Mgomo wa madaktari: Mapendekezo ya utatuzi

Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,036
592
Kwa kuwa fedha za nyongeza ya wabunge laki mbili thelathini elfu zimekwisha tengwa na zipo,basi serikali ikubaliane na wabunge kuwa badala ya wao kupewa posho fedha hizo na nyongeza kidogo wapewe madaktari na wauguzi kama ongezeko kwenye mishahara yao.kwa mfano tuseme laki nne au tano hivi kwenye mishahara yao bila kujali vyeo vyao.

nadhani madaktari/wauguzi hili linaweza kujadilika,tuwaombe madaktari wasivute sana tunadhani wao pia wana simanzi na roho hawapendi hali ilipofikia.Cha msingi Serikali iwe wazi kwao kuhusu uwezo wake wa kifedha na siyo kwa kutumia lugha ya kimabavu.Tukumbuke madaktari wanaishi katika jamii na wasingependa kudharauliwa na jamii.

Hali inasikitisha sana,Tumwogope Mungu jamani.Watoto wetu wasio na hatia yoyote wanaendelea kufa.Chonde Chonde wakuu,tuuweke ubinadam na utu mbele maslahi nyuma.Tusaidianeni kutatua jambo hili:A S embarassed:
 
Wana Jamvi,

Kama ningekuwa JK, mara baada ya kufika tu Ikulu toka Davos na Addis, Ningefanya yafuatayo, kutokana na yaliyojili kwa watanzania wonyonge kuhusiana na suala hili la mgomo wa Madaktari,

1. Kuwafuta kazi viongozi wote waandamizi wa Wizara ya Afya,

2. Kutengua uteuzi wa Waziri Mkuu na kulipelekea Bunge kuridhia,

3. Kutengua maamuzi yote ya Serikali yaliyotolewa kuhusu kuzuia mgomo wa madaktari, na kuwaruhusu kuendelea na vikao vyao,

4. Ningewafuata Madaktari huko wanakotaka niwafuate na kuwaomba vitu viwili tu, Moja, tuendeleze mazungumzo ya matatizo yao na kuanza kuyatatua moja baada ya jingine na Pili, ningewaomba warudi waendelee na kazi ili kuokoa maisha ya wanyonge.

5. Ningeanza kupanga kikosi kazi kipya Wizara ya Afya na Kumtafuta Waziri Mkuu mwingine.

Nadhani hayo ndo maamuzi sahihi kwa wakati tete kama huu.
 
Bahati mbaya au nzuri wewe siyo JK kwa hiyo mawazo yako ya fikra mgando hutayatekeleza.... keep encouraging your self, one day you can be JK.
 
Bahati mbaya au nzuri wewe siyo JK kwa hiyo mawazo yako ya fikra mgando hutayatekeleza.... keep encouraging your self, one day you can be JK.

Ahsante VGL, maneno huumba. Lakini salamu atapata kuwa muna mgando unasema hivi....
 
409364_10150558169979098_722479097_8686047_953297106_n.jpg
 
poor thinking. unajua idadi ya madaktari nchi nzima? watagawana sh ngapi? wabunge ni 300 tu plus kidogo. hata hivyo siungi mkono kabisa hao wanaoitwa wabunge kujiongezea kujilipa kodi zetu.
 
hawa hawa maktari uchwara au wengine unaotaka Kikwete awasikilize? huoni unamfanya aonekane siyo kiongozi mzuri kwa kusikiliza madai ya madaktari uchwara? au sasa hivi wameacha kuwa uchwara?
 
Sikusema awasikilize nimesema atimize masharti waliomuwekea. Usipende kupachika maneno yako kwangu.

Kwanza hajawekewa masharti na madaktari; na pili kwa yeye kutimiza "masharti" yasiyokuwepo tena ya madaktari uchwara kutamfanya aonekane vibaya. Madaktari wana madai na ili aweze kutimiza madai hayo mutual respect is necessary. Hawezi kwenda huku akifikiria ni madaktari uchwara. Na kumtaka Rais kutimiza madai ya madaktari uchwara kunamfanya aonekane very incompetent indeed.
 
Umenivutia kwa heading nikajua nitakuta kitu cha maana, kumbe vita yako ni makanisa Muulize kwanza hela zilizomsafirisha kwenda davos zimetoka wapi si zingetolewa hizo maana ameenda kutuabisha tu
 
[JFMP3][/JFMP3]
Sikusema awasikilize nimesema atimize masharti waliomuwekea. Usipende kupachika maneno yako kwangu.
[JFMP3][/JFMP3]

Magwanda wamekuonga uwatetee madaktari? hao nakosea jina lako mama FF. Kweli magamba mmelemewa, mnaona madaraka yanawapotoka, si haba!
 
Sawa Mama! Ila baada ya Serikali kuondoa hizo ruzuku, Bugando na KCMC watalazimika kuweka viwango vya Aga Khan. Je wananchi wa kawaida mtaziweza gharama hizo?

Na je, wafaham ni kiasi gani serikali inadaiwa na Kanisa? Serikali yetu hii, kuwa na mkataba nayo ni jambo moja, na wao kutimiza wajibu wao hasa kwenye suala la malipo ni swala lingine. Waulize Tanesco

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwa heshima na taadhima nakuomba timiza masharti yote waliokuwekea madaktari wa hospitali za Serikali.

Uwezo tunao, zirudishe zile pesa unazopeleka kwenye yale maelewanao na Hospitali za Kanisa (MoU), na zije kuwalipa na kuwahudumia madaktari walioajiriwa Serikalini. Ni wakati muafaka kwa Kanisa kujitegemea lenyewe na si kungoja ruzuku za Serikali.

Nawasilisha.

FaizaFoxy.

Na nyie wabunge mtaokwenda kuongelea haya kesho bungeni, msisahau hili. Mhakikishe hizi pesa zinaacha kupelekwa hospitali za makanisa na zinarudi kusaidia madaktari walioajiriwa Serikalini, wanazihitaji zaidi huku. Makanisa wataletewa zao kutoka Vatikan.
 
Hahahahah FF .................mie nlipenda kweli kuona serikali yako tukufu ikisimamia kidole gumba kwenye vitisho vyake. Wewe unawashauri vizuri watimize masharti wakati Mh. Pinda keshakiri kuwa madai ya madaktari hayatimiziki na serikali yoyote ile duniani na takwimu akatoa sas ni madai gani unashauri wayatimize??

Sio kuwa ndo style ya kubali yaishe???
 
Kwani hospitali za kanisa ni ngapi nchi hii na je embu nipe kadirio la kiasi gani mou wanapata ukilinganisha na mabilioni yanayohitajika kuongezwa kutoka hotuba ya mtoto wa mkulima?tatu unafikiri kuondoa hizo hela kutakuwa na athari zozote kwenye hizo hospitali?tatu ulishawahi kufanya uchunguzi za sadaka za makanisa?nne madam embu kuwa mkweli hospitali ngapi za serikali zina hadhi ya hospitali za kanisa?ni hayo tu kwa sasa.
 
hizo pesa za MOU zinalipa madaktari waliopo bugando,KCMC, na mahospitali mengi ya DDH ambayo ni ya kanisa.wote wamegoma.jielimishe ff.halafu rudi kwenye ile thread yetu tujadili.
 
Back
Top Bottom