Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Mgomo ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), umeingia dosari baada ya kubainika kutokuwa na tija kwa uchumi wa nchi na ustawi wa jamii.
Ikiwa mgomo huo unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 5, mwaka huu utafanikiwa, ni dhahiri kwamba utafanyika wakati ambapo mkutano wa kuhusu hali ya uchumi duniani (WEF) utakaoanza Mei 5 hadi 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utajumuisha wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji na taasisi za kiuchumi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Hivyo, usumbufu utakaotokana na mgomo huo si kwamba utawaathiri raia na watu wengine wanaoishi nchini tu, bali pia washiriki wa mkutano huo kutoka maeneo mbalimbali duniani, wakiwemo wawekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko, amesema mgomo wa wafanyakazi haupaswi kufanyika kwa vile athari zake zitakuwa kubwa kwa uchumi wa nchi na Watanzania wenyewe.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Ole Naiko, alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini ni fursa muhimu itakayothibitisha kuwepo kwa mazingira bora ya uwekezaji nchini.
Ole Naiko alisema migomo ni miongoni mwa adui wakubwa katika uwekezaji, hivyo ikiwa utafanyika wakati wa WEF, kuna hatari ya kujenga hofu na woga kwa wafanyabiashara wa nje wenye nia ya kuwekeza nchini.
Mkurugenzi huyo wa TIC alisema, mabadiliko ya uchumi wa dunia yameifanya sekta binafsi kuwa mwajiri mkuu wa wananchi walio wengi, hivyo ufanisi katika kuepuka mgomo unaoratibiwa na Tucta ni jambo lenye maana kubwa.
"Kama mgomo huu utafanyika wakati wawekezaji wakiwa hapa nchini, hii ni sawa na kujenga mazingira ya kuwakimbiza (wawekezaji), hivyo kuongeza tatizo la ajira nchini," alisema.
Alisema kwa hali hiyo Taifa linapaswa kupiga hatua katika kuhamasisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na kusema mkutano wa WEF ni moja ya fursa itakayochochea ufanisi huo.
"Kuna umuhimu wa kusaidiana, tusaidiane kama Taifa ili suala hili la mgomo lijadiliwe kwa ustaarabu," alisema.
Kwa upande wake, mmoja wa waratibu wa mgomo wa wafanyakazi, Gratian Mukoba, alipendekeza kwa serikali kuwezesha mchakato utakaofanikisha kupata suluhu ya madai ya msingi yanayosababisha hali hiyo.
Kutoka mkoani Kilimanjaro, Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Patrick Boisafi, alisema mgomo huo unajionyesha katika taswira ya kukidhi matakwa ya kisiasa zaidi ya maslahi ya nchi.
Alisema kwa nchi changa ikiwemo Tanzania, mgomo kama unaoitishwa na Tucta, una athari nyingi za kiuchumi na kijamii, hivyo njia pekee ni kudhibiti ili usitokee.
Boisafi alitoa mfano kuwa madai ya kupandisha kima cha chini cha mshahara kama inavyotajwa na Tucta, yanapaswa kuwiana na hali ya uchumi iliyopo badala ya `kukurupuka' kiasi cha kutokuwa na tija kwa pande zote.
Kwa hali hiyo, Boisafi alieleza kushangazwa na tamko la Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, kutangaza ongezeko la mishahara kwa sekta binafsi kufikia asilimia 100.
Habari hii imeandikwa na Mashaka Mgeta, Dar es Salaam na Salome Kitomari, Kilimanjaro
From Nipashe