Hivi unapomwita mkuu wa nchi kilaza unajisikiaje? Tena unamlinganisha na mwanae; hivi ungetendewa wewe hivyo ungejisikiaje. Usimtendee mwenzako usilopenda kutendewa wewe. Hata kama ana makosa ziko lugha za kuongea kama great thinkers sio kama kijiweni. Alichokosea ni nini? Je haki ya mwanadamu ni kifo au uhai? Ina maana ni sahihi madaktari kufanya madai yao kwa gharama za uhai wetu? Au wewe hujawahi kuuguliwa? Je unajua madaktari wanalipwa kiasi gani ukilinganisha na watumishi wengine wa umma? Je wao ndio wenye haki tu ya kulipwa fedha hata kama ni za bajeti yote na watumishi wengine waendelee kufa njaa? Let us be serious and realistic!!!!!!!!!!! Unapochangia jambo tafuta ukweli wa upande wa pili. Hebu fanya utafiti kidogo madaktari wanalipwaje ukilinganisha na watumishi wengine wa Serikali. Linganisha Scale yoyote ya madaktari uilinganishe na scale ya watumishi wengine wa serikali k.m. walimu, polisi, wahasibun.k. Uone jinsi ambavyo mishahara yao ni kama mara karibu tatu ya hao wengine. Sikatai kwamba wana haki ya kudai haki zao lakini si kwa gharama ya maisha ya watu na kwa kuzingatia kile wanacholipwa sasa na ukweli kwamba serikali ilishapokea madai yao.
Hivi madaktari wakipewa malipo wanayotaka na wahasibu nao wakagoma nao wadai kulipwa kama madaktari, wao watalipwa na nani? Au polisi wakigoma itakuwaje? Wote hatuwezi kuwa madaktari, uhasibu au ulinzi ungefanywa na nani ili wao waweze kufanya kazi zao? Sisi tu mwili mmoja kila mmoja ni kiungo kwa mwenzake hakuna ambaye peke yake anaweza kufanya kila kitu peke yake. Tuache ubinafsi kila mmoja anahitaji maisha mazuri.:lock1::decision::attention:
nimefatilia hoja zote za huu uzi ila nimeona hoja yako haistahili kuwepo hapa, jifunze kuwajibika na uiondoe maana haina maana na haileti motisha kwa wasomaji. Unasema eti kila fani ikigoma eti itakuwaje? Fani ya kutibu wagonjwa na kuuguza unafananisha na uhasibu? Damn siamini kama ulifikiri kabla ya kupost hii hoja yako.