Mgomo wa UDOM: Ni kweli FFU waliua wanafunzi wawili?

Tatizo kuna watu wanashindwa kuelewa maana ya neno "Tetesi". Angalia mwanzo wa heading ya hii thread harafu endelea kuchangia maada.
 
Mbona hao wanafunzi hawatajwi majina?
Au kifo kimekuwa siri siku hizi?
 


Kwanini unakurupuka kujibu hovyo hovyo bila kufikiri kidogo?...Hii ni tuhuma tu ambayo inagusa maisha ya watu kwa namna moja ama nyingine...ni heri iwe ni uzushi,lakini km kweli yalitokea tunahitaji mamlaka zenye dhamana zitoe tamko na hatua stahiki zilizochukuliwa....mliopo Dodoma tupeni vithibitisho zaidi tulie na hawa watu waliofanya udhalimu huu...kuna utaratibu wa kutangaza na kubandika matukio makubwa as well as madogo yanayowagusa wanachuo as well as utawala,nadhani tutajua ukweli tu soon..[/QUOTE]

SIPO DODOMA LAKINI NILIOWASILIANA NAO HUKO DODOMA WANASEMA HAKUNA KITU KAMA HICHO. NI UZUSHI TU. HAKUNA MWANAFUNZI WA UDOM ALIYEKUFA MWEZI HUU. WALIOFIKISHWA HOSPITALI YA MKOA WALIKUWA NA MAJERAHA MADOGO MADOGO TU NA KURUHUSIWA. HABARI ZA KUBAKWA MWANAFUNZI AU WANAFUNZI WA UDOM HAZIPO KABISA TENA WANASHANGAA. HUYO ANAYESEMA KUNA VITU KAMA HIVYO NI BORA AKATOA NA USHAHIDI
 
Ndugu 'Superman', 'Kweleakwelea', 'Jasusi', 'Mzee Invisible' na wengine jamvini, hebu ingieni msituni mara moja kutafuta taarifa kamili juu ya UDOM na madai haya ya mauaji.

Ni hatari sana kulinganisha UHAI WA MTU na kutamani kuficha mambo ili fulani aendelee kula keki asitimuliwe ofisi katika wizara fulani. Instances of 'EXTREME POLICE BRUTALITY' in Tanzania, excessive force on demostrators and rape case, the number of COLD-BLOOD KILLINGS, and prison silent murders are disturbingling on the rise SIDE-BY-SIDE with the increase in reports of MEGA-CORRUPTION scandles in our country.

Something is seriously wrong somewhere people on innocent university students merely using their constitutional rights to express their disatisfaction on certain things. Kuficha kifo ili waziri aendelee na kazi??? Na mambo yakija kujianika kweupeeee .... !!!!!

Halafu wanajamvini, tuone sababu ya kuwa Great Thinkers wa kweli wakati wote na tuwape wanafunzi hawa wa UDOM ushirikiano wanaouhitaji kwetu. Tusiwakemee wakati wote huku tukijua fika ya kwamba wakosaji wa hili na lile siku zote inakua ni mtu tu au kikundi kidogo miongoni mwao bila hata ya ridhaa yao.

Sidhani kama MAWAZIRI wetu hawa ambao miaka yote wajaa kiburi na kujiona zaidi ya binadamu wa kawaida, waanze tu hivi hivi kujikimbia Dodoma na kuendesha kikao hadi saa nane alfaji.

Si kawaida kwa serikali yetu ambayo kwake swala la uwajibikaji (ukiachilia mbali tu Mzee Mwinyi miaka hiyo, Pro Mbilinyi na Mporogomy) waanze tu kufumuka na KUKUBALI KILA KITU HADI NA YALE AMBAYO WANAFUNZI hawakuomba, kuna jambo zito ambalo magati yetu ya 'This Day', 'MwanaHalisi' tu ndio wanaoweza sasa kutupa HABARI KAMILI.

Hizi serikali zetu kunakonunuliwa vyeo siku zote ni kuburi kwa kwenda mbele. 'Wazee wa Africa Mashariki' hadi leo wanasota halafu ....
 
Mnh! FFU walimkabakeje mwanafunzi wakati wa maandamano? au kama mbuzi njiani mbio mbio...tusubiri mashahidi watambie
 
kumaliza utata tunamuomba mtu yeyote ambae yupo karibu na kubenea au ulimwengu watie timu udom kupata ukweli then mambo yawe hadharani.

Kwa Kubenea, Jenerali Ulimwengu, na hata kale ka-gazeti ka 'UWAZI' miaka fulani hivi wangekuja na full mkanda katika hili.

Hata hivyo, kuna vyombo vya kutosha tu ndani ya asasi za kiraia za hapa nchini na Kimatataifa; shughuli inayopigwa hapo chini usiombe, mara utausikia huko ma-Uingereza hukoo.

Kwani kuna nyaraka ngapi tunafichiwa hapa nyumbani huku wenzetu walioko majuu wanatueleza kwamba hizo hizo nyaraka nyeti na za siri hapa kwetu ndio wanatumia kama case-study za kufundishia darasani.

Hata hii mikataba ya Dowans tumefichwa usikute huko ni hadhari tu.
 
@engmtolera [I]kwanza mimi huwa nawachukia sana watu kama nyinyi wenye fikra finyu za kufikiria kwa kuangalia mwisho wa vidole vyako,nawachukia sana watu wasiokubali kubadilika na kutambuwa michango ya watu wengine,may be tubomoe chuo cha udom ili tuweze kuwafurahisha wana jf furani kwani yaonekana udom ni kero kwa watu wasiohitaji nchi hii iendelee ktk nyanja za elimu.

mkuu kubali kubadilika na tambuwa michango ya hii serikali,si vyema kuendelea kukejeri na kudharau chuo ambacho hata wajukuu wako watakuja kusoma hapo baadae
mapinduziiii daimaaa[/QUOTE][/I]

(red)Much better kuliko kuendelea kuwa na chuo kikuu cha kata tunahatarisha elimu yetu
 
NINAHISI KUNA WATU HUMU WAMEFANYA USAJILI MARA NYINGI ILI KUTOA MICHANGO INAYOLENGA KUPOTOSHA MWELEKEO WA FORUM HII!! SWALI LILILOULIZWA NI TETESI NA MUULIZAJI KAKILI KUWA KUNA TETESI. NI JAMBO RAHISI TU KWA WANAOFAHAMU KUSEMA NI KWELI NA VICTIMS NI ............. AMA SI KWELI NA WATU WOTE WAPO SALAMA CHUO. thats all!
 
Nipo UDOM, Kimsingi kuna haya madai kutoka kwa baadhi ya wanafunzi lakini ukijaribu kuwahoji mipasavyo kila mmoja anasema amesikia lakini hana uhakika. Ninahitimisha kwa kusema kwamba hakuna mtu aliyeuawa kwani kwa jinsi ninavyowafahamu wanafunzi lingekuwa limetokea pangechimbika
 
no comments.............ukweli utajulikana tu,lakini kama serikali ikiamua kufunika itafunika tu,mnakumbuka yule mtoto aliegongwa na moja ya gari lililokua kwenye msafara wa kampeni za urais kupitia chama cha kijani mbona polisi walikuja kusema eti yule mtoto aligongwa na gari jingine ambalo halikua kwenye msafara,MUNGU TUSAIDIE
 
Nipo UDOM, Kimsingi kuna haya madai kutoka kwa baadhi ya wanafunzi lakini ukijaribu kuwahoji mipasavyo kila mmoja anasema amesikia lakini hana uhakika. Ninahitimisha kwa kusema kwamba hakuna mtu aliyeuawa kwani kwa jinsi ninavyowafahamu wanafunzi lingekuwa limetokea pangechimbika

ila kwa wana udom me nina mashaka kidogo.....
 
Back
Top Bottom