Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wanafunzi wa shule kadhaa za msingi huko Mbagala wameandamana leo kwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupinga walimu wao kutokuonekana darasani kufuatia mgomo wa walimu ambao ulikuwa umeanza jana.
Hata hivyo mahakama ya kazi jana usiku ilitoa amri ya walimu kusitisha mgomo huo kwani kuna kesi ya msingi. Rais wa CWT ametoa wito kwa walimu kurejea madarasani hadi kesi hii itakapoamriwa.
Wakati huo huo mikoa mbalimbali imeanza kupokea fedha za malipo ya malimbikizi ya madai ya walimu.
Huko Moshi, Chuo Shiriki Ushirika leo kimewasimamisha masomo wanafunzi wa mwaka wa pili na watu ambao waligoma leo kuunga mkono wenzao wa mwaka wa kwanza waliosimamishwa masomo jana!