Mgomo Wa Madaktari: Jee, Serikali Kuwafukuza Kazi Kwa Summary Dismissal kwa "Insubordination"?

Wanabodi,
8. Kitendo cha mtumishi wa serikali, kukataa kutekeleza amri halali ya mkuu wake wa kazi, hiyo ni insubordination na adhabu yake ni summary dismissal!. Hivyo pamoja na genuinity yote ya madai ya madaktari, jee mgomo wao ni halali?, unafuata sheria za migomo kwa mujibu wa sheria zetu za kazi na maadili ya kidakitari?!.

Wasalaam

Pasco (wa jf)

Katika sheria mpya ya kazi, Industrial and Labour Relations Act-2004 hiyo kitu haipo na haitakiwi kusikika.
Badala yake kuna kitu kinaitwa "Termination of an Employment Contract". Na hii lazima ifuate Disciplinary Process kama ilivyoelezewa kwenye hiyo sheria.
 
hii serikali ya kidhalimu nakuambieni....Docs wastaafu wanaikubali huo mkwanja? aisee 5 solid years miksa sups kibao alafu unakuja kufanywa hamnazo inauma sana....
Kuna rafiki yangu amechange status, sasa hivi nina uhakika hajui hata sindano inashikwaje, yeye upumbavu huu alishaubaini miaka 4 iliyopita akaamuwa kujiunga na kampuni moja ya kigeni na anapiga pesa ndefu na mambo yake yapo super sana kama sio diesel.
Na nina uhakika saa hizi anapoliona hili saga Madaktari wenzake anacheka sana na anajiona ni kama Nabii ambaye aliona mbali sana.
 
hali si nzuri kwakweli, hivi ni madaktari wote wa vituo vya afya?au ni hopsitali za rufaa tu?
na je madaktari bingwa na registrars nao wamo katika mgomo?

naamini serikali itakaa na madaktari
 
Pasco!
Jambo usilolijua ni usiku wa kiza. Kanunue employment Act 2004 uisome na baada ya hapo anzisha thread upya.
Nenda na wakati. Anyway kuwafukuza kazi sio suluhisho ila ni sawa tu na mpumbavu anapoamua kwenda kulewa pombe ili apunguze mawazo na akiamka ngoma iko pale pale. Narudia WATANZANIA hawako serious. Kwa watu makini na if we had any opposition then nauona mgomo wa Madaktari ungekuwa ni chachu ya Mapinduzi ya umma. Kila mtu angegoma kufanya kazi kwani kwa kuwa matabibu wamegoma ukiumia una uhakika wa kufa kwani kuna mgomo. But nimefurahishwa na wale Doctors wa KCMC wao wameweka a functional strategy kwamba huduma za dharura zitaendelea kutolewa ila out patients hawatahudumiwa. That is professional ila hizi fujo za hao wa Dar sijui ni kinyume na kiapo chao. Let us do something tools down mpaka viwanja vya ndege tugome wote. Huyu Dr. Mponda ni mwongo na asulubiwe au apigwe mawe mpaka afe TRA wabslipwa kuliko Madaktari Kama anabisha alete data to prove that Doctors are the highiest paid civil servants.

Dr Mponda tunakuheshimu sana, ila kumbuka heshima ni kitu cha bure na kwamba cheo ni dhamana. Mbunge on call 200,000, dactari on call 10,000. Masikini wataalamu wa Tanzania, yaani wote wakagombee ubunge?
 
wewe pasco umetumwa kupima upepo ee?wakifukuzwa madaktari kada nyingine za afya zinaingia rasmi kwenye mgomo!!
kumbuka almost kila wilaya kuna M.D tofauti na miaka ya zamani,hawa wanaweza kutumika kuwashawishi mpaka walinzi kuingia kwenye mgomo.toka lini serikali ikaogopa kukutana na watu wake eti kisa hawana uhakika na usalama?huu ni upuuzi na muendelezo wa siasa za maji taka.chonde chonde pasco na kundi lako angalieni sana kwani kinachofuata ni maandamano ya wagonjwa na ndugu zao.kwa hiyo unategemea walipa kodi wakubali madaktari waliosomeshwa kwa kodi zao wafukuzwe kirahisi rahisi.
 
Sometime it takes a disaster of monumental propotion to change things. Serikali wajaribu kuwakufuza madaktari (hata kama sheria inawapa nguvu ya kuwakuza) ndio watajua fundi nani na kibarua ni nani.

Kwa upande mwingine serikali inaweza ikawa imezoea 'crying wolf' za walimu. Sasa wajaribu kuwasha baruti kwa hawa wadunga sindano kwa kisingizio cha some comical legal clause. Huu mgomo wa sasa ni cha mtoto. Itakula kwenu serikali.

Dawa hapa ni kwa mtu mzima waziri mkuu (hii issue imeshavuka ngazi ya waziri) kuwaangukia madaktari na kueleza nini wanafanya. Kukubali kosa sio dalili ya udhaifu, ni ukomavu na ujasiri.
 
So summary dismissal kwa serikali ni suluhisho rahisi kuliko madai ya huduma bora za afya? Well, let's wait and see. Kitu kimoja kiko wazi kabisa, kwamba kama madaktari watatishwa na wakatishika basi hiyo itakuwa disaster kwa umma na wataweka precedent kwamba vitisho vya serikali vinaweza kufanya kazi mahali popote pale kwenye sekta ya umma.

Kwa madaktari hawana choice bali kukomaa. Kila mwananchi yupo upande wao isipokuwa watawala wanaotibiwa India.
 
Altimutum hii na tishio la kuwafukuza kazi ni mpango wa Iron Lady Mama Blandina Nyoni, "never on earth to bow down on anyone!"!.
.....sifa za kijinga! Wait and see! go go go madaktari! watanzania tutawaunga mkono punde.
 
........... wataomba, kwa masharti yale yale waliyoyagomea!, na this time masharti yao ya ajira mpya yatatamka 'expresisly' not 'impliedly' ni marufuku kugoma, na ukigoma tuu jihesabu you have lost your job!.

Hapa pasco sasa unaaanza siasa....................... Kwani kuna ajira yeyote ile ambayo in the current form inakubali na kurusu migomo.migomo sio ya waajiri ni waajiriwa na ni option ya mwisho baada ya option nyingne zote kushindikana
 
wewe pasco umetumwa kupima upepo ee?wakifukuzwa madaktari kada nyingine za afya zinaingia rasmi kwenye mgomo!!
kumbuka almost kila wilaya kuna M.D tofauti na miaka ya zamani,hawa wanaweza kutumika kuwashawishi mpaka walinzi kuingia kwenye mgomo.toka lini serikali ikaogopa kukutana na watu wake eti kisa hawana uhakika na usalama?huu ni upuuzi na muendelezo wa siasa za maji taka.chonde chonde pasco na kundi lako angalieni sana kwani kinachofuata ni maandamano ya wagonjwa na ndugu zao.kwa hiyo unategemea walipa kodi wakubali madaktari waliosomeshwa kwa kodi zao wafukuzwe kirahisi rahisi.

Kama ungeisoma vizuri post yangu ya kwanza wala usingesumbuka akili yako na huyu Pasco wa JF. Huyu ana ushujaa wa kuparamia makaburi ya watu ili apate picha ya Dr Slaa na Kikwete badala ya kwenda kuzika! sasa wewe ndio unamshangaa leo kuja na hii cooked story?
 
Pasco mtumwa anaweza kulazimishwa kwenda asikotaka.
The deviding line ya wafanyakazi wa Tanzania na watumwa is very thin, Watumwa walinunuliwa kama bidhaa, wafanyakazi japo hawakununuliwa lakini wamejinunulisha na hawathaminiwi!. Pia watumwa, hawakulipwa, ila walikula bure na kulala bure, wafanyakazi japo wanalipwa, wanalipwa nothing, au peanut!, haitoshi kula, wala hawana mahali pa kulala!.
 
watu wakisikia mtu kagoma huwa wanauliza mgomo ni halali au siyo halali, sheria ya kazi ya Tanzania mpaka mgomo uwe halali hautakuwa ni mgomo tena au effective mgomo. ila kitu kingine cha kujiuliza ajira ni mkataba mwajiri ana wajibu wake na mwajiriwa ana wajibu wake, mwajiriwa akifanya kazi na mwajiri asipolipa mshahara nani kavunja mkataba? baada ya hapo inayofuata ni vurugu tu. kila mtu anastrugle 4 survival.
 
Sidhani kama serikali itakimbilia kuchukua uamuzi huo ambao kimsingi ni wa kijinga sana kama unavoonekana kupigia debe mkuu Pasco.I still believe watakaa nao na kumeet demands zao ambazo kimsingi ni very logical kwa ustawi wa sekta nzima ya afya kuanzia wenyewe matabibu na mgonjwa,besides tuna madaktari wengi hivo jobless mitaani ambao watawaajiri?au ndo kama alivosema Blandina wataajiri wageni kutoka nje ya nchi?
 
  • Wakuu ebu mwenye official statemt ya madai na malamiko ya madaktari aweke hapa
  • @Pasco tumia nguvu uliyotumia kutafuta picha ya Slaa na Jk kumoba dk slaaa aje hapa atupe msimamo na kauli ya chama chake
 
@Pasco

Naweza kukuridisha nyuma je unaweza kutuwekea hapa Nini hasa madai ya madaktari? Maana ukiona wasomi nao wanakuwa wanasiasa tujue nchi inakwenda pabaya. Na before gmo jithada gani zimefanyika zkashindindwa kuzaa matunda . itapendeza tupate pcha ya pande mbili zote za shilgi. so far naona madakatari wanaaibsha taaluma yao na wamekuwa "wabinafsi" sana.

@ CDM na vyama vingine vya SIASA

Alafu CHADEMA na vyama vyote vya siasa wanatakiwa watoe tamko na msimao wao wa chama juu ya mamba kama haya.

Wasidhani hili ni jambo la CCM tu. Yes CCM inangoza serikali lakini iliyogoemwa ni serikal . Na CDM au CUF wanaweza kuongoza Serikali siku moja . Hii ni wish ya kilwa mpenda mabadiliko na mm nikiwa mmoja wao

Dr Slaa, Mtatiro, au waemaji wenu wa mambo ya afya watanzania tunataa kusikia msimamo wenu Offcial.

alafu Pasco kwa uchokozi wangu zaidi baada ya kutafuta picha ya madokta wawili ukakosa tafadhali mtafute Dk slaa na muulize kuhusu hili. ikiwezekana aapata muda aje atupe msimamo wake (wa chama) kwenye hii thread. Au mtu yeyote mwenye acess na CHADEMA awaambie watoe tamko rasmi

Mara nyingi vyama vya upinzani hawatoi mbinu kwa serikali jinsi ya kutatua migogoro ya kila siku. Wao ndio wenye ridhaa ya wananchi na si ndio wanaokusanya kodi. sana sana vyama vya upinzania vitasema mkae nao na muwatimizie masharti yao, ili mambo yaendelee.
 
Issue hii imepata support kwa kila muajiriwa wa Serikali labda ukitoa TRA na sekta zingine ambazo mishahara yao na marupurupu yao ni mazuri (per DM na Over time). Ila kifupi ni kuwa Salary scale za nchi hii ni za kipuuzi ambazo taaluma haizingatiwi hata chembe... Kinachoangaliwa ni Taasisi gani unayofanya kazi....

Inakua ngumu kuona umemaliza six na mshikaji ambae umempa tafu sana Class then kwenye selection wanaangalia mwenye matokeo mazuri asome nini. This means ili ufanye Medicine kwa sasa wanahitaji DIV 1 kama sikosei then na kama hukupata matokeo hayo waweza omba kozi ingine somewhere else. Shule ya ma MD ni ngumu sana vitabu vyao ni vikubwa sana then wanaspend 5years Class and a year as Intern... Unamaliza suluba zote hizi mtu nakuja kukupa laki nane au tisa kwa mwezi???? Then jamaa aliepiga DIPLOMA yake ya KODI tena kwa miaka miwili au mitatu anaenda TRA analamba M kadhaa every moon... Inauma sana.

Serikali haiwezi fukuza Madaktari koz so far hawatoshi na bado wagonjwa wataendelea kuongezeka koz maisha hatarishi yanazidi kuongezeka daily... Nani mwenye uwezo wa kula chakula Bora kwa sasa??? (MLO KAMILI????) ni wachache mno... Hali ni mbaya sana so wagonjwa wataongezeka zaidi ya sasa.....

Kilichopo ni Serikali kuangalia upya scale zake za mishahara kwa watumishi wake...na kama madaktari watapandishiwa salary I bet sekta zingine zitagoma koz watajua ni possible if and only if TUTAGOMA...
 
Pasco, naomba uipitie employment act tena kujua nini ni insubordination. Kuhusu kufa anapanga Mungu, don't give me that crap! Wananchi wanakufa vifo ambavyo vingezuilika kama hawa watawala wetu wangekuwa wako timamu.

Madaktari kazeni, pengine ndio mwanzo wa mwisho wa baadhi ya watu.
 
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.

Hivi kuna anaejua ni kwa nini madaktari hawataki kwenda kwenye ukumbi ulioandaliwa na serikali? Na je ni kweli ukumbi unaotumiwa na madaktari kufanya mikutano yao ambako ndiko wanaitaka serikali ikawasikilize huko hauna usalama?na ni kweli hakutakuwa na usalama wa viongozi hao?kwani serikali inamwogopa mwananchi wake huku ikiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama?lakini pia siamini kama hawa madaktari hawana uwezo wa kutambua hili la kuitwa na wao wakakataa kutumia ukumbi unaoandaliwa na serikali.lazima kuna kitu,na huenda watu kama nyinyi kina pasco mmeshaanza kutumia mbinu za kuwatisha kwa kusambaza taarifa za kuwafanya wawe weak kwenye madai yao.naona pia kuna element za kuwalaumu madaktari eti wamemgomea mwajiri wake,mara wana ubinafsi,hivi ni kweli?nani yuko tayari kuifanyia kazi serikali bila kulipwa?na je madai yao ya kutaka hospitali ziwe na vifaa ni potofu,wao kudai nyumba kama makubaliano yao na mwajiri ni ujinga?je posho zao za kufanya kazi muda wa ziada nao ni upuuzi?kwanini juzi spika ,naibu spika wamejitokeza kutetea posho,ni vipi wabunge wa CCM mapovu yaliwatoka pale wabunge wa CDM waliposema posho sasa basi?leo wao madaktari kwa kuwa wanatibu watu hawastahili kulipwa madai yao?tena mtu mwingine anawajibu kwa dharau na kejeli.mi nadhani Summary dissmisal sio suluhisho kabisa la madai ya madaktari,tujiulize vizuri kabla ya kushabikia kwa kificho hili suala la mgomo wa madaktari,lakini pia tuangalie hali ya migomo hapa nchini,kila kukicha utasikia walimu,mara wanafunzi,mara kiwanda hiki,nini tatizo?na je solution yake ni nini?je ni SUMMARY DISSMISAL?
Tatizo ni serikali yetu na sisi wananchi,kwa hiyo tatizo limeshakuwa kubwa maana liko kwenye aspect mbili at a go.ni afadhali wananchi tusingekuwa wabovu tungeweza kukomesha migomo hii,lakini serikali mbovu na wanachi wabovu unategemea nini hapo?
na ndio maana mtu leo anakuja na hoja ya kushabikia kufukuzwa kazi kwa madktari,japo amekuja underground lakini hakika ni ushabiki huo.
Naumga mkono mgomo wa madktari kwani ni njia iliyo karibu na kupata haki zao,japo sio njia sahihi.
 
Mara nyingi vyama vya upinzani hawatoi mbinu kwa serikali jinsi ya kutatua migogoro ya kila siku. Wao ndio wenye ridhaa ya wananchi na si ndio wanaokusanya kodi. sana sana vyama vya upinzania vitasema mkae nao na muwatimizie masharti yao, ili mambo yaendelee.


Sio kutoa mbinu wanataiwa isue za kitifa ama hizi watoe tamko. Either waipnde seriali inavyodeal na abo au wawaponde madakatai au wawaombe wote wakae mezani maana wananchi ndo wanaumia.

CDM kukaa kimya sio ishara nzuri kwa chama chenye serkali kivuli bungeni. demokrasia inawahitaji watoe tamko.

la sivyo tutajua na CDM hawana njia wala hawajui ni jinsi gan ya kudeal na matatizo kama haya.........

Ukisema vyama vya upinzani hawati mbinu ina maana hata hotuba za bajeti kivuli na mengineyo na hata Ruzuku wanayopta ni ya kazi gani? Ni wajibu na jukumu lao kusema hiki mmekosea tungekuwa sisi tungefanya hivi.
 
It is easy for the government to do that. However, the consequences would not justify this course of action. I would consider this option to be borne of lack of wisdom.

I can see the starting of Tahrir square because teachers will follow suit and that will be the end of this government.

Ideally, there is a genuine case of malaise among the government officials handling the Drs issues. Instead of punishing the officials they turn to victims. This is a typical symptom of excessive abuse of power. Hawajui kuwa sio enzi za chama kimoja sasa na kuwa Mtanzania wa jana sio wa leo.

Watanzania wanajua kuwa hao viongozi wanaotoa maamuzi watafanya hivyo kwa kuwa hata wakiugua mafua wanapelekwa Appollo India. Hivyo, wananchi wanaweza kufa tu kuliko kumuwajibisha Blandina, Haji, Mtesigwa na Lucy. Hawa thamani yao ni kubwa kuliko Watanzania wote.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom