Guyton
JF-Expert Member
- Jan 15, 2011
- 264
- 78
Hapa ndipo madaktari wanapokosea kama mtizamo wao ndio huu wa Zimmerman. Hapa unachotafuta ni Daktari awe na mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine wote au maslahi yaendane na kazi? Hebu mfikirie rubani anayeongoza ndege yenye abiria 480, there is no room for error, hakuna cha kusema ati nurse alimix mafaili, one mistake half a thousand people are dead! mfikirie mtu anayetreat maji tunayotumia dar es Salaam kutoka mto Ruvu, no room for errors, mix-up of chemicals my dear the whole city is dead! Kwa hiyo hiyo arragance uliyo/mliyonayo is a grave mistake. Nchi nyingine zilizoendelea unazozitolea mifano, mishahara iko very close hamna tofauti kubwa kati ya dereva wa basi hata na daktari, wote wanatoa huduma muhimu kwa jamii. Sema mishahara inakidhi mahitaji. Madaktari wanayo baadhi ya madai ya msingi kabisa, suala la posho ni la msingi.
Kwa upande wa pili, madaktari nao wana matatizo makubwa sana na ndio maana naona baadhi ya watu wanaandika kwa hisia hapa. Nadhani kila mmoja wetu ameshatendwa in one way or another na wafanyakazi wa sekta ya afya. Na hii kwa kiasi kikubwa inatokana na arrogance waliyonayo kuwa they are the best, most important professionals, which is not true at all, kila mtu na fani yake ana umuhimu kwa jamii, you need to look it from the system perspective na sio kama units. Fani ya udaktari imeoza, purely rotten, wengi wana majina ya udaktari but ni wababaishaji wakubwa, hakuna kitu, empty headed enjoying being called with all sweet prefixes in the street, Dr, Dr! Madaktari wa leo hawana ethics, na mwili wa binadamu wanauchukulia kama wa mnyama tu, they dont care at all. Nasema wengi ni wababaishaji, lakini wapo wazuri na makini, wanaopenda kazi yao.
Mwisho, system nzima ya afya inahitaji complete overhaul, haiwezekani mgonjwa atoke Amana anafikishwa Muhimbili ati anapokelewa na Intern, ni upuuzi mtupu huu. Hospitali ya Rufaa inageuka ya kujifunzia tena? mgonjwa aliyezidiwa anaonwaje na daktari mwanafunzi kama sio uwendawazimu huu! nchi gani inafanya huu upuuzi? Hospitali za rufaa zinatakiwa 24 hours zina specialists, za kwetu ati zina interns. Akili za wapi hizi? Wagonjwa wengi naamini zaidi ya nusu wanafariki sio kwa maradhi yanayowasumbua, hapana wanakuwa mismanaged. Hili linajulikana, mara intern mara mwanafunzi wa masters mara nurse mara huyu, mpaka mtu anakata roho anafanyiwa mizaha tu.
kweli uhuru wa kulalamika unautumia vizuri kaka, mala Amana, mala intern, mala pilot, tunaposema hili ni jukwaa la greater thinker hatumaanishi kuandika text ndefu iliyojazwa na mitizamo ya hisia, next time jipange kaka.