soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Viongozi wa UDOM ninawaelewa na nawajua vizuri sana, nimewahi kufanya kazi nao UDSM. Ukweli kabisa, viongozi wa UDOM hawana udini wala ukabila. Suala la udini halipo UDOM, bali labda kuna watu wanapenda masilahi yao binafsi na ndoto zao za kutajirika kwa haraka, ambazo hazijawafikia kwa kiutaratibu ndio maana wanaimba udini ili viongozi wasafi watolewe na waje wa kuwafanya wepate mwanya wa kuiba.
Mimi niliwahi kufanya kazi na Prof. Mlacha UDSM, ni kiongozi mzuri sana. Prof. Kikula naye ndio kabisaa hana udini kabisa. Dr. Ame ndio anapenda watu bila ubaguzi wowote. Jamani hizi kuna sheria inayosema Wazanzibar hawatakiwi au hawaruhusiwi kufanya kazi UDOM au Tanzania Bara?.
Ni chuo gani cha Umma hapa Tanzania kinachowasafirisha wafanyakazi wake bure?. Au UDSM wafanyakazi wana safirishwa na Chuo?. Mbona mnasema daladala kwanini msizitumie nasikia zipo dala dala za UDOM nyingi tu. Kwani sera zinasemaje kuhusu kupewa Nyumba? Nchi inafuata utaratibu wa kutibiwa kwa bima, au ndio ninyi wa UDOM tu mnataka kutibiwa bure jamani?. Kama kweli Dept. ya fedha ni waisilimu watupu basi nawapongeza. Maana ndio hao hao ambao waliowafanyia mipango mizuri ya kuishi vizuri, kwani nasikia ni Chuo Kikubwa na kizuri sana. Kwa hiyo Bursar wenu na timu yake inafanya kazi vizuri hadi kufikia kuongeza idadi ya wanafunzi na walimu. Mafanikio bwana ni mipango mizuri ya hawa mabwana.
Jichunguzeni, Bunge lilianza Jana. Au wakuu wa Chadema waliwafikia na kuwapandikiza kitu na ndipo mmeanza?.
Eti walimu wanaacha kazi n... kwani waliopo hapo walipotoka si waliacha kazi kwingine na kuja UDOM. Huyo Nowe si aliacha Chuo sijui SUA na kuja UDOM?. Mbona hamuwasemi walioacha huko India, Urusi, Kenya, Uganda, Rwanda na wengine toka humu humu wamehamia UDOM siku chache tu zilizopita. Nasikia, walimu wanaojiunga na UDOM ni wengi sana, soma Prospectus zenu na machapisho mengine ujionee.
Mwacheni Prof. Mlacha na timu yake ambayo hadi sasa dunia nzima inashangaa Tanzania kuwa na maendeleo ya haraka na ya viwango. Angalia wanafunzi nasikia wengine wanatoka Msumbiji, Sweden... wanakimbilia UDOM. Acheni migomo fanyeni kazi, umoja wa waalimu ni kwa masuala ya ualimu na sio migomo isiyo ya kitaaluma.
Naungana nawe baadhi ya mambo ila ukweli haujui maana umekiri kuwa huwa unasikia. Wala CHADEMA hakihusiki kwa namna yeyote, tunataka mabadiliko.