Mgomo wa madaktari kuahirishwa leo!

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
cha madaktari kinachoendelea Don Bosco sasa hivi kimeazimia kuahirisha mgomo wa Madaktari ili kumpa muda Mh. Presidaa aweze kushughulikia madai yao kama walivyoelewana jana Ikulu.
My Take;
-Nawapongeza sana maDr kwa kuwa na busara hizo ingawaje inawezekana wakawa wamepigwa changa la macho lakini wameonyesha heshima kwa Mh. Raisi kwani kama wasingeweza kuelewana naye ingemaanisha kwamba hata Raisi sasa kazi imemshinda kama ilivyowashinda Juniors wake..BIG UP GENIOUS DRS......
-Ieleweke kwamba UMEAHIRISHWA, Sio kwamba UMEISHA

TAARIFA RASMI YA MAT
[h=6]RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)[/h]
 
Zawadi za vyeo anazotoa zitamgharimu sana JK. Wanaoweza kudeliver kazi ni wengi lakini macho yake yanatandwa na ukungu wa takrima kwa wanaojiweka vimbelembele. Ataelewa baada ya 2015 kwamba nani hasa alikuwa rafiki mwema kwake na nani ni migulumbaja wake.
 
Kwi kwi kwi teh teh teh, Gahwa kwa juisi ya tende imefanya kazi. Yale yale ya kina nanihii!

Nilisema humu.
 
cha madaktari kinachoendelea Don Bosco sasa hivi kimeazimia kuahirisha mgomo wa Madaktari ili kumpa muda Mh. Presidaa aweze kushughulikia madai yao kama walivyoelewana jana Ikulu.
My Take;
-Nawapongeza sana maDr kwa kuwa na busara hizo ingawaje inawezekana wakawa wamepigwa changa la macho lakini wameonyesha heshima kwa Mh. Raisi kwani kama wasingeweza kuelewana naye ingemaanisha kwamba hata Raisi sasa kazi imemshinda kama ilivyowashinda Juniors wake..BIG UP GENIOUS DRS......
-Ieleweke kwamba UMEAHIRISHWA, Sio kwamba UMEISHA

Doctors hongereeni sana sana sana tena sana. Nawapenda na kuwaheshi kwa jinsi mlivyokuwa Strategic. Suala lenu mmeendalo kwa ngazi husika, moja baada ya nyingine, tena kwa ustarabu wa hali ya juu kabisa. Ngazi moja ikishindwa, mnakwenda inayofuata, nayo ikishindwa mnakwenda inayofuata, mpaka mmefika ngazi ya juu kabisa ya maamuzi. Kwa hakika kuna vitu vichache watanzania wote inabidi tujifunze kwa sakata hili;

1. Kumbe watendaji wengi ktk idara na wizara mabalimbali za Serikali hawewezi kuwajibika na kutatua kero na matatizo yanayowakabli wananchi mpaka yafike ngazi ya juu kabisa. Sakata hili la Madaktari linatufundisha,

2. Kumbe tuna watendaji wengi ambao ni wababaishaji na ndio maana mambo mengi hayaendi hapa Tanzania, na kumbe kuna haja ya kufanya overhaul ya watendaji wa serikali kama tukitaka kuendelea kutokana na umangimeza, ulafi, ubinafsi na kutokuwajibika kwa watendaji waliopo,

3. Kufika kwa Mh. Rais na kukubali kumpa muda wa kufanyia kazi masuala yao, ni heshima kubwa waliompa Kiongozi wa Nchi kwamba tegemeo lao kwa sasa ni yeye tu. Lakini pia linatoa tahadhari kwake kuwa, kama naye atashindwa na kuleta siasa kama za wasaidizi wake, basi mambo yataendelea kama kawa.....

Madaktari hongereni sana na tena sana kwa mara nyingine, kama ni ujumbe umefika, na kwa mantiki hiyo, masuala yenu hakuna anayeweza kudeal nayo kuanzia wizara ya Afya, Ofisi ya waziri Mkuu wote wameshindwa na kutakiwa kufanyiwa kazi na IKULU. Ikiwa kama sector nyingi zipo hivyo na kila kitu kiende Ikulu, sasa kuna sababu gani ya kuendelea kuwa na wafujaji wa maliasili za watanzani humo maofisini bila kuwawajibisha.

Mh. Rais, bila shaka amepata ukweli kuhusu watendaji wako na uwezo wao; Kama ilivyokuwa kwa suala la KATIBA pale Bungeni na Mazungumzo yake na Vyama vya Siasa pale IKULU.

Somo hili limetulia sana! Lakini nadhani bila shaka Mkulu naye mtakuwa mmempa dose yake 3x3 kwa wiki mbili au kwa mwezi, nikiwa na maana mmempa time frame.
 
Kama mgomo umehairishwa basi ni taarifa njema kwa kila mtanzania,cha msingi Rais akubali na aheshimu makubaliano
 
katika harakati zozote ni vizuri kuwa tactical ... ku-retreat kidogo kwa kumpa nafasi mkuu ku-play his part ni tactic nzuri ambayo inaonyesha a high level of maturity na matumizi mazuri ya busara
 
JK akitekeleza madai yenu atakuwa amewaheshimu sana. Huyu mkuu wetu ana sifa moja kubwa ya kutotekeleza maamuzi magumu. Changa la macho hilo. Ushauri wangu kwenu maDr,s rudini kazini ili muokoe maisha ya waTZ wanaowategemea. mkuu akisafiri tena nje ya nnchi anaweza kuwaombea msaada wa vitendea kazi mnavyovidai, ila suala la mawaziri wa afya kuondolewa hiyo msahau.
 
nilielezea kwa undani kabisa katika post yangu "SIRI NZITO:.........", mod wakaifuta, lakini ndio yale yale yametokea.
 
Mimi naomba nukuu ya makubaliano ya kwanza baina ya madaktari na Pinda nione kama kweli Pinda aliwaahidi kuwaachisha kazi Mponda na Nkya.. Pinda anadai hapakuwepo na makubaliano hayo haya ni madai mapya kabisa, sasa isiwe hadithi ile ile ya kwanza walianza na Posho, tuliposema sana wakageuza madai na kuwa mazingira ya kufanyia kazi, Pinda alipotaka kukutana nao wakajataa wakisema hawawezi kwenda Karimjee ila Pinda awafuate wao Starlight, Haya wakutane Jumamosi wakasema ni siku ya Ibada kwao watakutana naye Jumatatu, tukasema mbona huenda kazini Jumamosi na Jumapili wakasema ooh hapana wanasubiri wajumbe wengine kutoka Bara.. haya Leo tena tunazidi kukata masiku ingawa mazungumzo yangeweza kuendelea huku mgomo wao ukiwa palepale - hawataki hadi Mponda na Nkya wajiuzuru... yaani hii sinema ya hostage taking inanoga kweli kweli utampenda kati ya The good, The bad and The Ugly - chaguo lako!
 
Nafikiri J.K anachofanya ni kuvuta muda na kuùnja baraza la mawaziri na kuwaweka pembeni kina Mponda au kuwahamishia wizara nyingine!
 
katika harakati zozote ni vizuri kuwa tactical ... ku-retreat kidogo kwa kumpa nafasi mkuu ku-play his part ni tactic nzuri ambayo inaonyesha a high level of maturity na matumizi mazuri ya busara

Sahihi kabisa mkuu,kuna wimbo moja wa Bob Marley,'half running away" alizungumzia hii,kwamba mtu anayepigana na kurudi nyuma anajiweka ktk mazingira ya kuendelea kupigana na kesho kwa mbinu mpya. Madaktari wako sahihi,kule tu kukutana na Presidaa kuelezea hali halisi its a good move nae kuelewa tatizo hasa incase wawakilishi/washauri wake walikuwa wanalifikisha in other way. Besides,,ni rais wa nchi,pamoja na yote akikuomba jambo utakataa vp? hata kama inauma lazima umpe muda,lengo ni kuleta maelewano
 
Tumehairisha mgomo ili kumpa Muda Mh Raisi Dr Jakaya Kikwete kushughulikia madai yetu,kiufupi hatuwezi kumlazimisha tukiheshimu mamlaka yake ametuelewa na leo rasmi,tunanyanyua vifaa tunarudi kazini.
Tunaamini anania ya dhati ya kuboresha afya za watanzania,sio kama mr mamba aliyetudanya pale cpl.
Mungu ibariki Tanzania
 
Hongereni sana Ma Docs na hongera rais kwa kujali maisha ya watanzania,
angalizo, mliyokubaliana myatekeleze hatutaki tena kusikia porojo za aina ya Pinda.
 
heshima kwa rais!!Tumeiona
heshima kwa wananchi!!Tumeiona

haya sasa serikali ina muda mwingine tena{mara ya tatu} kushughulikia mgomo huu.
isije ikapita miezi mitatu tukaingia kwenye mgomo mwingine wa madaktari tukaanza kulalamika.
 
Mimi naomba nukuu ya makubaliano ya kwanza baina ya madaktari na Pinda nione kama kweli Pinda aliwaahidi kuwaachisha kazi Mponda na Nkya.. Pinda anadai hapakuwepo na makubaliano hayo haya ni madai mapya kabisa, sasa isiwe hadithi ile ile ya kwanza walianza na Posho, tuliposema sana wakageuza madai na kuwa mazingira ya kufanyia kazi, Pinda alipotaka kukutana nao wakajataa wakisema hawawezi kwenda Karimjee ila Pinda awafuate wao Starlight, Haya wakutane Jumamosi wakasema ni siku ya Ibada kwao watakutana naye Jumatatu, tukasema mbona huenda kazini Jumamosi na Jumapili wakasema ooh hapana wanasubiri wajumbe wengine kutoka Bara.. haya Leo tena tunazidi kukata masiku ingawa mazungumzo yangeweza kuendelea huku mgomo wao ukiwa palepale - hawataki hadi Mponda na Nkya wajiuzuru... yaani hii sinema ya hostage taking inanoga kweli kweli utampenda kati ya The good, The bad and The Ugly - chaguo lako!

Hii ni miongoni mwa posts zako chache sana ambayo sjailewa mkuu. Hujui kwamba Mizengo kwa sasa ndiye mrithi halali wa Makamba snr, aliyekuwa na uwezo wa kusema jambo flani leo na kesho tu atadai hakusema hvyo. Huitaji Phd kujua nani alisimamia ukweli baina ya PM na Drs. Siye pinda huyu huyu aliyekaribia kulia issue ya Jairo hali ya kuwa ameshasaini yale mambo!
 
Back
Top Bottom