Mgonjwa wa Kwanza wa Mafua ya Nguruwe Atengenezewa Sanamu la Ukumbusho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
2635578.jpg


Mtoto Edgar Hernandez kushoto na sanamu alilotengenezewa kulia

Mtoto wa miaka mitano wa nchini Mexico ambaye ugonjwa wa mafua ya nguruwe ambao hadi sasa umeua zaidi ya watu 1,000 duniani uligunduliwa kwake, amejengewa sanamu la ukumbusho nchini humo. Edgar Hernandez alikuwa mgonjwa wa kwanza duniani kugundulika na ugonjwa wa mafua ya nguruwe hata hivyo mtoto huyo alifanikiwa kupona ugonjwa huo ambao umesambaa duniani hivi sasa.

Ugonjwa wa mafua ya nguruwe uligunduliwa nchini Mexico kwenye kijiji cha La Gloria na hadi sasa umeishaua jumla ya watu 1,000 katika nchi 34 huku ukiendelea kusambaa kwa kasi na kuendelea kutishia maisha ya watu wengi sana duniani.

Msanii Bernardo Luis Artasanchez ndiye aliyelitengeneza sanamu hilo kwaajili ya ukumbusho wa Edger ambaye alibatizwa jina la "Boy Zero" kwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa mafua ya nguruwe kuugua na kupona.

Wakazi wa kijiji cha La Gloria ambacho Edger anaishi walisema kuwa kuwekwa kwa sanamu hilo kijijini hapo kutasaidia kuvuta watalii wengi baada ya mashirika mengi ya habari kutoka sehemu mbali mbali duniani kumiminika kijijini hapo wakati ugonjwa wa mafua ya nguruwe ulipogunduliwa kwenye kijiji hicho mwezi machi mwaka huu.

Mtengenezaji wa sanamu hilo Bernardo Luis Artasanchez alisema kuwa atakuwa ni mtu mwenye furaha kuliko wote duniani iwapo watu watakuwa wakimiminika kwenye kijiji hicho kwaajili ya kulitembelea sanamu hilo.

Mtoto Edger yeye anachowaza hivi sasa ni kucheza na watoto wenzake tu baada ya kutumia muda mwingi akiwa kitandani akipatiwa matibabu ya ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom