Mgomo wa madaktari: Na makandokando yake

kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,213
849
Tangu mgomo wa madaktari uanze kumekuwa na maoni mengi, na hata matukio mengi. Moja kati ya hayo ni serikali kwenda mahakamani. Na kwa kufanya hivyo suala hili limeshindikana kujadiliwa bungeni na hivyo kukosa mawazo mbadala kutoka kwa wabunge ambao ungesaidia kuondoa mgomo huu.
Cha kushtusha wakati suala hilo lipo Mahakamani na Bunge likiwa limefungwa mdomo DR. Ulimboka alitekwa na kwenda kuteswa mahali ambapo miaka michache askri wetu walienda kuwauwa wafanya biashara wa madini. Na serikali imekataa kuhusika na hilo.
Wakati tukiwa bado tumepigwa na butwaa kuhusu suala la Dr. Ulimboka jana mchana serikali ilitangaza kupitia Mkurugenzi wa Hospital Mbeya kuwa madactari zaidi ya 80 walio kwenye mazoezi wamefukuzwa hapo hospitali ya Rufaa Mbeya na hivyo wanatakiwa kuondoka kwenye Makazi yao hapo hospitali ya Mbeya haraka iwezekavyo.
Ghafla jeshi la Polisi wakiwa wamevalia mavazi kama ya wale wanajeshi wa Marekani kule Afghnistani wakavamia makazi hayo na kuanza kuwatoa hiyo jioni bila ya kujua watakwenda wapi ukichukila kuwa hawa Madaktari kwao sio Mbeya.
Naomba kusaidiwa yafuatayo.
(1) Kama suala hili lipo mahakamani na hata bunge kushindwa kulijadili, je mamlaka ya kuwafukuza madaktari hawa yametolewa na mahakama gani?
(2) Upo utaratibu wa kumtoa mtumishi au mtu yoyote kwenye makazi ambayo alipewa kwa mujibu wa kanuni , hili suala la kuwatoa kwa tangazo la chini ya dakika tano na kwa kusimamiwa na polisi hii sheria serikali yetu imeinukuu kutoka nchi gani?
(4) Kwa zaidi ya miaka 10 sasa wananchi wa Mbeya wanaishi kwa mashaka kutokana na ujambazi wa upigaji nondo ambao mpaka sasa upo, je serikali isingeona busara kutumia nguvu hizi polisi kupambana na ujambazi badala ya Madaktari?
(3) Je kwa hekima ya serikali kuwafanyia hivi madaktari hao je haioni inawajengea hasira za ndani ambazo ni hatari kwa baadae kwa wanachi wanaohudumiwa na madaktari hao tukichukulia kuwa viongozi wetu wanatibiwa India na hawataathirika na haya?
(4) Na je kumekuwa na msemo kuwa kazi ya udaktari ni wito lakini tunafahamu hakuna chuo kinachotoa mafunzo haya bure na kuna vyuo vya udaktari hapa Tanzania ambavyo vinatoza mpaka karibu milioni 7 kwa mwaka na masomo ni ya miaka isiyopungua mitano, je kwa nini serikali isitangaze mafunzo hayo yawe bure sasa sifa ili suala la wito liwe na maana?
(4) Na kama kweli Udaktari ni wito, je kwa wito huo ina maana hata vifaa vya kazi kama dawa, gloves, sindano, sabuni nk. madaktari hao wawanunulie wagonjwa?
Naomba michango.
Edit Post Reply Reply With Quote



 
Utawala wa CCM unaelekea mwisho walidhani watamfikia mungu alipo sasa imekuwa kama wajenzi wa mnara wa BABERI mwisho wa siku lugha zao ziligongana hawakuelewana tena.Kwa upande wa serikali ndiyo hivyo hivyo sasa kila mmoja anatoa amri mwisho wa siku haonekani msema kweli.Serikali hiyo hiyo inakataa kufanya baadhi ya maamuzi eti suala liko mahakamani, lakini jana tunasikia serikali hiyo hiyo inatoa amri ya kufukuza madaktari hiyo amri ya mahakama itakuwa imevunjwa na nani sasa???? serikali imevunja au madaktari hiki ni kioja cha mwaka kwa JK
 
Back
Top Bottom