MGOMO wa MADAKTARI kama penati ya PIRLO....

Tusishabikie ,tutafute ufumbuzi jamani wagonjwa nao wana haki ya kutibiwa ipasavyo ikilinganisha serekali inatoa vitendea kazi na madaktari wanatumia pamoja na ujuzi walioupata darasani na uzoefu.

Hakuna ushabiki mgomo upo; serikali legelege inayoongozwa na rais dhaifu inatumia mikakati dhaifu kupambana na madaktari wa ukweli. Wananchi wanaumia lakini si kama wanavyoumizwa na serikali.

Ukisikia watu wanatumika kama ngao, ndiyo hiyo serikali ya kipuuzi inaweka binadamu wenye shida (wagonjwa) kujikinga na madai ya madaktari. Funguka wewe UKWELI UTAKUWEKA HURU DAIMA serikali yako dhaifu inaongozwa na watu dhaifu wanaowakilishwa na chama cha kipuuzi
 
FFU ndio wanatibu?

Serikali inakuza tu mambo bila sababu. Mbona safari za rais zisiahirishwe vifaa vya hosipitalini vikanunuliwa? Za kulipa IPTL zinatoka wapi? Huko Kiwira je? Kama vipi wauze Twiga na Tembo kama hawana hela
 
Dah hapa bugando wanaofanya kazi ni wanafunzi wa mwaka wa 3, ndo wapo mawodini, wanapita tu! mambo yamekuwa magumu hapa bugando!
 
kazi ipo wananchi tuamke tuitake serikali yetu iwasikilize madaktari la sivyo tutazidi kuumia. mwenye jukumu la kulinda afya za raia si madaktari ila ni serikali kwan i dr ni mdau tu. shame on this weak n deaf govt.2015 tuiwajibishe kwny ballot box.
 
Kama wanaona wabunge wanafaidi wakaingie kwenye siasa,kwani si wapo kule ma dr, wakilipwa na sisi walimu hatukubali!
 
Taratibu ila wenye madhara makubwa.Madaktari wanagoma kwa aina ya kipekee.Muhimbili,Bugando,KCMC na kwingineko ni balaa.Huduma zimedorora.Watu wanataabika.Serikali yalazimisha mijadala isiyo na faida.

Mgomo huu wa Madaktari wetu naufananisha na penati ya tatu ya timu ya Taifa ya Italia jana iliyopigwa na Andrea Pirlo.Mgomo umepangwa kiufundi.Hauna mshindo mkuu ila unatekelezeka.Unapoteza kabisa Serikali maboya.Serikali haijui namna ya kuuzuia.Pirlo alimpoteza Joe Hart jana,Madaktari wakioongozwa na Ulimboka wanaipoteza maboya Serikali...
bonge la penalty,penalty ya kiufundi joe hart uleeee
 
Idadi kubwa ya askari wa FFU mchana huu wamejazana hospitali ya Muhumbili, kutekeleza amri ya mahakama ya kazi.
Hao FFU watachoka tu na kisha watarudi makambini na mabomu yao ya machozi maana huo ni mgomo na wala sio maandamano.
 
Siku zote mtanzania wa kawaida ndiye anayekuwa jamvi!! Poor Tanzanians!! Ndugu zetu watakufa sana na serikali haijali!! Chonde chonde madaktari watanzania hawana kosa!! Waoneeni huruma tafadhali!! Sio wao!!!!
 
Rais alipoongea nao aliwakataza wasigome tena. Hatua gani inapaswa kufuatia?
 
Back
Top Bottom