Wasomi wenzangu, je hamjui namna ya kufuatilia matatizo yenu kwa njia sahihi? Kwani migomo ndio inayotatua?. Mbona ni suala dogo tu?. Kama mnashida fulani mfano ya kifedha inavyoonekana sehemu kubwa ya mada yenu ya mgomo, ni vema mkatuma wawakilishi kuanzia ngazi ya idara kama mnayo and then faculty na baadae ngazi ya chuo na ikishindikana sehemu husika mfano hazina kama mnavyosema na sio kwa Mh. Pinda au sijui kuilaumu CCM sijui na kulaumu mtu binafsi kama Misilamu au Mkristo fulani au Mzanzibar ???????.
Tuombe radhi ktk swali lako kuwa hatujui kutatua matatizo yetu. Jiulize katika haya;
i) Taasisi za umma zinaongozwa na scheme of service na sheria za utumishi wa umma zinazotolewa na wizara ama serikali moja tu ya Tanzania. Iweje mtu aajiriwe kama Assistant lecturer 2009 na hadi leo hajawahi kupata annual increment? Kibaya zaidi toka 2009 hadi leo ni kama miaka minne hadi leo lakini analingana mshahara na atakaeajiriwa leo 31/10/2012?
ii) Lugha zilizopo katika ofisi zinazoongozwa na hao watu hutaamini kama zinatolewa na mtu ambaye anatakiwa akuwezeshe shida yako imfikie mwajiri yaani serikali. Ulipaswa uwapongeze wahadhiri hawa kwa kuvumilia matusi/lugha chafu tena zenye dharau mno kana kwamba zinatolewa na mtu aliegharamia ujenzi wa chuo chote hiki. wakati nae ni mwajiriwa tu.
iii) Ungeweza kufanya utafiti kwanza ndipo ufikie kusema hatujui namna za kutatua matatizo yetu. Jiulize kama ni sawa pia kuwa mtu awe promoted toka Tutorial assistant hadi assistant lecturer akae miezi 13 (kumi na tatu) pasipokulipwa mshahara huo mpya. Anapokuja kulipwa anapunjwa na inapofika kujaza salary arrears claim form anajaza kwakulazimishwa ajaze mshahara wa mwaka wa fedha uliopita. Na hata hivyo madai haya ya matusi/kejeli/dharau uongozi unayafahamu vizuri sana, lakini ka nini usikemee kama hauya-support?
Ni vikao vingi sana vimefanyika kueleza matatizo ya wahadhiri hawa. Je wajua pia kuwa kuna mhadhiri ana miaka zaidi ya miwili hata promotion hajapata? halafu mwingine anaibuka kudai eti management ya UDOM imefanya mengi, si katai hata la klazimisha watu walipwe kisichostahili ya jasho lao na kusimamia hilo ni kazi kubwa si ndogo hata kidogo.