Mgomo wa wafanyakazi una maana viongozi wakiacha kuhongwa!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Ndugu wapendwa napongeza kwa viongozi wa vyma vya wafanyakazi katika kudai maslahi yao,..kwa upande wangu napendwa kuwaweka wazi hata mwenyekiti wa hivyo vyama,..vyama hivi hivi vimekuwa vikiwageuka wafanyakazi ifikapo wakati wa menejiment kutaka kutimiza mahitaji yao tena kwa kuhongwa pesa ndogo sana bila kujali maslahi ya wanyakazi ama watoto wanaokuja kuajiria baada ya wao kuondoka!!!!.......kwa mantiki yangu mgomo huu utakuwa na maana kama viongozi hawa watakubali kuacha kuwasaliti wafanyakazi na si kupiga kelele wakati wa nyongeza za mishahara!!!!!
tUNAWATAKIA MGOMO MWEMA WENYE MABADILIKO




Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi (Cotwu) kimeikaba koo Serikali na kudai kuwa hakitaitikia ombi la kuwataka wafanyakazi kusitisha mgomo wa nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Cotwu, Omari Guledi, kufuatia barua waliotumiwa na Baraza la Ushauri Uchumi na Jamii (LESCO) la kuwataka wakutane mwezi ujao kwenye meza ya mazungumzo.

Alisema muda huo sio wa kuketi mezani tena na serikali, badala yake ijibu hoja na madai ya wafanyakazi na si kusubiri hadi mgomo umepamba moto ndipo inatuma barua za mazungumzo.

“Ni kweli nimepokea barua kutoka LESCO ikinitaka tukutane kwenye meza ya mazungumzo kitu ambacho kwa sasa hakiwezekani kwani taarifa ya mgomo ilifikiwa na mkutanao mkuu wa Tcta ambao huitishwa mara moja kwa mwaka,” alisema.

Alilisisitiza kuwa mgomo utakuwepo kama ilivyopangwa kwani imefika wakati sasa kila mafanyakazi anaonekana kuchoka.

Naye Katibu Cotwu, Matias Mjema, alisema wao wanawashawishi wafanyakazi wote wagome kwani maneno kutoka serikalini yamekuwa mengi na hivyo wamechoka.

Alisema kinachoshangaza ni serikali ilikuwa wapi muda wote huo mpaka vyama vya wafanyakazi kufikia maamuzi ya mwisho.

Mjema aliwatoa hofu wafanyakazi kuwa mpaka sasa hamna mazungumzo yoyote na serikali kwani vyama vyote vimekataa ombi hilo na kudai kuwa mwaliko huo haukuja wakati mwafaka.

Tucta ilitangaza mgomo wa wafanyakazi nchi nzima Mei 5, mwaka huu kufuatia madai yao ikiwemo nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kutoka Sh. 104, 000 hadi 315,000 kwa mwezi.

Wakati wa kutangaza mgomo huo baadhi ya vyama vimedai kuwa serikali inadharau wafanyakazi kwa kuwalipa kiasi kidogo cha mshahara ambacho ni sawa na posho ya siku ya moja ya Mbunge..

Wafanyakazi hao walisema katika matamko yao kwamba serikali imekuwa mstari wa mbele kuwataka wasitishe mgomo ili wafanye mazungumzo, jambo ambalo mara zote limekuwa kama mbinu za kuwalaghai na baadaye halitekelezi.

Vyama vingi vya wafanyakazi vimetangaza kuunga mkono mgomo huo.


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom