Mh. Abood (MB), Meya wa Moro na Wasomi vyuo vikuu Moro mlifata nini Kata ya Kihonda?

Kanuni za uchumi zipo wazi, HAKUNA KUTOA BILA KUPATA, kwa hiyo sidhani kama akina Abood eti wanatoa kwa sababu ya kuwapenda watu. Kumbuka alivyokuwa amefulia akabaki na mabasi mawili tu machovu. Aliyemwokoa ni Mwinyi (kwa kumwamini na kufanya kampuni hii ya Abood kwa kuweka mtaji wake) wakazi wa Morogoro wanajua kama Abood anawafichia siri watu wakubwa serikalini. Scandinavia walishindwa kwa kuwa walikuwa wanakwepa ushuru sasa wamepotea wamejitokeza Green Star hatujui nani yu nyuma yao lakini nao ni walewale. Kwa uhakika usijitesa na kutafuta historia sijui ya Meya na watoto wa Abood bali jua tu kuwa Abood ni dalali wa wakubwa kwa upande wa mabasi na ili awatunzie siri ilibidi wamfanye mmoja wao.
Weka chama cha upinzani 2015 uone kitakachotokea kwa mabasi yale pamoja na vituo vya mafuta vya Camel na Lake Oil ndo utajua kuwa sisi si lolote ila upepo uvumao kuelekea tusikokujua.
 
kwa kweli kilichotokea siku ile ya mkutano wa mh mbunge na meya wa manispaa ya morogoro ni aibu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiita wana ccm,kwani mida ya saa kumi na mbili meya nondo aliwadanganya hao wanaojiita wasomi kuwa ndo anasaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya magorofani to mazimbu kwa kiwango cha lami,sasa hao wanaccm wa hivyo vyuo hawajiulizi ni mkataba gani wa serikali unasainiwa kwenye mkutano wa ccm?tena saa kumi na mbili?wao wakaishia kupiga makofi na baadae kama kawaida ya ccm wakawapa chakula ambacho hata hivyo walianza kukigombania ka mateja.Hii ni aibu kubwa kwa wasomi wetu wanaosukumwa na matumbo na posho ya shs 2500
 
Back
Top Bottom