Mgomo wa Walimu waiva; watoa notisi ya masaa 48

kweli akili yako inaelekea kuhamia matak*ni kutokana na kauli yako inaonekana hata ufaulu wako ni duni tena wa kuunga unga umesahau kuwa hata wewe hapo ulipo hao hao walimu anao wananga ndo walokufikisha hapo kima wewe unaongea utadhani umetoka kushikishwa ukuta tena nahisi ndipo uliko toka.kweli masikin akipata matak*o hulia mbwata.
.
Unataka kupigwa BAN eeeh!
 
Sioni sababu ya kugoma zaidi ya kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura na kuchagua chama makini.
 
Waalimu wengi hawana qualifications za kukidhi kiwango! Kama walivyo askari, wengi wao walichagu fani hiyo baada ya kukosa options zingine zaidi ya hizo kutokana na viwango vyao duni vya ufaulu. hivyo basi ni kwamba serikali inawapa fadhila tu kuwalipa hata laki 3 kwa mwezi, otherwise hawakustahili hata kumi.
We kwa akili zako zilivyo ipo siku utatukana hata wazazi wako waliokuzaa, walimu ndiyo msingi wa kwanza wa mtu yeyote mwenye maendeleo kielimu hata kimaisha unapotoa maneno yako yasiyo na adabu inaonyesha umesahau ulipotoka na ipo siku utakumbuka. kama walimu wasingekuwepo leo hii ungeweza kuandika huo upuuzi wako humu JF? tafakari kabla ya kutenda.
 
Sioni sababu ya kugoma zaidi ya kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura na kuchagua chama makini.
Kugoma ni inevitable.
ila kwa kuwa serikali ya JK watoto hata wasipofundishwa si ishu, ila inaweza kolezwa na maandamano.
 
TUSI hili....we kwenu huna ndugu mwalimu atiii?

Mimi naamini kada ya ualimu cku hizi ina vijana wasomi waliopass vizuri sana zamani kweli walimu walikuwa wale waliofelifeli ila sasa kuna vijana wasomi wenye weledi wa hali ya juu sana!!
 
I wish ungejua hata wasomi wa Tanzania nao ni kama hawa walimu. Kwa elimu yako wewe (Division 1) umeifikisha wapi Tanzania!! Sidhani kama hawa wa division 4 hawakukukfundisha wewe na kufikia hapo ulipo ukadhiriki hata kuwatukana. SHAME ON YOU.
my take!! huenda walimu safari hii wameamua???

Impossible for these people to strike! Mtu wa div 4 ya point 28 hawezi kugoma. These are the most uncoordinated people! These are the kind of people who can be hired and fired at will. Their labour power is tied!
Wana nguvu ya ajabu alkini hawawezi kuitumia maana hata viongozi wao, ni legelege! Just wait and see!

 
Hapa walimu wanachotafuta ni kuthibitisha Mgomo, lakini wameishaaza siku nyingi na matokeo ya mgomo huo tunauona kulingana na kipimo cha matokeo ya ufauru kwa watoto wetu, tunaomba kama serikali ni sikivu kama inavyojiita itatue tatizo ili tuweze kusonga mbele la sivyo nchi inaweza kushindwa kutawalika.
 
Walimu mlindeni Mwenyekiti wenu yasije mkuta ya Dr. Ulimboka hawa watu sio wazuri kwani hawawezi kurudia kosa walilolifanya kwa Dr. Uli. watampoteza kabisa.
 
Kama madaktari wameshindwa, waalimu mtafanya nini????? "LIWALO NA LIWE" ndiyo suluhisho, Mfupa mgumu ulio mshinda fisi, mbwa utaufanya nini?????? Angalia yasitokee tena yale yale ya dr. uli.
 
waalimu wengi hawana qualifications za kukidhi kiwango! Kama walivyo askari, wengi wao walichagu fani hiyo baada ya kukosa options zingine zaidi ya hizo kutokana na viwango vyao duni vya ufaulu. Hivyo basi ni kwamba serikali inawapa fadhila tu kuwalipa hata laki 3 kwa mwezi, otherwise hawakustahili hata kumi.
kama hiyo ndiyo hali halisi , hata hiyo nguvu ya kugoma sijui wanaipata wapi. nafikiri ndiyo maana serikali haijali kabisa.
 
Waalimu wengi hawana qualifications za kukidhi kiwango! Kama walivyo askari, wengi wao walichagu fani hiyo baada ya kukosa options zingine zaidi ya hizo kutokana na viwango vyao duni vya ufaulu. hivyo basi ni kwamba serikali inawapa fadhila tu kuwalipa hata laki 3 kwa mwezi, otherwise hawakustahili hata kumi.
Acha uhuni huo... Darasa nilihotimu mimi Form 6 Waliopata division 1 Point 4 na 5 walienda kusomea Ualimu wakati wenye division 3 za 14 walienda kusoma sheria. Inaelekea unafikiria kwa kutumia masaburi wewe
 
CHAMA cha Walimu nchini (CWT) kiko katika hatua za mwisho kutangaza rasmi kuanza kwa mgomo wa walimu nchini, unaotarajiwa kutangazwa rasmi wakati wowote baada ya saa 48 kuanzia asubuhi ya leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema mgomo huo sasa umeiva, baada ya mgogoro baina yao na Serikali uliodumu kwa siku 30 kumalizika bila kufikia suluhisho.

Msimamo huo wa CWT unatolewa wakati madai ya Madaktari yakiwa bado hayajapatiwa ufumbuziwa kudumu na kusababisha kuzorota kwa huduma za afya katika hospitali za umma
.
“Baada ya kushindwa kutatuliwa, zoezi la kupiga kura limeanza tangu jana (juzi) na litaendelea hadi kesho (leo) saa 3 asubuhi, baada ya muda huo kupita, Chama kitakuwa na kazi ya kupokea matokeo ya upigaji kura kutoka kila Wilaya,” alisema Mukoba na kuongeza:

“Ikiwa walimu watakaounga mkono mgomo watakuwa wengi kuliko wale watakaoupinga, Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza mgomo ambao utakuwa umeamuliwa na muda wa mgomo huo.

Rais huyo alifafanua kuwa baada ya uamuzi huo kufikiwa CWT itatoa notisi ya saa 48 kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Mkuu wa Utumishi wa Umma kumwarifu tarehe ya kuanza kwa mgomo ili alinde mali zake kama Sheria inavyoeleza.

Mukoba alisema, mgogoro na Serikali ulisajiliwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Juni 8 mwaka huu na kupewa namba CMA/DSM/ILA/369/12 na msuluhisi aliyeteuliwa na Tume hiyo Cosmas Msigwa kushindwa kuwasuluhisha.

“Siku 30 zilianza kuhesabiwa Juni 26 na kumalizika Julai 25 mwaka huu, kwa msuluhishi Msigwa kutoa Cheti cha kuthibitisha kuwa mgogoro umeshindikana kusuluhishwa kwa mjibu wa Sheria,” alisema Mukoba na kuongeza:

Ndani ya siku hizo 30 tumekutana kujadiliana kwa vikao vitatu lakini hakukuwa na dalili zozote za Serikali kuhakikisha inatatua matatizo yetu.

Rais huyo alisema, madai ya Serikali kushindwa kuyatatua ilisema ni kutokuwa na takwimu za walimu wangapi wanastahili kulipwa na huenda wengine wameshakufa.

“Hoja hii ilikuwa na nia ya kupotosha ukweli wa madai ya walimu kwa kuwa kikao cha Julai 10 mwaka huu, Serikali iliwasilisha taarifa kuwa ingetumia zaidi ya Sh4 trilioni kulipa mishahara ya walimu tu kama ikilipa mishahara kwa viwango vilivyowasilishwa na CWT iweje itake tena takwimu,” alihoji Mukoba.

Mukoba alisema Serikali ilikuwa haijui walimu wangapi wanafundisha masomo ya Sayansi na wangapi wanafundisha katika mazingira maguku kitendo ambacho walikipinga.

“Tulipinga hoja hizo kwa maelezo kwamba Serikali ndio yenye Shule za mchepuo wa Sayansi na inafahamu fika walimu wa Sayansi ni wangapi kwa kuwa takwimu hizo zilitolewa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu” alisema Mukoba na kuongeza:

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mlugo aliliambia Bunge kuwa Serikali imetumia Sh22 bilioni kuwalipa walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu Sh500,000 mara moja tu wanapokwenda kuanza kazi, na kama imetambua hilo iweje isifahamu maeneo yenye kuhitaji posho ya mazingira magumu?”.

Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekia Oluoch alitoa wito kwa wazazi na wanafunzi akiwataka kutowafikiria walimu vibaya wakati wakiwa katika mgomo huo na kitakachofanyika ni kudai maslahi yao.

“Tunawapenda sana wanafunzi, lakini watambue kiwango ambacho Serikali inatulipa ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yetu ndio maana tunaamua kugoma hivyo watuunge mkono,” alisema Oluoch.


my take!! huenda walimu safari hii wameamua???

Kama jana...kama leo...kama kesho, na hata milele....hakuna mgomo hapa
 
Wagome waone, tutapeleka Jeshi likafundishe. The last person nchi hii anaeweza kuwa na uthubutu wa kugoma ni mwalimu. Kwanza hata kabla mgomo wenyewe haujaanza wenyewe washaanza kujichanganya. Eti kama sensa intaangukia kipindi cha mgomo, basi wataahirisha mgomo hadi sensa ipite, kisa wanajua wao.

Waalimu wetu nawashindwa kuelewa tu kuwa hata bila waalimu wanafunzi wanaweza kusoma na wakafaulu japo wengi watafeli haswa wale wasiojituma. Ama pia ualimu sio kama udaktari, serikali kwa kipindi kifupi tu inaweza kuzalisha waalimu wa dharura, na jinsi waTz tusivyo na ushirikiano nafasi zikitangazwa tu wengi wataenda kulamba hizo ajira fasta.

so Baba Mukoba, think twice, tafuteni njia m badala ya kuifanya Serikali kutatua matatizo yenu. Mgomo will not work for you.
 
Back
Top Bottom