Mgomo wa wafanyakazi wa TAZARA

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Hawa sio wasafiri, ni wafanyakazi wa Tazara wakiwa kwenye mgomo kama walivyokutwa kwa mbali na kamera jana 24/8/2009.
attachment.php


Hebu tusome habari kutoka gazeti la Mwananchi la leo 25/8/2009

Wafanyakazi Tazara waanza mgomo

Waandishi Wetu

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) jana walianza mgomo wa kutokufanya kazi kwa kile walichodai kuwa wanatafakari kwanza hadi menejimenti itakapoyakubali madai yao na kuyafanyia kazi.

Hatua ya wafanyakazi hao kugoma imekuja baada ya makubaliano ya pamoja katika mkutano baina yao na uongozi Chama cha wafanyakazi wa reli (Trawu) taifa uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa abiria wa Tazara Mkoani Mbeya

Hata hivyo, taarifa zilizowahi kuchapishwa kwenye gazeti hili zilisema mamlaka hiyo kwa sasa ina hali mbaya kifedha kiasi cha kuhaha kusaka mikopo kutoka mabenki ya kimataifa.

Jana, wafanyakazi wa Tanzara, vituo vya Dar es Salaam na Mbeya walionekana wakizagaa bila kufanya kazi huku wakisisitiza kwamba walikuwa kwenye vikao vya tathimini.

Hivi karibuni viongozi wa Trawu walitoa taarifa ya matokeo ya kikao cha majadiliano kuhusu mkataba wa hali bora ya kati yao na mwajiri kilichofanyika Agosti 4, 2009 Mkoani Morogoro na kushindwa kufikia muafaka.

Taarifa ya matokeo ya kikao hicho cha majadiliano ilitolewa na katibu Mkuu wa Trawu, Sylivester Rwegasira ambaye alisema kuwa vipengele ambavyo mwajiri amevikataa katika majadiliano hayo ni pamoja na umri wa kisheria wa kustaafu wa miaka 60 kwa wafanyakazi wa upande wa Tanzania ambapo mwajiri anahitaji ule wa sheria ya nchini Zambia ya miaka 55.

Alivitaja vipengele vingine kuwa ni pamoja na wafanyakazi wa Tanzania kulipwa mishahara kwa thamani ya dola moja kwa Sh 1300 bila masharti,ongezeko la mishahara, muundo wa utumishi na muundo wa mishahara ambao madai yake yamekuwa ya muda mrefu

Rwegasira alivitaja vipengele vingine kuwa ni pamoja na pensheni ya Tazara ambapo mwajiri analazimisha wafanyakazi kujiunga badala ya kutoa uhuru kwa mfanyakazi na kipengele cha kuitaka menejimenti kuondoa utaifa katika shirika hilo kwa kuacha kuwabagua watanzania hasa katika nafasi za uongozi na malipo.

Naye Mwenyekiti wa Ttrawu Kanda ya Dar es Salaam Yusuf Mandai aliliambia gazeti hili jana kuwa, wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi wa shirika hilo kutosikiliza kilio chao cha muda mrefu Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Tazara, Damas Ndumbaro alisema kuwa kukusanyika kwa wafanyakazi hao na kujadili matatizo yao ni haki ya msingi na kuwa ofisi yake haijapata madai ya wafanyakazi hao na kuahidi kuyatatua pindi yatakapoletwa mezani.

Kuhusu safari ya treni inayotarajia kuondoka kesho asubuhi, Ndumbaro alisema kuwa safari hizo zitakuwepo kama kawaida kwakuwa anaamini kuwa wafanyakazi hao hawajagoma na endapo usumbufu utajitokeza basi uongozi utatoa tamko kwa wasafiri.

"Siwezi kuwazuia wafanyakazi kujadili matatizo yao kwakuwa ndio njia mojawapo ya kutatua tatizo sisi tunasubiri wayawasilishe ndipo tuweze kuyashughulikia, lakini kuhusu umri wa kustaafu suala lipo Mahakama ya Rufaa na sheria hairuhusu kulizungumzia hadi mahakama itakapoamua" alisema Ndumbaro.

Habari hii imeandaliwa na Brandy Nelson, Keneth Goliama, Mbeya na Subira Kaswaga

Source: Mwanachi
 

Attachments

  • Image001.jpg
    Image001.jpg
    28.3 KB · Views: 101
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom