Mgonjwa ajinyonga Muhimbili

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SUSAN Chiganga (51) aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Da es Salaam, amejinyonga kwa kutumia kanga akiwa ndani ya bafu la wodi aliyolazwa.

Inaelezwa kuwa mwili wa mgonjwa huyo ambaye alitokea wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, na kulazwa katika wodi namba 20 iliyo katika jengo la Sewahaji ulikutwa juzi ukining’inia katika bomba la maji ya mvua.

Akizungumza na Tanzania Daima Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, alisema siku ya tukio mgonjwa huyo aliamka majira ya saa 5 usiku na kwenda kujisaidia ambapo alichukua muda mrefu pasipo kutoka.

Alisema kutokana na hali hiyo muuguzi wa zamu alimfuata na alipogusa mlango alikuta ukiwa umefungwa na kuamini kuwa mgonjwa huyo alikuwa akioga kwani wakati akiwa nje alisikia maji yakitiririka.

“Baada ya kufikiri hivyo muuguzi huyo aliamua kurejea wodini kuendelea na kazi lakini ilipopita nusu saa bila Susan kurudi ndipo alipoamua kumfuatilia tena na aliposukuma mlango na kuchungulia alikuta mwili wake ukining’inia katika bomba la maji ya mvua,” alisema Aligaesha.

Baada ya tukio hilo mhudumu huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali hiyo ambapo walilazimika kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Oysterbay ndipo askari polisi walipokwenda ili kufanya taratibu zao za kikazi.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alikiri kupokea taarifa hizo na kueleza kuwa mgonjwa huyo alilazwa hospitalini hapo Aprili 24 akitokea katika Taasisi ya Saratani (Ocean Road) akisumbuliwa na uvimbe jichoni.

Alisema kabla ya kifo chake marehemu hakuacha ujumbe wowote lakini wanaendelea na uchunguzi zaidi.
 
why report to oysterbay police,kwani kile kituo cha muhimbili hakipo tena?pole yake.
 
Back
Top Bottom