Mgomo wa madaktari: Kigwangwalla kufukuzwa CCM?

ni mzuri sema ajapata support nzuri na ukizingatia amekaa na wazee pale muda mwingine anaogopa kujibishana nao aje tu chadema tutampokea na kumrudisha agombee nzega na jimbo atalichukua aina shida
 
Eheeee, Nani? Hawa Ghasia! Kweli yeye ni gasia. Kama Kigangwala hakufunzwa na wazazi wake na akapigania haki za wanyonge, yeye Hawa Ghasia kavunzwa na nani kusimamia upupu unaofanywa na genge lake dhidi ya wanyonge? Japokua umbea ni kazi ya wanawake lakini wa Hawa umepitiliza mazee.
 
Tatizo Moja la Dogo Kigangwala ni kambwa amezidi ushamba wa akili. Utakuaje CCM alafu utetee maslai ya wanyonge? Haya sio mahesabu ya trigonometric kiasi ya kushindwa kujua kuwa alipaswa kuwa CDM ili afunguke anavyotaka. Tafadhali usichelewe hiyo kesho kufanya uamuzi wa mada wa kuichana kadi ya magamba hadharani!
 
Huyu mkw.er.e asipougua mipresha na mi BP haugui tena mpaka siku ya mwisho,vijana wake alowachomeka ndo wanaibananisha serkali yake kinoma!,check January,kigwangwala,benno malisa na jussa!!!
 
hiyo habari siwezi kuishangaa kwani hao waliomshambulia Hamis wanajulikana kwa utendaji wao mbovu uliopelekea serikali yote ya JK kudharauliwa hivyo wamebaki kujikweza kwa mabosi wao ili wapate huruma
 
Mh. Daktari siyo mnafiki Kama wao, wanafanya uozo wanategemea watetewe hakuna hapo... VITA MBELE.
 
Huyo Adam malima ache kumchamba mwenzake ,atuambie yeye amerudisha lini na wapi kadi ya NRA.....

Atuambie ....mbona bado yupo kwenye payroll ya MAnji ,bosi wake wa zamani....na amewekwa pale Nishati ...ili kusimamia tendaaa zakinyonyiji za kampuni za manji ....Tanesco ambako wanamlipa manji kwa dola na pound pamoja na kuwa local company ....
 
Pambana dr mpaka aki ipatikane,unachofanya unajiondolea dhamb kwa Mungu dhamb ya unafiki ndan ya ccm
 
Wanabodi, hii imetoka jikoni kabisa:

Baada yake alikuja Mhe. Hawa Ghasia ambaye alimtukana Kingwangallah kuwa ni mbishi, jeuri na hakufunzwa na wazazi wake na kwamba CCM hawatomuweza.................

kama ni kweli ina maana Hawa ghasia naona anashindwa kutofautsha Vikoa vya Siasa na Vikao vya familia. Kuna watu wanataka heshima na mama na mwana hata kama wako mjeongoni kisa tu wamewazidi umri vijana.
 
Kama alikaa kimya pasi kuwajibu ni ishara njema kuwa alikubali kosa,kwa chama chake,hata mimi binafsi nakubliana na hukumu ya CCM dhidi yake,kwa kuwa yu mwanachama wa CCM,lakini kwa chama chake kilipofika HK anastahki hongera na sifa ya kusimamia maslahi ya Taifa na si maslahi ya chama chake.Basi kwa kuwa ndani ya chama chake hakuna watetezi wa Taifa ukimya wake kwa tafsiri ya waliokuwa wakimshambulia ni kukubali kuwa yuko pekee yake kusimamia mahitaji na maslahi ya Watanzania.Hivyo kwa lolote litakalo tokea apokee heshima ya kuvuliwa uwanachama na ubunge wa CCM kwa niaba ya Taifa.Kwa kizazi chake awezi kulingana uwezo wa kufikilia wa wazee ambao ni lika la mama zake ndani ya vikao vya CCM,ambao walifundishwa kuwa hakuna Taifa pasipo CCM na kuwa watiifu hata kwa upumbavu ulio dhahiri machoni pa Taifa.

Ila kwa jinsi JK alivyo mjanja anajua sana kuwa watu walio ndani ya ya CCM ni aina gani ya watu,watu wasitalajie kuwa atapokea ushauri wa kukubali kijana huyo kufukuzwa CCM kwa kuwa itakuwa ndio mwanzo wa CCM kukaribisha msiba wake,kwa kuanza na laana ya kijana huyo ndani ya chama hicho.Kwa kuwa ni kwa kukulupuka huko kwa washupaliaji wa upupu huo ndio kulikopelekea maamuzi ya kuwa NAPE afukuzwe chama wakati ule wa uchaguzi wa kinyanganyilo cha umoja wa vijana na jengo la umoja wa vijana.Kwa picha ile JK aliona mbele leo hii Nape ndie mtu pekee anaeongea lugha moja na umma wa Tanzania nje ya kundi kubwa la Wanaccm ambao wananchi wanawaona kama watu walafi wa kupindukia wachache wenye kulihujumu Taifa chinii ya kivuli cha chama Tawala.

Hivyo wale wanofikili ndani ya CCM kuwa watamfukuza HK hawatamfukuza kwa kuwa JK anajua anawaitaji watu aina ya HK kwa sana,kuliko kundi la hao wanaomsurubu kijana huyo HK.Kwa kuwa ni heri ya kuwa na HK mmoja kuliko kuwa na kundi la Mawazili kumi wa baraza la JK na wabunge mia kwa tiketi ya CCM.Kwa kuwa watu aina ya HK ndio watakao simama mbele ya hadhara na kusema pasipo woga kuwa nao kwa tiketi ya CCM walipigana vita ya ufisadi, siku CCM watakapo kuwa waksulubiwa na umma kwa kukumbatia ufisadi na maovu mengine dhidi ya umma.
 
Hakuna wa kumfukuza kwani wote wamechafuka. Hata wakimfukuza aende tu mahakamani, atadunda mpaka 2015, kwani serikali haina pesa ya kuendeshea uchaguzi kwasasa.
 
Back
Top Bottom