MGOMO WA WALIMU WAPAMBA MOTO: Habari na matukio katika picha

........upepo tu;

serikali inatakiwa iliangalie swala hili kwa jicho la pembeni na huu ni mwanzo wa kuelekea kuwa na taifa la watu wasiokuwa na ulewa wa kuchanganua mambo. mwalimu ni mtu muhimu sana lakini nashangaa kwa nini Tanzania inawasahau sana na kutowathamini. kama tunaweza kulinganisha na nchi nyingine wanavyowalipa wabunge kwa nin isifanyike hivyo kwa walimu pia. "WE ARE PLANTING SEEDS OF OUR OWN DISTRUCTION"
 
Mpaka Hapo Viongozi wa serikali watakapokatazwa kupeleka watoto wao shule binafsi, hali hii itaendelea tu. Hapo watoto waliokosa kufundishwa hakuna mtoto wa Rais, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa mikoa na Wilaya na hata makatibu tarafa. Watoto wao wanaendelea na masomo shule binafsi. Nani atawatetea hawa watoto wa shule za serikali?

Ukiwakataza watapelekwa Uingereza kwa Scholarshipi za serikali na nyingine zinazokuja kutoka kwa nchi rafiki. Wengine tunao vyuoni wanatafuta PASS baada ya hapo katibu tawala Wilaya mpya, Mkuu wa mkoa mpya ulioanzishwa, mkuu wa wilaya mpya iliyoanzishwa. In short ni ukilitimba tu huu...........
 
1. Mgomo huu wa walimu na maandamano ya wanafunzi, sio kero kwa viongozi wetu kwakua hamna kiongozi hata mmoja mwanae anayesoma Saint. Halmashauri.......!

2. MwnaHalisi imefungiwa....ukiangalia kisa.....utaona kuna tatizo la kufikiri ndani ya serikali.....! Gazeti limesema; aliyemteka Ulimboka ni RAma wa Tiss,......halijasema ni Tiss....! Kwa hali hii kweli wataweza kutumia akili kutatua migogoro, maandamano n.k?

3. Mbunge anayepokea zaidi ya 300,000/- kwa siku ukilinganisha na mwalimu anayepokea mshahara huo kwa mwezi, halafu bado bunge linaona fedha hiyo ni ndogo kwa wabunge na wanampango wa kuongeza.....sasa uiano upo vipi kwa kada zingine kama walimu?

4. Zamani, walimu ulikuwa ni wito kwakuwa watoto wa viongozi wote nao walikuwa wakisoma st. Halmashauri, sasa hivi Ualimu siyo wito tena, baada ya hizi akademia kuota kama uyoga, huku wamiliki wao wengine wakiibia serikali umeme na kusamahewa kodi kupitia mradi wao wa makanisa......!

5. Nchi lazima iwe ngumu kutawalika kwakua, wapishi ambao ni viongozi, wanavimbiwa kwa kujipakulia wenyewe nyama, na wenye nchi ambao ni wengi wanaambiwa wagawane supu na mifupa, kibaya zaidi hata hiyo mifupa haipatikani kwa wakati....!
 
Hivi posho ya wabunge kwa mwaka bajeti yake ni kiasi gani? ikiondolewa na mshahara wao kulimwa kidogo na matumizi ya magari ya kifahari (millioni 200 gari moja) yakaondolewa na kutumia magari ya millioni 40 hivi kila moja,pamoja na kufilisi wale wote walioliingizia taifa hasara kubwa za mabilioni ya fedha. na fungu litakalopatikana likapelekwa kwenye sekta muhimu kama za Afya,Elimu haitasaidia? kama itasaidia kikwazo nini? Oohh nimesahau mabilioni ya fedha yanayoyeyuka kwa mikataba mibovu ya madini, na wale Twiga kule Dubai....argggghhhh!!
 
mkuu sasa itv na madai ya walimu wao imekuiwaje tena.....sipati connection hapo ebu nisaidie au wanataka wauze sura maana hawa watotowetu wa kiduku, face book, na .com hawa ni hatari sana

wanataka kupewa airtime watoe malalamiko yao
 
Serikali imetoa tamko ya kwamba wapo walimu wanawashinikiza watoto kuandamana na wanadai wamewaandalia mabango na kuwaandikia maneno ya kuhitaji haki yao ya kupata elimu. Lakini mie kama mie nataka kusema. Watoto ambao wenye ukaribu mkubwa na walimu wao ni wa Msingi ndo wanajua umuhimu wa mwalimu. Yani katika kumfungua mtoto ufahamu wake na kumleta ajue mambo mengi mpaka mtoto anatambua kuna mgomo jua hawa sio watoto ila nao wanatambua haki zao za msingi ni kupata elimu na kuitumia elimu yao katika kuifanya serikali ijue kwamba nao wanaufahamu mambo mbali mbali nchi inapitia, ufisadi wanatambua. Ukiwauliza fisadi kubwa bungeni matoto yanajibu. Ukiwauliza serikali ambayo ipo madarakani imeingia kwa haki wanajibu "imechakachua kura". Alafu leo serikali inawatumu walimu kuwafanya wanafunzi waandamane. Hivi kuwe kuna mbadilishano wakazi. Wabunge na mawaziri wachukue nyadhifa za uwalimu kwa muda wa mwez mmoja na walimu wachukue nyadhifa zao tuone. Je wataweza?
 
Hivi posho ya wabunge kwa mwaka bajeti yake ni kiasi gani? ikiondolewa na mshahara wao kulimwa kidogo na matumizi ya magari ya kifahari (millioni 200 gari moja) yakaondolewa na kutumia magari ya millioni 40 hivi kila moja,pamoja na kufilisi wale wote walioliingizia taifa hasara kubwa za mabilioni ya fedha. na fungu litakalopatikana likapelekwa kwenye sekta muhimu kama za Afya,Elimu haitasaidia? kama itasaidia kikwazo nini? Oohh nimesahau mabilioni ya fedha yanayoyeyuka kwa mikataba mibovu ya madini, na wale Twiga kule Dubai....argggghhhh!!

Bila kusahau mikoa na wilaya mpya kila kukicha ili mradi mtoto wa aliesimamia ubatizo na zrobaini ya watoto zao wapate ajira za kutetemekewa. Tanzania ni kama kahaba, haina muelekeo kabisa.
 
Mie nadhani itakuwa takribani millioni 200-300 kwa mwaka. Kwasababu kwa mshahara wamewapandishia mwaka huu kwahyo wadau wamesema itakuwa m10 kwa mwezi na makorombwezo yote inazidi. Watu wanakula hela babu. Huyo mbunge mmoja je wabunge wote itakuwaje. Alafu m2 akidai nyongeza ya hata sh. 20000/= tu mpaka agome na atimuliwe kazi. Wakati mwingine agomi akisema nataka mshahara uongezwe unaongezwa. Serikali haiko stable we must destroy this.
 
Jamani elimu inachezewa kiasi hiki! kweli Baba wa Taifa angefufuka leo angekufa hapohapo kuliko kuona zahama hili. Kikwete na wasaidizi wako mko wapi na mnafanya nini mpaka wajukuu wanawadai haki yao ya kusoma? Mmetengeneza a lost generation a midst influence mnafikiri Mungu anasemaje kuhusu uzembe huu???? Aibu kweli kweli Mungu tusaidie.
 
Bila kusahau mikoa na wilaya mpya kila kukicha ili mradi mtoto wa aliesimamia ubatizo na zrobaini ya watoto zao wapate ajira za kutetemekewa. Tanzania ni kama kahaba, haina muelekeo kabisa.

Kweli kabisa serikali yetu inatumia gharama nyingi sana kujiendesha kuliko kuwatumikia wananchi wake..Hata wabunge wa viti maalum binafsi sioni umuhimu wao, ni kupeana ulaji tu
 
Sikuwahi kufikiria kuwa hata siku moja nitakuja kujiunga na JF lakini mambo mengi yamenigusa mpaa ikanivutia nifanye hivyo hasa kwa jinsi serikali yetu inavyotuburuza as if walioenda shule ni wao tu walioko madarakani inasikitisha, migomo kila kukicha sasa naomba kuuliza katika huu mgomo wa walimu watamliulimboka naniiiiiiiii? maana kwao kila ateteaye haki za wananchi kwao ni adui ambaye anastahili kunyongwa mpaka kufa, linaisha hili linaibuka hili wameanza madaktari, mara waalim, MWISHO WAKAAMUA HATA HAKI ZAO HAKUNA KUPATA (NSSF) maana hili linamgusa kila mtu uwe doctor,mwalimu nk. duh nafwaaaaaaaaaaaaa
 
Hili KUNJI la walimu muziki wake si mchezo, naona madaktari wangejifunzia hapa warudi kambini waanze upya.
 
Kweli kabisa serikali yetu inatumia gharama nyingi sana kujiendesha kuliko kuwatumikia wananchi wake..Hata wabunge wa viti maalum binafsi sioni umuhimu wao, ni kupeana ulaji tu

Hapo kwenye wabunge viti maalum, VICK KAMATA ana historia nzuri na Jua Kali(Jk) ... Napata kigugumiz juu ya hili na sielewi kabisa.
 
Mahenge hali ni mbaya, shule zote zamsingi za mjini walimu wamegoma. mkuu wa wilaya amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri kutoa tangazo redio ulanga kupinga tangazo la katibu cwt (w) la kutaka mgomo uendelee na kusisitiza kwamba mgomo ni halali. Hivyo mkurugenzi ametangaza kupitia redio ulanga kwamba mgomo si halali kwa vile eti kura za kuunga mkono zilikuwa ni za siri.LAKINI TUNASEMA KWAMBA ALUTA KONTINUA!!!. MKUBWA HATISHIWI NYAU
 
hawa madogo nawaunga mkono ninatamani watanzania wote tuingie mitaani kuwaenzi hawa watoto wameosha wanaweza na wana jua haki zao
 
1. Mgomo huu wa walimu na maandamano ya wanafunzi, sio kero kwa viongozi wetu kwakua hamna kiongozi hata mmoja mwanae anayesoma Saint. Halmashauri.......!

2. MwnaHalisi imefungiwa....ukiangalia kisa.....utaona kuna tatizo la kufikiri ndani ya serikali.....! Gazeti limesema; aliyemteka Ulimboka ni RAma wa Tiss,......halijasema ni Tiss....! Kwa hali hii kweli wataweza kutumia akili kutatua migogoro, maandamano n.k?

3. Mbunge anayepokea zaidi ya 300,000/- kwa siku ukilinganisha na mwalimu anayepokea mshahara huo kwa mwezi, halafu bado bunge linaona fedha hiyo ni ndogo kwa wabunge na wanampango wa kuongeza.....sasa uiano upo vipi kwa kada zingine kama walimu?

4. Zamani, walimu ulikuwa ni wito kwakuwa watoto wa viongozi wote nao walikuwa wakisoma st. Halmashauri, sasa hivi Ualimu siyo wito tena, baada ya hizi akademia kuota kama uyoga, huku wamiliki wao wengine wakiibia serikali umeme na kusamahewa kodi kupitia mradi wao wa makanisa......!

5. Nchi lazima iwe ngumu kutawalika kwakua, wapishi ambao ni viongozi, wanavimbiwa kwa kujipakulia wenyewe nyama, na wenye nchi ambao ni wengi wanaambiwa wagawane supu na mifupa, kibaya zaidi hata hiyo mifupa haipatikani kwa wakati....!
mkuu asante lakini hata kama watoto wao hawasomi kwenye shule hizi cha moto wanakiona wanaonekana kutembea bila nguo
 
Back
Top Bottom