anapokuwa kwenye 'days' zake mara zote huwa anaenda chaka bila kujijua. Mkuu wake-Bi Kiroboto alishafunga mjadala kwamba malipo yalishafanyika tangia kikao kilichopita, sasa yeye sijui katumwa na nani kum 'contradict' Bi Kiroboto!
 
yule mama jinsi alivyobanwa na mtangazaji nilitamani hata kipindi kisiishe ili aendelee kumubana, yule mwanahabari katuonesha kuwa yeye ni mwanahabari kweli na sio hawa waliopo nchini ambao kazi yao ni kuambiwa na kuanddika kile walichoambiwa bila hata ya kuhoji kama nilivyoshuhudia leo na ndio maana tumeishia kuwalaumu kuwa waandishi wengi wa habari wanahongwa na kuandika wanachoambiwa wakiandike tena pasipo kuhoji kile wanachokiandika. Amauti


Mie mwenyewe niliyafurahia sana mahojiano yale mkuu, nilitamani niyarekodi.....!
 
Mkuu heshima kwako,

Uoga ndiyo uliotufikisha mahali tulipo. hivyo siogopi. hata wakini piga Ban nitaendelea kumwita BI KIROBOTO

kuna watu ni waoga nchi hii! Ndo maana mi nasema bora kuchafuke masikio yetu yazoee kelele za risasi na mabomu ndo tutaendelea
 
nashauri badala ya kuwapa posho wabunge ni bora zikajengwa hostel za bunge halafu wakawekewa mpishi.
kwa upande mwingine inabidi tuanze kukagua matumizi ya posho hizo kama zinatumika kulingana na makusudio yake.
Watakaguliwaje wakati kama ni risiti wanaweza wakanunua tu?

Dawa ni wananchi kukataa hiyo posho isiongezwe, labda tu kama na wafanyakazi wengine wa serikali wataongezewa mishahara kwasababu maisha magumu hayapo Dodoma pekee.Yapo kila mahali.
 
Hivi Mbunge anapoona ugumu wa maisha na kutaka malipo ya ongezeke anadhani watanzania wenzake wanaishije?

Nasubiri ukombozi wa kweli uwadie!
 
nashauri badala ya kuwapa posho wabunge ni bora zikajengwa hostel za bunge halafu wakawekewa mpishi.
kwa upande mwingine inabidi tuanze kukagua matumizi ya posho hizo kama zinatumika kulingana na makusudio yake.


Mkuu hili wazo la kujengewa HOSTEL na kutafutiwa MPISHI nimelipenda sana. Kwa kweli hapo hata posho itabidi ifutwe kabisaaa!
 
Back
Top Bottom