Mgomo wa Madaktari: Serikali Yasalimu Amri! Yaomba Mazungumzo Upya!

Mbona sielewi kwani serikali ilikataa mazungumzo na madaktari au madaktari ndio walikataa mazungumzo na viongozi wa wizara ya Afya wakimtaka waziri mkuu?.. Sasa haya mazungumzo mapya yanahusu kitu gani kinyume cha yale yaliyotangulia!
 
Madaktari na manesi wetu kote nchini KAZENI UZI ZAIDI kwani kwa ujasiri huu matakwa yenu ytajipa badla ya kuwazawadia wale wazembe wa Bungeni Dodoma Posho-Mshahara-wa-Mtu mpewe nyinyi kwani ndio mnaotujali afya zetu.

Wananchi tunawaunga mkono kwa kila namna n hao 'Ma-Zimbwela' waliovishwa nguo za udaktari kuonekana madaktari huko Mout Meru Arusha WAKOME KABISA kabla machalii hawajawapa fundisho sawa na Madiwani wa CHADEMA walipotikisa kiberiti katika mji huo wa A-Taun.


Pinda unawafukuza lini madaktari? mbona hutoi tamko?
 
huyu pinda kilaza sana.jikumbushe staili aliyotumia katika mgogoro wa madiwani arusha,alikurupuka sana alakini ukweli ulidhihirika baadae,ikawa aibu yake,kama anabisha mulizeni mbunge LEMA
 
Nimeyapenda maneno hayo chini hadi nimeweka kama sahihi yangu.

Kaka yangu haya mambo yanachosha sana,sasa hivi naangalia taarifa channel 10,madaktari aliokuwa anajivunia PM kutoka Lugalo ni 15 tu ndio wamepelekwa Muhimbili,kweli unawatolea watu vitisho vya kuwafukuza kazi,kumbe back up unayotegemea ni Madaktari 15 tu,hii siasa itatufikisha kubaya .
 
Mbona sielewi kwani serikali ilikataa mazungumzo na madaktari au madaktari ndio walikataa mazungumzo na viongozi wa wizara ya Afya wakimtaka waziri mkuu?.. Sasa haya mazungumzo mapya yanahusu kitu gani kinyume cha yale yaliyotangulia!

Mkandara the whole saga ni vulu vulu. Serikali ikisema nyundo madaktari wanasema maziwa ili mradi mambo hayajakaa sawa. Lakini nahisi mzizi wa kutoelewana kati ya serikali na hawa madaktari ni wajumbe/washauri toka ofisi ya waziri mkuu. Kuna tabia (ya muda mrefu) kwa watu wanaowazunguka viongozi wakuu kupindisha mambo! Sijui kwa nini? Pia wakubwa nao wamekuwa na tabia ya kuto-cross check kile wanachoombiwa. Matekoe yake unakuta viongozi wanatoa matamko kwa mambo ambayo sivyo.

Kwa mfano madaktari walisema kabisa hawawezi kuonana na waziri mkuu Jumapili kwa sababu timu ilikuwa haijatimia, sasa kwa nini Waziri mkuu alienda Karimjee? Watu wake walimwambia nini baada ya madaktari kuwaambia categorically kuwa Jumapili haiwezekani? Au walifiri madkatari wana tania? Wapi skills za negotion? Na kama wakubwa wetu wanashindwa ku-negotiate mambo madogo kama kukutanisha Waziri mkuu na madaktari wanawezaje ku-negotiate mambo mazito kwenye ulingo wa kimataifa ambapo wajanja wanatumia kila mbinu kupata kile wanataka?
 
Serikali haikusita kuongea na Madaktari, madaktari ndio waliosita kuongea na Serikali. Hata Pinda alisema waziwazi milango ya maongezi iko wazi. Kwanini mnapenda kusema uongo?

Serikali ya Kikwete ni sikivu kuliko Serikali yoyote ile. Ni nani asiyelijuwa hilo? Tumeona kina Mbowe na Slaa hata walipo susa Rais akawaambia mtakuja tu, na walipokwenda akawapokea na kuwapa Juisi kwa mkono wake. Jee, nani asiyeyajuwa hayo?

Aksante FF
Hii serikali ni sikivu sana kiasi kwamba haikuona umuhimu wa kureact faster mpaka baada ya siku kadhaa za mgomo?? Kweli ni serikali sikivu.
 
Hatimaye serikali imesalimu amri, yatafuta mazungumzo upya na madaktari.

Source ni Waziri wa Afya akizungumza na BBC Swahili jioni hii.

More to follow!

Ni kituko cha mwaka!!!! Waziri mkuu anastahili kujiuzulu kwa kushindwa kuwashawishi madaktari warudi kazini.
 
Dr. Mponda amesisitiza licha ya madaktari hao kuamriwa kurudi kazini, Dr. Mponda amesema baadhi ya madai ya madaktari hao ni genuine hivyo serikali bado iko tayari kuzungumza nao nini inaweza kutekeleza na nini haiwezi!.

BBC pia ilimpata Dr. Ulimboka ambaye alikubali kuwa wako tayari kuzungumza na Pinda. Dr. Ulimboka amesema wazi hawako tayari kuzungumza na watendaji wa wizarani ambao ndio wameufikisha mgogoro huo hapo ulipofika!.

My Take
Kumbe serikali bado iko tayari kuendeleza mazungumzo!. Sasa kwa nini Pinda aliharakisha kuutoa msimamo ule ile Jumapili ilhali ingesubiri mpaka Jumatatu ndipo wangeyamaliza!.

Kurejea kwenye meza ya mazungumzo ni uthibitisho mwingine wa serikali legelege dhaifu na ya waoga kama kunguru!.

Kwa serikali sasa kuwapigia magoti madaktari, Mhe. Pinda nae sasa awajibike kwa aibu!. Afadhali ya Lowassa aliwajibika ili kusave faces, Pinda awajibike kwa aibu ya mwaka kujidai kuchukua maamuzi magumu wakati uwezo hana!.

Oh poor government!.

Aibu!.
 
Tusiwabeze, wamejirudi na kuchagua njia ya busara. Tuwapongeze kwa hatua hiyo!
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom