MGOMO wa MADAKTARI kama penati ya PIRLO....

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Taratibu ila wenye madhara makubwa.Madaktari wanagoma kwa aina ya kipekee.Muhimbili,Bugando,KCMC na kwingineko ni balaa.Huduma zimedorora.Watu wanataabika.Serikali yalazimisha mijadala isiyo na faida.

Mgomo huu wa Madaktari wetu naufananisha na penati ya tatu ya timu ya Taifa ya Italia jana iliyopigwa na Andrea Pirlo.Mgomo umepangwa kiufundi.Hauna mshindo mkuu ila unatekelezeka.Unapoteza kabisa Serikali maboya.Serikali haijui namna ya kuuzuia.Pirlo alimpoteza Joe Hart jana,Madaktari wakioongozwa na Ulimboka wanaipoteza maboya Serikali...
 
Serekali haioni mbali,wanafikiri wanaweza pata madaktari wa fastafasta kama ilivyokua kwa walimu wa kata.wanafikiri kutumia masaburi.hiyo ni taaluma nyeti na yakuheshimika duniani kote,udaktari na ualimu chakushangaza hapa kwetu siasa ndio sekta ya kuheshimika ingawa ndio wanaoongoza kwa madudu na haya yote yanayoendelea sasahivi.
 
Tusishabikie ,tutafute ufumbuzi jamani wagonjwa nao wana haki ya kutibiwa ipasavyo ikilinganisha serekali inatoa vitendea kazi na madaktari wanatumia pamoja na ujuzi walioupata darasani na uzoefu.
 
nipo bugando hali ni mbaya! jamaa wametoka kwenye kikao wamekubaliana kugoma, npo na mgonjwa ila wangu imebidi nisaidiwe na washikaji madaktari niliosoma nao! c utani hali ni mbaya, kama hauamin fika ujinee
 
Naelekea hapo, ila siumwi. Kuna jirani yangu anaumwa ameomba tumuhamishie hospitali nyingine, andadai kuna rasharasha za mgomo!
 
Madhara ni kwa Mtanzania! Tusishabikie na kufurahia kugoma! Ni vizuri kufikiri kuhusu ufumbuzi.
 
Tusishabikie ,tutafute ufumbuzi jamani wagonjwa nao wana haki ya kutibiwa ipasavyo ikilinganisha serekali inatoa vitendea kazi na madaktari wanatumia pamoja na ujuzi walioupata darasani na uzoefu.

Tuambie ufumbuzi unaoutaka wewe utafutweje na ni nani atakayeutoa. Usiwe na kigugumizi mmezoea kulaumu madaktari kila wanapoeleza ukweli halisi. Nao ni watu na wanategemewa na lundo la watu nyuma yao. Kila kitu hivi sasa kiangaliwe kwa maslahi ya wote. Serikali haiko juu ya ya haki ya mtu yeyote.
 
Tusishabikie ,tutafute ufumbuzi jamani wagonjwa nao wana haki ya kutibiwa ipasavyo ikilinganisha serekali inatoa vitendea kazi na madaktari wanatumia pamoja na ujuzi walioupata darasani na uzoefu.

...Hapo kwenye maandishi mekundu; ni vitendea kazi gani wavizungumzumia hapa? Vyumba vya madaktari havitoshi, maabara hazina madawa ya kupimia magonjwa mbalimbali, vipimo vya VVU hakuna nchi nzima, wagonjwa kulazwa chini kwa uhaba wa vitanda na magodoro, n.k hebu tufafanulie mkuu vitendea kazi gani unaviongelea ww?
 
One day everybody will come to his/her sense and take our national agendas serious. Tutafika tunapotaka kwenda
 
Tusishabikie ,tutafute ufumbuzi jamani wagonjwa nao wana haki ya kutibiwa ipasavyo ikilinganisha serekali inatoa vitendea kazi na madaktari wanatumia pamoja na ujuzi walioupata darasani na uzoefu.

Nani alikufundisha kwamba Madaktari waliingia fani hiyo kama fani ya hisani ili familia zao ziteseke wakati watawala wanatesa kwa mgongo wa fedha za walipa kodi?! watawala na familia zao wanatibiwa ulaya. India, Amerika na Afrika kusini ambako madaktari wanaheshimika kitaaluma, wana vifaa vya kutosha na mafao mazuri, hawa wa kwetu ndio wa kulinda na kutetea haki za wagonjwa na sio watawala wanaotafuna pesa za wavuja jasho! usiwe mvivu wa kusoma!! yasome vizuri madai ya madaktari, jaribu kukumbuka wameanza lini kudai haki hizo then jaribu pia kuangalia serikali imechukua hatua gani katika kipindi hicho chote. fanya utafiti kidogo wa mlinganisho katika nchi nyingine uangalie maingira ya kazi na mafao ya madaktari?! Hawa madaktari wetu sio vichaa kuamua kukinzana na serikali mwajiri wao pasipo sababu za msingi.tafakari
 
...Hapo kwenye maandishi mekundu; ni vitendea kazi gani wavizungumzumia hapa? Vyumba vya madaktari havitoshi, maabara hazina madawa ya kupimia magonjwa mbalimbali, vipimo vya VVU hakuna nchi nzima, wagonjwa kulazwa chini kwa uhaba wa vitanda na magodoro, n.k hebu tufafanulie mkuu vitendea kazi gani unaviongelea ww?

Vifaa vinavyotolewa na serikali ni CONDOMS kwa msaada wa watu wa Marekani
 
kama mishahara ya wafanyakazi wetu haitoshi na huduma muhimu za jamii zinadorora kuna umuhimu gani wa kutenga pesa kwa ajili ya kuanzisha jkt kwa mujibu wa sheria? serikali iangalie vipaumbele vya maana zaidi.
 
Tangu lini serikali yetu ikawa na vipengele vya maana??
 
Tatizo linalosumbua kizazi hiki ni ubinafsi. Kama ilivyotabiriwa kuwa Siku za mwisho, wengi watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa kuliko kumpenda Mungu. Kwa hiyo tatizo la huu mgomo ni upendaji pesa wa wanasiasa na hao madaktari.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Nahisi matumaini ya serikali kuwa tisho la mahakama lingezuia mgomo halikufikiria vizuri na inawezekana mahakama ikawa imekizuia chama cha madaktari wasigome (MAT) kumbe waliogoma ni Jumuiya ya Madaktari na Si MAT iliyozuiwa na Mahakama wasigome, Hali ni mbaya Jirani yangu kafariki jana Amana kwa kushindwa kumpeleka Muhimbili baada ya kuwa hawawezi kumhudumia aliangukiwa na ukuta wa Choo, manesi wanasema hata tukimpeleka Muhimbili hakuna huduma atafia mapokezi tunabishana nao toka saa 12.30 jioni na ilipofika saa 2. usk kafariki. bila hata kuhudumiwa,
 
Idadi kubwa ya askari wa FFU mchana huu wamejazana hospitali ya Muhumbili, kutekeleza amri ya mahakama ya kazi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom