Mgomo wa madaktari na uongozi wa nchi

Posa

Member
Nov 12, 2010
76
79
Ni mara ya tatu sasa mgomo wa madaktari unatokea na mara zote uongozi wa nchi haonekani badala yake wanakuja kutusomea postmortem.

Hivi nini maana uongozi maana sio katika hili tu bali ni kwenye mambo mengi makubwa na madogo madogo ya nchi hii. Rais yuko wapi au baada ya watu kufa tusubiri mkutano wa wazee wa dar?
 
Tathmini yao ilionyesgha kuwa migomo ya awali haikuwa na madhara (kumb: Taarifa ya Naibu waziri wa Afya Bungeni). Hivyo serikali yetu hii inaamini hii migomo si tishio wala shinikizo.
 
Inatakiwa busara ya hali ya juu sana kupita uwezo wa kawaida wa viongozi wa sasa na dhamira ya kweli na dhati kumaliza tatizo hili.

Basically inafika wakati Madaktari wanakosa the best alternative ya kudai haki zao na mazingira bora ya kazi zaidi ya hii ya kugoma.

Lakini pia, kutimiza madai ya Madaktari kunahitajika pesa za ziada ambazo, kama serikali iko very very serious na ina dhamira ya kweli hizo pesa zinaweza kupatikana simply kwa kukusanya kodi vizuri, kuziba mianya ya rushwa, kupunguza matumizi na kubuni vyanzo vingine vya fedha na mapato.

Lakini pia, kutekeleza madai ya madaktari, ni kufungua njia ya sekta nyingine kama Elimu, nk kuanza kudai haki yao na hivyo kusababisha migomo zaidi.

Ndiyo maana nasema inatakiwa busara ya hali ya juu sana. It is about total change and 100% commitment kumaliza mgomo huu wa Madaktari.

Na kama kweli Madaktari wamedhamiria as they sound this time, the government will never have any alternative other than bowing down. Wasipo bow down na watu wakafa, what happened last time will happen this time massively: Wanaharakati will join mgomo, Wanafunzi; Raia, nk.

Wasipokuwa makini, hii pia ni kete muhimu kwa opposition.

Kama Madakatari wameamua kweli kujitoa muhanga, they just remind me of some of the readings: "Ili wengi wapone, moja lazima afe kwa ajili yao". Literally means, kwa madaktari kujitoa na raia kuathirika au kuwa wahanga ikiwepo vifo, it is only way Serikali ya Kidikteta itasikia na kubadilika (Utawala wa Kidikteta si lazima utumie mabavu, ila kutowapatia raia haki zao ni aina ya Udikteta).

Siungi Mkono Mgomo maana najua wengi watakufa na kaathirika, lakini kama Serikali imeweka pamba masikioni, Goo . . Gooo Doctors on Strike.

Rwanda inaheshimiwa sana Duniani sasa kwa better performance because of Genocide. Kama ina maana kupitia mgomo huu, tanzania will change for better, then let it me. It is a bitter pill to swallow, but we will finally get cured.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Inatakiwa busara ya hali ya juu sana kupita uwezo wa kawaida wa viongozi wa sasa na dhamira ya kweli na dhati kumaliza tatizo hili.

Basically inafika wakati Madaktari wanakosa the best alternative ya kudai haki zao na mazingira bora ya kazi zaidi ya hii ya kugoma.

Lakini pia, kutimiza madai ya Madaktari kunahitajika pesa za ziada ambazo, kama serikali iko very very serious na ina dhamira ya kweli hizo pesa zinaweza kupatikana simply kwa kukusanya kodi vizuri, kuziba mianya ya rushwa, kupunguza matumizi na kubuni vyanzo vingine vya fedha na mapato...

Nakubaliana na mtazamo wako Ndugu Allien. Sasa hapa unamshauri nani kutumia busara ya hali ya juu?

Nionavyo mimi muda wa kutumia busara ulikuwepo tangu kitambo, na hili sakata lisingefika hapa lilipo sasa. Tatizo kubwa ninaloliona ni badala ya busara kutumika, serikali imekuwa ikipika propaganda na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya madaktari. Hii imepelekea wengi kukiuka ethics zao kwani wakiitikia wito wao wanaonekana madai yao si ya msingi.

Ukisikiliza madaktari wanasema wanataka kuboreshwa kwa huduma na maslahi yao, ila serikali inapiga kelele kuwa madaktari wanapigania maslahi yao ambayo ni makubwa.

Sikuwahi hata sikumoja kusikia Serikali ikitolea tamko ama ufafanuzi juu ya yale madai yanayopiganiwa katika kuboresha huduma za afya kama madawa, vifaa na mitambo, vitanda, ukarabati nk. Je serikali haioni kipaumbele/msingi wa kuboresha mazingira ya afya kwa ujumla ili kuboresha afya za walipa kodi wake?
 
Ni mara ya tatu sasa mgomo wa madaktari unatokea na mara zote uongozi wa nchi haonekani badala yake wanakuja kutusomea postmortem. Hivi nini maana uongozi maana sio katika hili tu bali ni kwenye mambo mengi makubwa na madogo madogo ya nchi hii. Rais yuko wapi au baada ya watu kufa tusubiri mkutano wa wazee wa dar.
Mbona mheshimiwa Mnyika alishafafanua hili bungeni tena bila hata kuumauma maneno, uDHAIFU wa rais, uZEMBE wa bunge na upuuzi wa CCM.
 
Kama serikali haimfahamu alietisha mgomo wa Madaktari na mahakama kutoa hukumu ya kesi kwa chombo habacho hakihusiani na mgomo huo inaonyesha ya kua serikali haina nia na makini kulishughulikia matatizo ya madaktari.

Dkt. Mkopi aisahihisha, aifahamisha Serikali: Mgomo wa Madaktari haujaitishwa na MAT


Mgomo wa madaktari ulioanza juzi na unaoendelea bila kikomo hadi hapo masuala yaliyowekwa mezani yatakapotatuliwa, haujaitishwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi anaishangaa Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi kutoa agizo la kuitaka MAT isitishe mgomo.

Dkt. Mkopi emesema MAT haikutangaza mgomo wowote, siyo huu wala uliopita kwa kuwa inafahamu taratibu na sheria kwa kuwa chama hicho kipo chini ya Serikali.

"Hapa naona Serikali inajikanganya kabisa kwa sababu MAT haijatangaza mgomo huu, huu mgomo siyo wa MAT jamani, hata ule mgomo wa awali haukutangazwa na MAT. Hata mkitazama mabango yaliyobandikwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na sehemu nyingine yanasema kabisa ni Jumuiya ya Madaktari ndiyo iliyotangaza mgomo huo.

Lakini bila kufahamu, tunashangaa Mahakama Kuu inatuagiza sisi MAT tusitishe mgomo, hivi hili linatoka wapi? Hata kama hiyo taarifa ipo, bado haijatufikia kwani hata sisi tunaisikia kwenye vyombo vya habari tu. Kwa kifupi, MAT, sio ‘trade union' hii ni ‘professional union', kwa hiyo, siyo kila daktari ni lazima awe mwanachama wa MAT.

Daktari anaweza akawa mwanachama wa Jumuiya ya Madaktari, lakini siyo mwanachama wa MAT na pia mwanachama anaweza akawa pande zote mbili, yaani ni mwanachama wa MAT ni Jumuiya ya Madaktari. Kwa hiyo, inawezekana hao waliopo kwenye Jumuiya ya Madaktari siyo wanachama wa MAT, ndiyo maana nasema



Source: Dkt. Mkopi aisahihisha, aifahamisha Serikali: Mgomo wa Madaktari haujaitishwa na MAT - wavuti

 
watu wa kawaida hawana thamani mbele ya serikali yetu, ndio maana hata bajeti wameitengeneza kujifikiria wao zaidi. wananchi amkeni 2015 muwe makini zaidi lasivyo hali itazidi kua ngumu
 
[
Siungi Mkono Mgomo maana najua wengi watakufa na kaathirika, lakini kama Serikali imeweka pamba masikioni, Goo . . Gooo Doctors on Strike.

Baada ya mgomo wa kwanza nilishaona kuwa serikali imeweka pamba masikioni, na kitu ambacho inafanya ni kama mchezo wa chess. Tatizo ni kuwa wamekuwa wakifanya mchezo na maisha ya watu tokea siku nyingi.
 
Serikali ya mabulicheka hawajijui wanafanya nini hili la sasa litawapndoa kama walifanyia masihara
 
bila kujali alieitisha mgomo lakini wataoathirika ni sisi na ndugu na jamaa na marafiki zetu,acheni kushabikia ujinga.
 
bila kujali alieitisha mgomo lakini wataoathirika ni sisi na ndugu na jamaa na marafiki zetu,acheni kushabikia ujinga.

Dawa zikikosekana hospitalini huku unahudumiwa na muhudumu mwenye ukata na hasira atakayeathirika ni nani?
 
Sio kuwa haina nia ya kutatua mgogoro huo bali Mtu alie washauri kwenda mahakamani ni Dhaifu na alieona ni sifa kwama tume kwenda mahakamani Kuzuia mgomo nae Ni Dhaifu, Na Bunge lililokubali kuongezewa mishahara na Madiwani nao ni Dhaifu. Nani asiye jua kwamba ili uweze kuwa Daktari wa kutibu ni lazima uwe na akili nyingi haishangazi serikari kuzidiwa na Madoctor
 
Tuna rais dhaifu sana, asiyejua ni yapi majukumu yake, amekaa pale ikulu kama zuzu tu, rais mnafiki na asiyekuwa na uchungu na Taifa lake. Inashangaza sana, juzi kwenye mauaji ya raia wa Denmark kule mbugani Serengeti JK alikuwa very fast kutoa executive directives kwa mawaziri wake (Kagasheki na Nchmbi), lakini kwa swala la msingi na muhimu kama hili la madaktari JK amekaa kimya, as if hakuna kinachotokea. JK hatufai kabisa watanzania, hafai kuendelea kututumikia sisi wananchi, mbaya zaidi, sisi wananchi tunaendelea kumuacha akifanya madudu yake tu. Tubadilike jamani, tuandamane tukamtoe pale ikulu, hawezi kutupiga risasi raia wote, afterall akileta mzaha ICC itakuya yake...
 
Leo ni siku ya juma3 tar 25/06/12 ambapo wananchi wengi walisubiria kujua hatima ya mgomo wa madaktari. Taarifa ya habari ITV, STAR TV NA CHANEL TEN wameripoti kuwa hali ni mbaya Bugando , Mhimbili, MOI, OCEAN ROAD, MBEYA Kwani madaktari wengi wameunga mkono mgomo hali inayo wafanya wananch weng kuhaha huku walio na uwezo wakipeleka wagonjwa private. Kwa upande mwingine TBC1 Wameendelea na mgomo wa kutotangaza mgomo wa madaktari. Wa Tz kwakwel hali ni mbaya
 
Back
Top Bottom