Mgomo Wa Madaktari: Jee, Serikali Kuwafukuza Kazi Kwa Summary Dismissal kwa "Insubordination"?

  • Wakuu ebu mwenye official statemt ya madai na malamiko ya madaktari aweke hapa
  • @Pasco tumia nguvu uliyotumia kutafuta picha ya Slaa na Jk kumoba dk slaaa aje hapa atupe msimamo na kauli ya chama chake
Ndugu yangu Zing, Dr., nikutane nae wapi?, labda utokee tena msiba wa mwana jfchadema mwingine tukutane makaburini!.

Ila unaweza kumlazimisha kuzungumza kwa kumsingizia kitu kama ukipandisha thread na kudai, "Jee Mgomo wa Madaktari Unachochewa na Chadema Kama ile Migomo ya vyuo Vikuu?" au unaweza kuamua kumlisha Dr nanii maneno ili kumlazimisha kuyatema kama

" Kufuatia serikali kuwadharau madaktari. Dr. so and so ameapa Kuongoza Maandamano ya Watanzania Wote kuitwaa ile haki yake aliopokwa hivyo kuingia Ikulu moja kwa moja!. Amshauri ninii abakie uhamishoni huko huko alipo na asithubutu kukanyaga tena Tz"!. ukimlisha maneno kama hayo, fasta ataibuka kuyatema!.
 
I can see the starting of Tahrir square because teachers will follow suit and that will be the end of this government.
.
Mkuu Mween, huu ni uchochezi!. Angalia usimponze Max!. Waalimu nawaombeni sana msimsikilize Mween, nyie sio kama madaktari, kwa sababu nyinyi walimu kazi yenu ni humble job!, siyo kazi ya migomo kwa sababu hata mkigoma, it won't make any diference because you don't save life, no one will die!.
 
Wanabodi,
Hili ni opinion question yangu kuwa jee, serikali inajipanga kuwafukuza kazi madaktari wote waliogoma kwa 'summary dismissal" kwa kutumia kipengele cha "insubordination"?. Lengo likiwa ni kuzuia mgomo huu usisambae nchi nzima hivyo ku paralyse sekta nzima ya Tanzania?.

5. Wakati ninaandika opinion hii, serikali tayari imeshawaandikia barua madfaktari wote wastaafu ambao ni able, kurejea kazini kwa dharura!, madaktari wote wa jeshi wamemepawa amri ya stand by, kuwa tayari kufanya kazi masaa 18!.
6. Mpango huo wa kuwafukuza kazi kwa "summary dismissal",kwa kutumia kifungu cha "insubordination" utawanyima haki zao zote, ukiondoa michango yao tuu waliyokatwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii!.
7. Taarifa za mpango huo wa serikali zimetumwa mjini Davos nchini Uswisi kupata baraka za mkuu nchi, na kuna uwezekano kabla ya utekelezaji wa uamuzi huu, rais Jakaya Kikwete, ataikatiza ziara yake ya nchini Uswisi na kurejea nyumbani over the weekend ambapo kabla ya kumalizika altimatum hiyo, Rais Kikwete atalihutubia taifa kwa mtindo ule wa kuuzuia ule mgomo wa wafanyakazi!.
8. Kitendo cha mtumishi wa serikali, kukataa kutekeleza amri halali ya mkuu wake wa kazi, hiyo ni insubordination na adhabu yake ni summary dismissal!. Hivyo pamoja na genuinity yote ya madai ya madaktari, jee mgomo wao ni halali?, unafuata sheria za migomo kwa mujibu wa sheria zetu za kazi na maadili ya kidakitari?!.

Wasalaam

Pasco (wa jf)

Ni vizuri sana umekuja ni hili wazo ambapo hii serikali yenye kumbukumbu mbovu itakuwa imesahau. Katika kipindi cha mwanza cha JK madaktari waligoma wa muhimbili. Serikali wakati huo ikionekana kama makini ili amua kuwafukuza lakini ilipojaribu tu hivyo na wauguzi wakaweka vyombo chini na uwezekano wa kusambaa ulikuwa mkubwa. Hatimaye serikali ilikubali kila kitu kilichodaiwa.

Sasa sote tunajua hii ni serikali legelege, haina mgogo au ubavu. Blandina Nyoni na Dr Mutasiwa wanaweza kushauri hilo kwa vile wamekataliwa. Na kama wataendelea kuwa wizarani nadhani mgomo hautaisha, kwao lolote liwe na hivyo watatamani wao wabaki kwa gharama yoyote hata ikibidi kutumia majeshi.

Kipindi hiki kwa uasisis wa BW Mkapa matabaka yaliundwa ikiwa ni pamoja na tabaka linalotambulika kama watumishi wa Afya Human Resource for Health. Japo hawa hawana mshikamano lakini sasa itabidi kushirikiana, siku zote watu hushirikiana natika matatizo.

Serikali inacheza mchezo mbaya sana, itakuja kujuta sana na siajabu wasifikie 2015. Umoja sio lazima uwe wa mawaziri au wa sisiemu au wa serikali kulazimisha Nyoni na Mtasiwa wabaki. Safari hii serikali imeshika pabaya, ninafuu wakubali yaishe sasa kuliko kushindwa na kuwaomba. Hivi hii serikali inajilipa malipo na posho kubwa kubwa wanadhani wengine hawaoni wala hawapendi.

Afya kazaneni jipeni moyo, mtashinda udhalimu huu
 
Pasco said:
3. Asubuhi hii Naibu Waziri wa Afya, Dr. Lucy Nkya, ametangaza serikali haiwezi kuwafuata madaktari hapo walipo kwa kwa sababu hawana uhakika na usalama wa eneo hilo la kukutania, na kuwataka wakubali kukutania katika eneo watakalotayarishiwa na serikali
Duh! Ni usalama gani huo wanauzungumzia?
Mahali ambapo madaktari wanapaona ni salama eti serikali na dola zake wanaona si salama, hawa serikali lazima watakuwa wachawi.
 
Ma Spin-doctors wa Magamba wameanza kupima upepo.' Mkiona tunatembea na walinzi wengi mjue tumeanza kuwaibia' J. K. Nyerere. Madaktari shikilieni hapohapo, sisi wagonjwa tunawasapoti
 
hivi mbona msiba wa watu hawa hihamishi ili kutoa usalama wa viongozi? usalama na mahali pazuri ni pale palipo na mgomo wa wanao dai haki? aliye shauri hivyo akili zake zitakuwa likizo au ndio kufikiria kwa masaburi yake?
 
halafu hao alternative doctors wanao patikana kwa miaka sita ukijumlisha na wa interniship tena with Div I or II ukisha wafukuza utaenda wapi kupiga filimbi kupata alternative , hivi kweli viongzi wetu wanafikiria kwa masaburi yao?
 
Hii imenichekesha sana dah!
Mkuu, with all due respect, serikali yetu sijui vipi?

Nimeshindwa kuelewa ni kivipi serikali inaweza kuwalalamikia madaktari kuhusu usalama wa pahala watakapokutania...

Ni afadhali wangesema mahali hapo si salama kwa madaktari, wameshindwa kusema hivyo kwasababu madaktari hao wanaona hapo walipo ni salama, so kama serikali inaona haiko salama, impeleke Mwema akawalinde hao wawakilishi watakaoiwakilisha, sasa zaidi ya hapo utaacha kushangazwa?

Si uchuro huu?

Maktari hao ni watu wenye elimu ya kutosha kuweza kutambua kama usalama wao uko hatarini, wamefanya jambo la maana kukataa kwenda kwenye huo ukumbi mwingine ambao ni "salama" kwa sirkali.
 
we Pasco ngoja uugue tena ndio ujue umuhimu wa dr labda wawe wanakupeleka india maana hua wanasema binadamu ni rahisi kusahau, lakini kwa hao watawala wetu ninavyo wajua hawakawi kukutupa/kukusahau, risk and rewards zita ku-face wewe wewe mwenyewe.
 
Jamani tuache longo longo , jambo la maana ni sie tusio na kazi na kila aliye na nafasi tufike hapo walipo madaktari na tuwaunge mkono kwa lolote kama mambo ya Tunisia vile!
 
Sitashangaa kabisa ikiwa kuwa mpango huo wa serikali umepangwa hivyo. Kwani nadhani wanafikiri wapo salama sana hawa, hivi huyu Mama Nyoni anafikiri ataishi wapi? Hembu ngoja wafanya hivyo waone. nina uhakika ndio utakuwa mwisho wa serikali hii kuwa madarakani, kwani hata wanaccm wengine wataungana na vyama vyote vya siasa na wananchi wote kupinga uamuzi huo wa serikali. Lakini kwa vile hii serikali ni kiziwi, acha wafanye tu. kwani kuwapiga roba akina nyoni wala si kazi kubwa....
 
Mkuu Pasco,kwa mujibu wa taarifa ya ITV ya saa mbili usiku,ujumbe wa serikali umeamua kuwafuata Madaktari na kuongea nao,Japo PM hakwenda,na pia wauguzi wametoa siku mpaka Jumatatu (kwa mujibu ya thread moja hapa) Serikali imalize mgogoro wa Madaktari vinginevyo na wao watagoma.Unadhani bado Iron Lady atatoa summary dismissal hasa ukizingatia serikali inaelekea kusalimu amri na si madaktari?
 
Hakuna serikali itakayo wafuata? Je cha leo kilichotokea ni kipi? Amekuja waziri wao afya na timu yake bado tumemtimua na kumwomba aje waziri mkuu maana hatuna imani nao tena kwani tumewafata sana ila kwa viburi vyao vya kujiona miungu watu ndio wametufikisha huku tulipo. Wauguzi nao wanajiandaa kugoma kuanzia jtatu.
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.
 
Mkuu Pasco,kwa mujibu wa taarifa ya ITV ya saa mbili usiku,ujumbe wa serikali umeamua kuwafuata Madaktari na kuongea nao,Japo PM hakwenda,na pia wauguzi wametoa siku mpaka Jumatatu (kwa mujibu ya thread moja hapa) Serikali imalize mgogoro wa Madaktari vinginevyo na wao watagoma.Unadhani bado Iron Lady atatoa summary dismissal hasa ukizingatia serikali inaelekea kusalimu amri na si madaktari?
Nyamizi, asante kwa update, Japo sijaona news lakini serikali itakuwa imekwenda na kauli ya kuwa imeyakubali madai yao yote ni genuine hivyo kuwataka warejee kazini Jumatatu asubuhi wakati serikali ikishughulikia utekelezaji wa madai hayo!. kwa vile nia ya kuwatimua ipo watakaoendelea na mgomo bado hawatajuwa salama!.
 
Hakuna serikali itakayo wafuata? Je cha leo kilichotokea ni kipi? Amekuja waziri wao afya na timu yake bado tumemtimua na kumwomba aje waziri mkuu maana hatuna imani nao tena kwani tumewafata sana ila kwa viburi vyao vya kujiona miungu watu ndio wametufikisha huku tulipo. Wauguzi nao wanajiandaa kugoma kuanzia jtatu.
Dr. Mallaba, serikali is playing games on you!.
 
Nyamizi, asante kwa update, Japo sijaona news lakini serikali itakuwa imekwenda na kauli ya kuwa imeyakubali madai yao yote ni genuine hivyo kuwataka warejee kazini Jumatatu asubuhi wakati serikali ikishughulikia utekelezaji wa madai hayo!. kwa vile nia ya kuwatimua ipo watakaoendelea na mgomo bado hawatajuwa salama!.

Nimekupata Pasco na ni hivyo waziri alivyosema,lakini swali langu ni kwa nini serikali inaacha kushughulikia haya matatizo mapema mpaka yanafikia hapo? Hivi kweli unatatua vipi tatizo kwa kuongea na vyombo vya habari badala ya kuwaface wahusika (Madaktari) moja kwa moja?
 
Dr. Mallaba, serikali is playing games on you!.

The government will lose; kwa sababu nguvu ya serikali yoyote ile ni dola na silaha lakini nguvu ya silaha na dola haijawahi kuhakikisha serikali zote zinakuwepo! Hakuna nguvu kubwa zaidi kama ya roho ya mwanadamu isiyotii! Wakiwasukumiza madaktari kwenye kona na madaktari wakachukua uamuzi wa "live or die free" serikali haiwezi kuwalazimisha. Itawashikia bunduki kichwani kuwapeleka hospitali?
 
Ndugu yangu Zing, Dr., nikutane nae wapi?, labda utokee tena msiba wa mwana jfchadema mwingine tukutane makaburini!.

Ila unaweza kumlazimisha kuzungumza kwa kumsingizia kitu kama ukipandisha thread na kudai, "Jee Mgomo wa Madaktari Unachochewa na Chadema Kama ile Migomo ya vyuo Vikuu?" au unaweza kuamua kumlisha Dr nanii maneno ili kumlazimisha kuyatema kama

" Kufuatia serikali kuwadharau madaktari. Dr. so and so ameapa Kuongoza Maandamano ya Watanzania Wote kuitwaa ile haki yake aliopokwa hivyo kuingia Ikulu moja kwa moja!. Amshauri ninii abakie uhamishoni huko huko alipo na asithubutu kukanyaga tena Tz"!. ukimlisha maneno kama hayo, fasta ataibuka kuyatema!.

nimecheka kweli na huyo nanii akiamua kukanyaga Tanzania?
 
Back
Top Bottom