Mgomo wa Madaktari: KCMC kufungwa kesho

sioni umuhimu wa kusubiri kamati ya bunge kuendelea kukusanya taarifa wakati watu wanakufa,mwisho wa siku mwenye maamuzi ni serikali kwa nini uamuzi huo usifanywe sasa?fire all those who are responsible!
Makinda anasema kushughulikia suala hili kunahitaji utulivu,mimi nasema linahitaji uharaka na dharura kwa serikali kutoa maamuzi.
 
...sasa wodi tufugie kuku!
Hali ni mbaya, serikali badala ya kutumia akili wanatumia nguvu. Kweli alieshiba hamjui mwenye njaa.
 
YAP, naona saa ya ukombozi imekaribia. Suala la mapinduzi huwa halichagui. Watakaopoteza maisha tuwaombee maisha mema na wasamehewe makosa yao lakini huenda ikawa ndio mwanzo wa Tanzania mpya kwa vizazi vijavyo. Salamu kwa viongozi wa CWT ambao wanakurupuka na kukubali kuyumbishwa kitoto. Siku moja kabla hawajatangaza mgomo wanachama wao watakuwa tayari wameweka "chaki zao chini" Endeleeni madaktari. Tuko nyuma yenu. Tukiona watanzania wengi wagonjwa wanapotea basi wananchi hatutakuwa na uamuzi zaidi ya kuingia barabarani, hapo tutabadili historia yetu.
 
my God. Mungu Tanzania tunasubiri kudra zako maana serikali tulioambiwa imetoka kwako sasa imeshindwa na hali unaiona . Tunakuomba uwapokee hao wanaokuja sasa kutokana na mgomo wa madaktari maana siku zao zilikuwa bbado ila serikali yao ndio imeamua wafe. Amen
 
Mleta huu uzi ulitakiwa usubiri kesho wakishagoma ndiyo utuambie, la sivyo hii ipeleke jukwaa la tetesi!
 
Nchi yangu Tanzania nakupenda kwa roho....ndo tugawane sasa wengine mishahara mikubwa wanasinzia tu madr wameamua
 
Ngoja wafe wee badae watajua mchawi wa wafu ni nani ndo wafanye maamuzi magumu.
 
Hivi hii serikali...
Sasa ni serikali gani isiyokuwa na empathy na raia wake? Kweli tuirudishe serikali ya chama hiki itakapotimu 2015....?

Jamani,nini tena unachotaka uambiwe..wakati unaona kabisa kwa macho yako...
 
kama tungewapa fursa ya kwanza wagonjwa waliolazwa hospitalini wengi wao wasingeongea kama sisi hapa.
 
Back
Top Bottom