Mgomo wa wauza mafuta umeanza tena

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Kuna kila dalili kuwa wauza mafuta wamegoma tena kufuatia kushuka kwa bei ya Petrol na Diesel kwa mujibu wa bei elekezi iliyotolewa na EWURA kwa mwezi wa Octoba ambapo Petrol imeshuka hadi sh. 1991 kutoka 2300 ya mwezi uliopita.
Vituo vingi vya kuuza nishati hiyo vimekuwa haviuzi petrol toka mida ya saa nne asubuhi.
 
Hata mm nisingeuza hayo mafuta,kwani mtu mwenye stock yake ya lita 100,000 ameinunua mwezi uliopita kwa bei flani leo aiuze tu kwa bei yoyote kisa Serikali na bei elekezi. Hivi serikali hii inajua ni mafuta kiasi gani yameingia nchini, na kwa siku yanatumika kiasi gani, ili mwisho wa mwezi wawe na rejeo la kushuka au kupanda kwa bei?
 
Lakini watumiaji pia pengine wanayo haki ya kujiuliza; mbona bei elekezi zikipandishwa wauzaji pia wanapandisha bila kujali kuwa stock waliyokuwa nayo waliinunua kwa bei ya chini?
 
Ningekuwa na uwezo ningempiga huyu jamaa risasi...
 
hawa wafanya biashara ni waguni, hakuna asiejua utaratibu wa ewura kutangaza bei mpya kila mwezi,
hakuna asiejua makadirio ya mauzo ktk kituo chake kwa mwezi,
kwa mfanya biashara makini atakuwa anafutilia bei ktk soko la dunia ambacho ndio kigezo kikubwa kinachotumiwa na ewura.
Mi naamini wanafanya usanii wa makusudi kwa manufaa yao.
 
ridhiwani anamiliki lake oil filling stations,..mafuta yatapanda tu
 
Mimi naona kuna kila dalili ya mgomo kwa sababu serikali yenyewe ni kama haieleweki.

Kaka tuongee tu ukweli,
Unafahamu hii inayoitwa "bei elekezi" inatokea wapi? Wana-refer bei ya nje ya nchi ya wiki hii wakati mafuta yamenunuliwa miezi mpaka mitatu iliyopita!!!

Hii formula yao ni fake Rulerman. Wangetumia system ya "weighted average".

TBS, TPA, EWURA, SUMATRA, TRA, WMA wote hawa data za ujazo wa mafuta yaliyokuwepo kabla + yaliyoingia = yaliyopo sasa. Weighted average haitasumbua ku-calculate bei.

Ewura wanaweka ukokotozi wa bei zao ambao haulingani kati ya kampuni moja na ingine.

Juzi serikali imeshinda kesi against hawa waagizaji, but I am telling you it was kesi ya ngedere hakimu nyani. Na hawa waagizaji wakaamrishwa kulipa 100mil ya mawakili wa serikali.

Ubabe ni mwingi mkuu, waagizaji nao wana madai yao ya msingi mkuu!!
 
Lakini watumiaji pia pengine wanayo haki ya kujiuliza; mbona bei elekezi zikipandishwa wauzaji pia wanapandisha bila kujali kuwa stock waliyokuwa nayo waliinunua kwa bei ya chini?
Mkuu, serikali so called EWURA ndio wangekua na hichi kibarua mtumiaji wa lita 5 kama mimi naanzia wapi hii kazi yakujiuliza stock na bei. Ndio maana nikasema old stock - current = tu mafuta mapya na bei mpya.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kaka tuongee tu ukweli,
Unafahamu hii inayoitwa "bei elekezi" inatokea wapi? Wana-refer bei ya nje ya nchi ya wiki hii wakati mafuta yamenunuliwa miezi mpaka mitatu iliyopita!!!

Hii formula yao ni fake Rulerman. Wangetumia system ya "weighted average".

TBS, TPA, EWURA, SUMATRA, TRA, WMA wote hawa data za ujazo wa mafuta yaliyokuwepo kabla + yaliyoingia = yaliyopo sasa. Weighted average haitasumbua ku-calculate bei.

Ewura wanaweka ukokotozi wa bei zao ambao haulingani kati ya kampuni moja na ingine.

Juzi serikali imeshinda kesi against hawa waagizaji, but I am telling you it was kesi ya ngedere hakimu nyani. Na hawa waagizaji wakaamrishwa kulipa 100mil ya mawakili wa serikali.

Ubabe ni mwingi mkuu, waagizaji nao wana madai yao ya msingi mkuu!!

Mkuu, siku hizi (Toka December 2011) mafuta yote yanaagizwa kwa pamoja na makampuni yenyewe, hivyo bei haitatofautiana kwenye source supplier. Biashara ya mafuta imejaa ubabaishaji na wizi, ndiyo maana hawataki kufuatiliwa. Hizo old stock unazoziongelewa huwa hazipo wakati bei wanapandisha? Mbona huwa hawabishi? Na ushahidi kuwa biashara inalipa, ni kila mara vituo vipya vinaongezeka...havifungwi, mbona hatujiulizi?
 
Mkuu, serikali so called EWURA ndio wangekua na hichi kibarua mtumiaji wa lita 5 kama mimi naanzia wapi hii kazi yakujiuliza stock na bei. Ndio maana nikasema old stock - current = tu mafuta mapya na bei mpya.
Mkuu, hapo juu umeonesha kama vile unawaonea huruma wauzaji wa mafuta kuwa watapata hasara kwa sababu stock waliyonayo waliinunua kwa bei kubwa! Ndio maana nauliza hao wauzaji huwa wanafanya nini bei elekezi zikipanda? - Wanasubiri wamalize stock ya zamani? Serikali na EWURA, binafsi nawalaumu kwa uzembe na kuwa legelege katika kusimamia sheria na maslahi ya 'walaji'!
 
Hapo kwenye blue ndio pakufanyia kazi, kwani hawa jamaa wauza mafuta ndipo wanafungia magoli yao, angalizo tu mafuta hayaozi kwahiyo wauzaji watakua wanasema hawana mafuta hata kama kisima kimejaa.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
kuna kila dalili kuwa wauza mafuta wamegoma tena kufuatia kushuka kwa bei ya petrol na diesel kwa mujibu wa bei elekezi iliyotolewa na ewura kwa mwezi wa octoba ambapo petrol imeshuka hadi sh. 1991 kutoka 2300 ya mwezi uliopita.
Vituo vingi vya kuuza nishati hiyo vimekuwa haviuzi petrol toka mida ya saa nne asubuhi.
na vasco dagama yuko marekani anakula bata!
 
Ila vizuri yapungue jamani

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Thats why Azimio la Arusha liliharamisha viongozi wa umma kufanya biashara,sasa tumechagua soko holela na kuruhusu kiongozi kama rais,waziri na familia zao kumiliki njia kuu za uchumi wa nchi,what do you expect?
 
Back
Top Bottom