Mgomo wa Madaktari: Kigwangalla asema 'Sihusiki!', kuchukua hatua za kisheria dhidi ya media

chikakatata

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
220
98
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari: Dkt. Hamisi Kigwangalla Akanusha Kuutaka Uwaziri


Thursday, March 8, 2012

OFISI YA MBUNGE, JIMBO LA NZEGA


Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (MB)



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tunapenda kuutarifu umma kwamba Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesikitishwa sana kupata taarifa kutoka baadhi ya vyombo vya habari kuwa anatajwa kuchochea mgomo wa madaktari. Hata siku moja hajawahi kuwa mchochezi wa mgomo huu na yeye binafsi siku zote amekuwa mstari wa mbele kusema ukweli na kuweka hadharani msimamo wake na wala siyo kuchochea kwa kificho chini kwa chini.

Pia kuna gazeti moja la kila wiki limeandika jana stori (kwenye ukurasa wake wa mbele) kuwa Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla ‘anatajwa kuchochea mgomo huo kwa malengo ya kuutaka uwaziri.' Vyombo vingi vya habari vikivutiwa na kichwa hiki cha habari vimekuwa vikimpigia simu Mhe. Mbunge kumtaka atoe ufafanuzi. Mhe. Mbunge amesikitishwa sana na taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti hili na tayari Mwanasheria wake ameanza kujipanga kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulitaka gazeti hili limsafishe kwenye jamii kwa kuchapisha habari ya kumsafisha ama lipelekwe mahakamani.

Kwa taarifa hii tunakanusha ushiriki wa aina yoyote ile unaotajwa kumhusisha Mbunge wa Nzega kwenye uchochezi ama wa namna yoyote ile inayofikirika zaidi ya msimamo ambao Mhe. Mbunge Dkt. Kigwangalla amewahi kuuweka wazi siku za nyuma kwenye mikutano ya wazi ya madaktari au kwenye vyombo vya habari.

Pia ifahamike kuwa kwa kuweka wazi msimamo wake kwamba madaktari wana madai ya msingi na hivyo wasikilizwe (ambayo kwa sasa serikali ilishakiri na kuyakubali madai yao na kutamka hadharani kuwa inayafanyia kazi) haimaanishi kuwa ni uchochezi bali ni matumizi ya haki za msingi za binadamu kama zilivyoainishwa kwenye Kati ba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwenye mikataba mbali mbali ya kimataifa ya haki za binadam.


Na pia tunapenda kuwataarifu wanahabari kuwa Dkt. Hamisi Kigwangalla hajahudhuria mkutano wowote ule wa madaktari uliopelekea madaktari kuazimia kugoma tena na hivyo kumhusisha na ushawishi ama uchochezi ni kupotosha umma na kuvunja sheria.

Na zaidi kufikiria kuwa madaktari nchi nzima wanaweza kugoma kwa kumsikiliza mtu mmoja tu ni kuwatukana na kuwadhalilisha kwa kuwaona hawana uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi yao, ilhali hawa ni watu makini, wenye elimu na ujuzi wa hali ya juu na wengi wao wanamshinda elimu, ujuzi na uzoefu kwa mbali sana Mhe. Mbunge Dkt. Kigwangalla.

Hali kadhalika, Mhe. Dkt. Kigwangalla aliomba Ubunge na hakutarajia kuwa angepewa Uwaziri na ni wazo la kitoto kufikiria kwamba mtu mwenye busara zake na hadhi yake kama yeye angeweza kupanga mkakati wa kumn'goa Waziri yeyote Yule ili awekwe yeye, maana kwanza hana muamana na mamlaka ya uteuzi, ambayo kimsingi ndiyo yenye uamuzi wa kumteua nani na kumuondoa nani, na pia haiyumkiniki kuwa eti ‘uwe mstari wa mbele kuvumbua maovu na mapungufu ya kiutendaji ya mtu ambaye unataka atolewe kwenye nafasi ili wewe uwekwe hapo!'

Kwa namna yoyote ile kama Dkt. Kigwangalla angekuwa anaitaka nafasi ya Uwaziri asingeunga mkono madai ya madaktari. Na kwamba kama kuna mtu ana Taarifa zozote zile zinazoweza kuthibitisha kuwa amekuwa akipanga mikakati ya kutafuta Uwaziri basi aziweke wazi na Mhe. Mbunge atakuwa tayari kujivua nafasi zake zote za uongozi alizonazo.


Mhe. Mbunge anawashauri waandishi wa habari kuwa waandike taarifa ambazo wana uhakika nazo tu na wasikubali kutumiwa na makundi ya wana siasa wenye malengo ya kuchafua wenzao.

Mwisho, mara zote toka mgogoro huu baina ya madaktari na serikali uanze, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) amekuwa akishauri pande zote mbili zikutane, zijadiliane na kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo, na leo hii tena bado anasisitiza kuwa njia pekee sahihi na sawia ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu ni kuzungumza na kuelewana kwenye mambo ya msingi. Hii ndiyo njia pekee itakayoepusha adha kwa wananchi wanaohitaji huduma za afya, ambao wao ni waathirika wasio na hatia.


Imetolewa Leo Tar 8/Machi/2012 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega.
a

 
Mh!!!!hamis andrea!!!!!!haya bwana!!!!!!pengine kwa sababu kizazi kinachoendesha mambo yote haya ni kizazi chenu cha muhimbili kilichomaliza undergraduate 2000-2005,na hata kama hauutaki nina hakika ndoto hizo unazo!!from shy bush to muhas,to nzega mp,ni mtu uliye na ndoto za kupanda juu siku zote!!!!
 
Mwanzo ilikuwa bwana (Dr.) Ulimboka, sasa naona wanarukia kwa Dr Kingwangalla kuwa ndio anachochea mgomo wa madaktari! Ni lini wataacha kutafuta visingizio?

Dr. Kingwangalla wala usipoteze muda wako kuchukua hatua za kisheria, umeshatoa hii press release inatosha kabisa. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayemaini eti mgomo wa madaktrari umechochewa na mtu mmoja!
 
Ulimboka amehojiwa leo magic,yupo mafichoni.bwana kigwa kwa hili huchomoki coz ulikuwa ukisuport ule wa kwanza mpaka coucus ya chama chako ikakupiga mkwara.HAPA USI2ZINGUE BW SAIDI BAGAILE.nadhani bashe anakupa homa izi
 
kwa kuchafua watu pumbafu zenu nyie,mlishindwa kwa ulimboka ss mmehamia kwingine ili kupooza soo
 
Kwani huyo Bagaile a.k.a Hamis Kigwangala yuko Chadema? Maana wakubwa wanasema Chadema ndiyo wanaochochea huu mgomo.Ama kweli mfa maji haishi kutapatapa, yaani Serikali ya CCM inatafuta mchawi kila uchao.
 
No offense lakini, Unamfahamu huyu jamaa vizuri au unamsikia tu! Nisiseme zaidi

Dr. Hamis hawezi kuona ajabu ya maneno haya kwani yanatoka kwa msomali Bashe a. k.a. Al shabaab!!
 
"ifahamike kuwa kwa kuweka wazi msimamo wake kwamba madaktari wana madai ya msingi na hivyo wasikilizwe (ambayo kwa sasa serikali ilishakiri na kuyakubali madai yao na kutamka hadharani kuwa inayafanyia kazi) haimaanishi kuwa ni uchochezi bali ni matumizi ya haki za msingi za binadamu kama zilivyoainishwa kwenye Kati ba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwenye mikataba mbali mbali ya kimataifa ya haki za binadam. "
 
Kwani huyo Bagaile a.k.a Hamis Kigwangala yuko Chadema? Maana wakubwa wanasema Chadema ndiyo wanaochochea huu mgomo.Ama kweli mfa maji haishi kutapatapa, yaani Serikali ya CCM inatafuta mchawi kila uchao.

Mkuu hv kwanini mnamuita Said Bagaille
 
Back
Top Bottom