Mgomo wa Madaktari: Serikali Yasalimu Amri! Yaomba Mazungumzo Upya!

Hakuna aliyetishwa, wameamrishwa, waliorudi wamerudi wasio rudi hawajarudi, sasa hivi natazama TV leo asubuhi Madaktari wote wa Mbeya wameripoti na hakuna mgomo huko, au hulijui hilo?

Faiza umechukua nafasi ya Tambwe Hiza? Naona nafasi ya propaganda unaimudu sana yaani unaposema mavi yanukia waridi unaniacha hoi.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mkuu uniquote vibaya aliyesema madaktari ni Faiza Foxy

Chama
Gongo la Mboto DSM

mkuu sikukwoti vibaya, mimi na wewe hoja yetu ni moja yaani kuwashangaa hao Kina Pinda na FF ambao sasa hivi wanawaita madaktari wetu uchwara.
 
Huo sio ukweli, hawa madaktari uchwara wanaochochea hii migomo wanajulikana agenda zao za siri na kina nani wanaowachochea, Serikali inafanya kila njia isiwape mwanya, lakini mwenye lake hakosi kulitafuta.

Ukweli ni nani asioujuwa?

Hapo kwenye red ndio maana viongozi wetu huwa wanatibiwa nje ya nchi?
 
Ni mbunge hadi hivi sasa amesema nini? au hana upande sasa hivi hadi awe na madaraka serikalini?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Vacuum ya utendaji wa Lowasa inaonekana serikalini.

Udhaifu huu wa kiuongozi wa JK haukuwahi kuonekana kipindi chote Lowassa yuko serikalini kama PM. Kipindi kile Lowassa alikuwa anatoa shingo nje ikatwe kwa mufaa ya JK, hivi sasa hakuna wa kufanya hivyo
 
Kama nilimwelewa vizuri Pinda, hakumaanisha kuwa serikali haitawasikiliza tena madaktari bali aliwataka warejee kazini na madai yao yale yanayowezekana kwa sasa yatashughulikiwa na mengine yatasubiri bajeti.... hata hivyo yetu masikio, lakini natumai msimamo wa serikali ni ule ule.
 
Kaka, serikali haikuwa na lengo la kutatua mgogoro; walichotaka ni kulazimisha hoja ziishe kwa sababu wao wana dola. Wangeweza kabisa kufanya mazungumzo haya kwa kuonesha unyenyekevu na kukaa chini lakini wakataka madaktari waende kuwabembeleza kwenye viti vyao vya enzi! Hivi unafikiria kama ungekuwa mwaka wa uchaguzi serikali inge react hivi? Sasa hivi serikali imetambua kuwa "hiari yashinda utumwa"; wametambua serikali haina support kwa wananchi kwenye hili. Sasa, pa kuanzia ni kuwafuta kazi Waziri, Katibu na Mganga mkuu kwanza kuonesha kweli wameyapa uzito madai ya madaktari kutoka hapo mambo mengine yanzungumzika tena kwa haraka kweli.
Mkuu wangu sidhani kama tunaelewana. hata hivyo nimeandika hoja yangu nyuma kidogo siioni tena sijui imepotelea wapi.. nitarudia maswala yangu..

1. Hawa madaktari wanasema hawataki kuonana na viongozi wa wizara toka mwanzo wakimtaka waziri mkuu. nani asiyetaka mazungumzo..
2. Ijumaa tu tuliambiwa waziri mkuu alikuwa akutane hnao Karimjee kwa kuzingatia usalama wake, wakakataa wakitaka waziri mkuu aende Starlight na ubishi ukawa huo hadi siku inakwisha na ndipo Pinda akasema wakutane Jumapili wao wakajibu hawawezi kutana naye Jumapili isipokuwa Jumatatu Karimjee au sijui Starlight. haikuwekwa wazi ktk mvutano huo..
3. Sababu tulizopewa wallikuwa wakisubiri watu kutoka mikoani nami nauliza ile siku ya kwanza walipotaka kuonana na waziri mkuu walikuwa tayari vipi ikiwa wa mikoani hawakuwepo?..
4. Leo hii nimepata habari ya kwamba MAT hawakuwasiliana hata na TUCTA kuhusiana na mgomo huu wakati TUCTA ndicho chombo cha waajiriwa watumishi wa Umma. Na viongoizi wa MAT ni madaktari kutoka private Hospitals.. vipi hii kitu..
5. haya leo tena tunaambiwa wamekubali kukutana na viongozi wa wizara ya Afya kwa nini walikataa siku ya kwanza wakisema hawa ndio sababu hadi wamefikia hapa walipo?.Wanamtaka waziri mkuu tu.
6. Kwa nini wafanya mgomo wakati rais yuko ziara nje ya nchi?

Hivyo inaonyesha mambo haya yanafanywa kienyeji sana kiasi kwamba hakuna utaratibu. Na sii ajabu tukaambiwa tena madaktari wamekataa kuzungumza na waziri wa Afya wakimtaka waziri mkuu au rais..
 
Hata Malria ya Zitto wameshindwa kuitibu mpaka kenda India, sasa kama sio uchwara ni nini hao? vilaza tu, watu zinawapeleka hapo dhiki tu, mwenye uwezo anaenda kutibiwa hapo? thubutu. Ukweli ubaki kuwa ukweli.
zitto aligunduliwa kuwa na chronic sinusitis na daktari anayeitwa juma mfinanga,aliyesoma na kufanya kazi muhimbili .kilichoshindikana ni vifaa vya kimtibia hapa muhimbili.madaktari wetu wana ujuzi sana ila tunawakwamisha kufanya kazi.
 
Hatimaye serikali imesalimu amri, yatafuta mazungumzo upya na madaktari.

Source ni Waziri wa Afya akizungumza na BBC Swahili jioni hii.

Dr. Mponda amesisitiza licha ya madaktari hao kuamriwa kurudi kazini, Dr. Mponda amesema baadhi ya madai ya madaktari hao ni genuine hivyo serikali bado iko tayari kuzungumza nao nini inaweza kutekeleza na nini haiwezi!.

BBC pia ilimpata Dr. Ulimboka ambaye alikubali kuwa wako tayari kuzungumza na Pinda. Dr. Ulimboka amesema wazi hawako tayari kuzungumza na watendaji wa wizarani ambao ndio wameufikisha mgogoro huo hapo ulipofika!.

My Take
Kumbe serikali bado iko tayari kuendeleza mazungumzo!. Sasa kwa nini Pinda aliharakisha kuutoa msimamo ule ile Jumapili ilhali ingesubiri mpaka Jumatatu ndipo wangeyamaliza!.

Kurejea kwenye meza ya mazungumzo ni uthibitisho mwingine wa serikali legelege dhaifu na ya waoga kama kunguru!.

Kwa serikali sasa kuwapigia magoti madaktari, Mhe. Pinda nae sasa awajibike kwa aibu!. Afadhali ya Lowassa aliwajibika ili kusave faces, Pinda awajibike kwa aibu ya mwaka kujidai kuchukua maamuzi magumu wakati uwezo hana!.

Oh poor government!.

Aibu!.

Alitoa maamuzi hayo ili apate nafasi ya kwenda bungeni kupitisha nyongeza haramu ya posho zawabunge.
 
madaktari wenyewe wameshiba kama vyura vya kihans hata kupumua tabu sijui watawezaje kuhudumha wagonjwa wote hao

Halafu sasa yule kiongozi wao hao wanajeshi madaktari ni babu tena inaonekana kabisa ametoka kwenye retirement kwa jinsi nilivyomuona kwenye taarifa ya habari, umri umeenda sana.
 
zitto aligunduliwa kuwa na chronic sinusitis na daktari anayeitwa juma mfinanga,aliyesoma na kufanya kazi muhimbili .kilichoshindikana ni vifaa vya kimtibia hapa muhimbili.madaktari wetu wana ujuzi sana ila tunawakwamisha kufanya kazi.

Na kama kumbukumbu zangu ni sahihi hata malaria yake iligunduliwa Muhimbili. Agha Khan hawakuona kitu!
 
Ushasema walalahoi. Wewe unafikiri wanaokwenda nje ni viongozi tu? watu wengi sana wenye uwezo wao wanakwenda nje, au wanakwenda Hospitali za kulipia au hata hapo Muhimbili wanaenda fast track, na wengi waa kiumwa hupiga simu na madaktari bingwa huwafata majumbani mwao, yote ni mambo ya uwezo tu. Hakuna siri kwa hilo.

Wangekuwa wanajuwa kuwa wanawasaidia walalahoi tusingewaona wakigoma, wapo hapo kwa maslahi na walalahoi wanakwenda huko kwa kuwa hawana option, wangekuwa na options usingewaona huko.

Ngoja niwatafite wawekezaji wa Hospitali za uhakika sasa, nilete na madaktari wa uhakika, hivi uchwara labda vitajifunza zaidi.

Tutawezekeza mpaka mahousegirl.
 
Kwa hiyo hairuhusiwi kufanya mgomo wakati rais akiwa nje ya nchi? Kwamba wangesubiri mpaka rais arudi ndio wagome?
Bila shaka, ni ujinga mke/mume kufanya mgomo wakati mume/mke yuko nje safarini. unaumiza watoto ili iweje?..Hivi unataka kunambia hawa madaktari walitegemea Pinda ataweza kutoa majibu ya madai yao? hivi kweli unafikiri Pinda anaweza kusema posho zetu zitaongezwa na kuwa Tsh 200,000 kwa siku!..
 
Na yule aliye-mpasuwa mtu kichwa badala ya mguu? alikuwa hana vifaa?

Uwezo gani wewe? watu wanaenda hapo kwa kuwa hawana option tu, daktari wa maana atakaa hapo? angoje nini? hao wote waliokuwepo ni uchwara tu.
yule aleyehusishwa na sakata hilo ambalo ni kawaida katika medical field ni one of the three neurosurgions in tanzania uliza ameokoa na anaendelea kuokoa watanzania wangapi leo hii?uliza yuko wapi kama sasa hivi kama sio MOI.
 
Back
Top Bottom